Zijue faida mbalimbali za kula papai kiafya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.

Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.

Wiki mbili zilizopita tumeona vyakula kama karanga, korosho vinavyoweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, wiki hii pia tunaona papai nalo limo kwenye orodha ya vyakula vinavyotoa kinga ya ugonjwa huo.

Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.

HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.

KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.

KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya âbeta-caroteneâ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k

NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.

TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.

MICHANGO MINGINE KUTOKA KWA WADAU WA JF
 
Tatizo letu wadanganyika wengi hatuli kabisa matunda, akili zetu tumehamishia kwenye bia, nyama choma na ngono.
Ni kweli Kabisa Kaka,hatupo serious na Chakula,hatuzingatii kabisa nn tunakula na kwa nn,sisi tunajilia tu ili mradi tushibe!! Na sehemu kubwa ya budget ya wanaume wengi wa kitanzania huenda kwenye Ngono,Pombe na yatokanayo!!!
 
Thanks for the useful thread ... binafsi napenda sana papai & nanasi
 
Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake.
Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda la papai lina faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

UTAJIRI WA VITAMINI
Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalo liweka tunda hili katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamin.
Mti wa papai​

FAIDA ZA KIAFYA ZA TUNDA LA PAPAI

Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa :


Mbegu za Papai
1. Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni
2. Kutibu Udhaifu wa tumbo
3. Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
4. Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni

Mizizi Ya Papai​

5. Kutibu Kifua kikuu
6. Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
7. Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
8. Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
9. Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)

Majani Ya Mpapai

10. Pia yanasaidia kutofunga choo
11. Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.

12. Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 12 kwa siku 5.

13. Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.

14. Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.

15. Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.

16. Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.

17. Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.

18. Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5.
 
Aiseee, asante sana nina mipapai nje ya nyumba hapa lakini nakula papai tu mengine wala siyajui. Ubarikiwe mkuu.
 
Hizi ni baadhi ya faida ambazo unaweza kuzipata kwa kula papai au kunywa juisi yake

Papai lina fibrin ambayo hupunguza kuganda kwa damu

Fibrin inaweza kuzuia kiharusi

Lycopene iliyomo katika papai inaweza kupunguza hatari ya kansa ya kibofu

Mbegu za papai hutibu homa ya matumbo (typhoid)

Juisi ya papai huondoa sumu mwilini
Juisi ya papai hutibu vyema shinikizo la damu
Juisi ya papai husaidia kuzuia magonjwa ya moyo

Juisi ya papai ina folate, vitamini C na E ambavyo huzuia saratani ya utumbo.

Juisi ya papai hujenga kinga ya mwili
 
hapohapo nina swali mkuu!!! je mtu ambaye tayari anakiharusi,papai linaweza kumsaidia kupona kiharusi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…