Zijue faida mbalimbali za kula papai kiafya

Zijue faida mbalimbali za kula papai kiafya

hapohapo nina swali mkuu!!! je mtu ambaye tayari anakiharusi,papai linaweza kumsaidia kupona kiharusi??
kiukweli sidhani ila nachojua mazoea ya kula papai mara kwa mara yanapunguza kupata kiharusi kwa asilimia fulani
 
hapohapo nina swali mkuu!!! je mtu ambaye tayari anakiharusi,papai linaweza kumsaidia kupona kiharusi??
sijui kama kakujibu ila nadhani jibu ni hapana matunda yanatusaidia kutukinga na magonjwa ukishapata magonjwa dawa halisi zinahusika.
 
kiukweli sidhani ila nachojua mazoea ya kula papai mara kwa mara yanapunguza kupata kiharusi kwa asilimia fulani
umemjibu sahihi papai linazuia kiharusi ukishapta utafuata utaratibu wa matibabu kulinga na plan ya dokta wako.
 
Hizi ni faida za kiafya za kula tunda papai

Papai ni katika matunda yayayopatikana maeneo mengi duniani. Tunda hili limekuwa likizungumziwa sana na watoaji wetu wa tiba za kiasili na hata za hospitalini. Yapo matunda mengi sana yenye sifa hizi za kutajwa katika nyanja za tiba ama vile ndimu, limao, nanasi, komamanga, pensheni, maembe na machungwa na mengineyo. Hata hivy zipo pia mboga ambazo zinatajwa katika nyanja za kiafya kama uyoga, kabichi, karoti, vitunguu, nyanya na pilipili. Katika makala hii tutakwenda kuona tu faida za papai na namna luinavyotajwa katika nyanja hizi za afya. Makala hii itaangalia kwa ufupi faida hizo bila kuingia ndani zaidi na kuwachosha wasomaji.

1. Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.

2. Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hii husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).

3. Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchuja miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

4. Papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Hupunguza hatari ya kuuguwa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.

5. Ulaji wa antioxidanti zilizopo kwenye papai kama beta-carotene husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratan kwa vijana. Ulaji wa tunda hili husaidia katika kudhibiti upatikanaji wa saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.

6. Papai ni katika matunda yenye vitamini K ambavyo ni muhimu katika afya ya mifupa. Hivyo ulaji wa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa na kudhibiti kupasuka kwa mifupa. Vitamin k pia husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo. Kumbuka madini haya pia ni muhimu katika kuimarisha na kudhibiti afya ya mifupa.

7. Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa papai ni tunda zuri kwa wenye kisukari. Papai ni katika vyakula vyenye maji kwa wingi. Tafiti zinaonesha kuwa watu wenye kisukari type 1 diabetes wameweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini mwao. Wakati huohuo watu wenye kisukari type 2 diabetes wameweza kuimarisha kiwango cha sukari mwilini pamoja na kiwango cha homoni ya insulin.

8. Ndani ya papai kuna enzyme zinazoitwa papain hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pia kama tulivyo sema papai lina maji nmengi na kambakamba vyote kwa pamoja husaidia katika upatikanaji wa choo na kusaidia katika kudhibiti mmeng’enyo wa chakula.

9. Madini ya potassium (aina ya chumvi) na vitamini vilivyomo kwenye papai husaidia katika kulinda afya ya moyo dhidi ya maradhi hatari yanayoshambulia mfumo wa usukumwaji wa damu. Ulaji wa madini haya wakati huohuo ukiwa unapunguza ulaji wa madini ya sodium (chumvi hii tunayotumia) husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi hatari kama shambulio la moyo, presha na kiharusi (stroke).

10. Ndani ya papai kuna chembechembe ya Choline, haya ni muhimu katika kusaidia miili yetu hasa kulala, kujongea kwa misuli (kukunja na kukunjuka, kutanuka na kusinjaa). pia husaidia katika kulinda mpangiliuo wa utando wa seli, husaidia katika kutunza kumbukumbu pamoja na kujifunza yaani kusoma. Pia husaidia katika ufyonzwaji wa fati (mafuta).

Kwa ufupi papai lina matumizi mengi sana kama ukuaji wa nywele na kuzifanya zing’ae, kupona kwa vidonda, ukuaji wa tishu na ukuaji wa mwili kwa ujumla. Na haya yote ni kutokana na kuwepo kwa vitamin C na vitamin A.

Mwisho nimalizie kwa kusema kuwa matunda ni dawa. Ni vyema kujitahidi kula matunda na mboga za majani mara kwa mara. Pia viungio vya mboga kama vitunguu, tangawizi, bamia na karoti viungio hivi ni muhimu sana. Makala hii imekusanya maelezo kwa uchache. Hivyo ni vyema kuongezea maarifa sehemu nyingine ili upate ufahamu zaidi kuhusu ubora wa matunda na mboga mbalimbali.

PAPAI.png
 

Attachments

Back
Top Bottom