Zijue faida na hasara za kuajiriwa

Zijue faida na hasara za kuajiriwa

FAJES

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
720
Reaction score
644
Faida za Ajira:
1. Uhakika wa kipato kwa kila mwezi. Haijalishi hali ya uchumi imepanda au imeshuka, kipato kinabakia palepale.
2. Uhakika wa matibabu kupitia BIMA YA AFYA.
3. Kupata connections mbalimbali za Wadau.
4. Kuwa na uhakika wa kupata MKOPO kwa dhamana ya ajira yako.
5. Kuwa na social capital.

HASARA.
1.Kuwa mtumwa kwa mwajiri (kukosa uhuru wa kuamua wapi uishi, lini usafiri, kazi gani ya ziada ufanye)

2.Kuendelea kuishi maisha fukara maana kwa kawaida mwajiri hulipa mshahara wa mfanyakazi aweze kula na kuvaa na siyo kuendelea kimaisha kwa kumiliki mali. Chunguza Wafanyakazi wengi utapata majawabu.

3.Kuishi maisha yenye stress na hofu wakati wote kwa kuhofia mwajiri wako atasema nini juu yako kwa kesho yako.

4.Kuishi maisha yasiyo na furaha na Amani, haswa Mama na Baba mnapokuwa waajiriwa katika sehemu tofauti.

5. Kuwa mtumwa wa madeni na mikopo. Waajiriwa wengi hukopa kufanya ujasiriamali ili hali hawana nafasi ya kusimamia miradi wanayoianzisha na hivyo kuishia kuwa watumwa wa mikopo na madeni baada ya hasara wanazopata mara kwa mara.

Ni juu yako kuchagua aina ya maisha unayohitaji.!
 
Upo sahihi ila hasara hizi unaweza kuzipata zaidi endapo uta ajiliwa na mtu binafsi especially kama haihisiani na elimu yani ilimradi ujue tu kusoma na kuandika aisee utajutaa wale wazee wa 7000 kwa muhindi inakua kazi ku make yaani ukipata hiyo pesa unaishia kula tu.
 
Stress nyingi za watumishi ni kujitakia...Sasa unakopa halafu unanunua furniture za ndani au unakopa unaenda kuolea ili iweje!!baadae deni linakuwa kubwa unaanza kupagawa boksa unaivalia kichwani....Eeenh bwana eenh kuajiriwa kuna raha yake asikuambie mtU kitu....Sipo serious kivile!
 
Naomba zijue hasara za kuajiriwa:-
1. Lazima uamke kwa lazima kwa wakati ulio pamngiwa.
2. Lazima ufuate na ufanye kile ambacho kuna mtu alisha kifikiria na kuki create.
3. Hauwezi ukawa na uhuru kama sisi wakulima.
4. Lazima uwe mtiufu kwa kila bosi wako hata kama anakuonea.
5. Hauwezi ukapombeka hadi muda wenye unataka.
6. Marufuku kwenda kazi ukiwa umelewa.
7. Unaishi na utaishi kwa hofu na mashaka kwamba muda wowote unaweza ukafukuzwa kazi.
8. Ukiamka na mning'inio lazima uende kazi huku kichwa kinakuuma.
9. Unakua na kama umeolewa na alie kuajiri.
Anyway.........
Ngoja niishie hapa
 
Sio kila mtu ajiajiri
 
Mimi nimeajiriwa....nimegundua kitu kimoja ambacho kinanikwaza...na chenye thamani zaidi ya pesa...UHURU...kuna siku mtu.unajuskia huna hamu tu yakutoka saa 11 alfajiri lkn huna namna....unaweza ukawamiss.ndugu zako wa mkoani etc
.lkn sasa ukiwaza hizo process na mashartu dah....

Mzazi anaweza akakupigia anaumwa na ukweli akawa anaumwa lkn movement ya harakaharaka kwenda mkoani utata.....UHURU dah
 
Kuajiriwa ni mateso makubwa sana....hasa hasa kwa watu wenye elimu ndogo yan kaz zao ni za kipato kidgo.....ni manyanyaso makubwa yasiopimika
 
Ukiajiriwa Bosi ndo anakupangia cha kufanya iwe kwa hiari au kwa lazima ni lazima ufanye tu utimize lengo lake.
 
Kwa awamu hii ya magufuli, tuliochukua uamuzi wa kuacha kazi na kujiajiri, kuna wkt unafukiria bora ungebaki na ajira yako.

Mzunguko mdogo sana, watu wengi wanakopa, pesa ngumu kupatikana na ikipatikana thaman yake ndogo sanaa
Jaribu kufight nje ya nje kama una professional
 
Ukiajiriwa pasipo na wizi kutegemea salary tu unapoteza mda wako heri kafungue kibanda cha chipis,utaishia kurithisha umasikini vizazi vyako
 
Mimi nimeajiriwa....nimegundua kitu kimoja ambacho kinanikwaza...na chenye thamani zaidi ya pesa...UHURU...kuna siku mtu.unajuskia huna hamu tu yakutoka saa 11 alfajiri lkn huna namna....unaweza ukawamiss.ndugu zako wa mkoani etc
.lkn sasa ukiwaza hizo process na mashartu dah....
Mzazi anaweza akakupigia anaumwa na ukweli akawa anaumwa lkn movement ya harakaharaka kwenda mkoani utata.....UHURU dah
Kukosa UHURU wa kufanya jambo unalohitaji kwa muda muafaka tayari ni kuingiliwa kwa uhuru binafsi ktk maisha yako, kwa lugha rahisi ni kuwa " mtumwa" bila ya kujitambua. Kuwa mtumwa ni "manyanyaso" na kuingiliwa uhuru binafsi wa kuishi.
 
Stress nyingi za watumishi ni kujitakia...Sasa unakopa halafu unanunua furniture za ndani au unakopa unaenda kuolea ili iweje!!baadae deni linakuwa kubwa unaanza kupagawa boksa unaivalia kichwani....Eeenh bwana eenh kuajiriwa kuna raha yake asikuambie mtU kitu
No wonder kwny avatar yako umepiga picha kwenye baiskeli hapo na umeridhika na maisha hayo.
 
kuajiriwa ni kugumu wakuu acheni tu! mara mia ukauza pipi zako ukiwa na uhuru kuliko kuajiriwa na bosi anayekuchukulia kama kamdudu fulani hivi! Uhuru siyo kitu cha kuchezea wakuu.
 
Back
Top Bottom