Zijue faida za kuoga mwili mzima kiafya

Zijue faida za kuoga mwili mzima kiafya

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
Je wewe ni miongoni mwa watu wanaokwepa maji, kila ukiwaza kuoga unapata uvivu na kuogopa baridi?
Kuoga kuna raha yake na kuna manufaa makubwa katika maendeleo ya mwili wa binadamu.

Sasa leo hii tuangazie umuhimu wa kuoga, sio kuoga tu yaani kuoga mwili mzima kiafya na kiakili.
Hizi hapa faida za kuoga mwili mzima kwa mujibu wa wataalamu.

1.kwa mujibu wa Dkt Zack wa Cleveland Clinic ya Ohio Marekani kuoga hususani maji ya vuguvugu kunasaidia kupata usingizi wa haraka na uliokamilika.
Anasema wakati wa mchana mwili unapata Sana joto hivyo wakati wa kulala ukifika inahitaji kupunguza nyuzi joto mbili au tatu ili kupata uwiano sahihi wa joto la mwili ambapo kuoga ndio suluhisho.

2.Dr Zack pia anasema kuoga kunasaidia kuponya majeraha ya mwili kwa kuyafisha na kuondoa wadudu mithiri ya bakteria ambao husalia kwenye ngozi, ndio maana hata watu wenye vidonda hushauriwa kuonya vidonda vyao kwa maji ya vuguvugu.

3.Kuoga pia kunasaidia kuupoza mwili kwa kuondoa uchovu kwa kuifungua ngozi na kufanya mfumo wa utoaji taka mwili kuwa katika hali nzuri zaidi hivyo kuuweka mwili katika hali ya utulivu zaidi.
4.Jarida la Pinner Bathing linaeleza kuwa kuoga kubaboresha mfumo wa upumuaji hivyo kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo pamoja na shinikizo la damu.

Hata hivyo kwa mujibu wa Dkt. Zack kuoga kunaweza kuwa na madhara kwa binadamu hivyo chukua tahadhari zifuatazo.

Usioge kila siku ili kuepuka madhara ya ngozi ikiwemo kuwa na ngozi kavu kwa sababu kuoga kunaweza kuondoa mafuta asilia yanayokuwa kwenye ngozi ya binadamu.

Pia epuka kutumia maji ya moto, tumia maji ya vuguvugu yasiyozidi nyuzi joto 40 kwenye kipimo cha sentigredi ili kuepuka kuuchosha na kuunguza mwili.

Weka taulo lako katika hali ya usafi ili kuepuka madhara ya maambukizi ya magonjwa ya ngozi.

Na usisahau kujikausha mwili kwa kujifuta baada ya kuoga.

© Peter Mwaihola.
Photo_1745818706308.png
 
© Peter Mwaihola.View attachment 3318333
Kupiga povu la mwili Muhimu sana!
 
Back
Top Bottom