Zijue faida za mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kipindi cha ujenzi na mara baada ya ujenzi kukamilika


Ukisoma Faida za mradi huu Unawalenga watanzania wote bila kubagua na ni mali ya watanzania...
Sio yale mazingaumbwe ya bagamoyo na makanjanja wa kichina
 
Nimependa Issue ya Local Content, Kuanzia suala la Saruji, Nondo mpka Kuwashirikisha Contractors Wazawa kujifunza! Bravo
 
SGR NI KITU CHA MAANA MNO KWA USTAWI WA NCHI NA VIZAZI VYOTE JAPO HAVIKUWEPO KWENYE PLAN LAKINI NI VYA UMUHIMU SANA.TUNAOMBA SERIKALI HII RELI IKAMILIKE MPAKA MWANZA NA YA TABORA KIGOMA KALEMA MPANDA IKAMILIKE PIA KABLA YA 2023 HATA YA DAR...ARUSHA NA DAR MBEYA...TUTAPATA MACHUNGU LAKINI HIVYO VIKIKAMILIKA UCHUMI UTAKUWA KWA ASILIMIA 18%
 
Unajua kumwambia mwanao faida ya kujenga nyumba ya kisasa wakati ana njaa sijui kama atakuelewa!!
 
It doesn't matter,hizi fursa huwezi kulinganisha na bandari.
Halafu acha kuongelea micro stuffs,hiyo SGR ikikamilika hizo ajira 8000+ zitaendelea kuwepo?
 
Nyie Wakuda TRC Nasikia Kichwa chenu cha Majaribio Kutoka UTURUKI kilicholetwa na Yapi Merkezi kimepinduka!!!
 

Hivi bado mnadanya watu kwamba mtafufua reli ya Tanga- Arusha? Au mnaandika muhalalishe kulipwa mishahara? Hiyo reli ya Sgr mpaka sasa imefikia asilimia ngapi toka Dar- moro na moro-Dom?
 
Bomba la mafuta mali ya Uganda ni vipi unawafanyia maamuzi ya mauzo! Kumbuka hili si bomba la kwanza nchini, lipo linatoka Dar es Salaam mpaka Zambia humo mote linamopita ikiwepo Mbagala, Chalinze, Morogoro, Iringa, Mbeya na Songwe hakuna fursa zozote juu ya bomba zaidi ya marufuku!
 
Tupo Kwenye Light Track
Tanzania Kwasasa Ipo Vema Maendeleo Hayana Chama
 
Hivi bado mnadanya watu kwamba mtafufua reli ya Tanga- Arusha? Au mnaandika muhalalishe kulipwa mishahara? Hiyo reli ya Sgr mpaka sasa imefikia asilimia ngapi toka Dar- moro na moro-Dom?
Mradi wa Ufufuaji wa Reli ya Tanga - Moshi - Arusha unaendelea. Kwa sasa umefika Zaidi ya 70%
 
siku ya Leo nitatumia muda mwingi sana kuelimisha watu ujumbe huu. kwa kweli tunahitaji sana watu wapate elimu.
 
Nataka utueleze kwa nn mnadhani hii SGR haitakumbwa na matatizo ya uendeshaji kama ilivyo kwa TAZARA au Reli ya kati na ile ya Tanga Arusha?

Watanzania tunashida sana ya kusimamia miradi hasa mikubwa. Tumeona kwa BRT, ATCL n.k. Ni muijiza gani mtafanya ili msikwame kama hao wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…