Zijue faida za Pombe

Zijue faida za Pombe

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Kama ulikua hujui faida ya POMBE MWILINI wacha nikufahamishe;-
Kila kitu hapa duniani kina faida na hasara,
Sasa leo wacha nikufahamishe faida ya kunywa pombe,
Lakini kabla sijakuletea faida ya pombe mwilini,
Wacha kwanza nikufahamishe pombe ni nini,
Pombe ni neno ambalo linajumuisha aina zote za vilevi unazozifahamu,
Kiafya mwanaume anatakiwa anywe pombe zisizo zidi chupa mbili kwa siku,
Wakati mwanamke anatakiwa anywe chupa moja.

FAIDA ZA POMBE

1) HUPUNGUZA HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA MOYO

Unywaji wa pombe kwa kiasi huongeza aina fulani ya lehemu nzuri inayoitwa high density lipopoprotein,
Lehemu hii hulinda moyo lakini pia pombe hulainisha damu,
Na kuifanya iwe nyepesi hivyo kupita kirahisi kwenye mishipa ya damu na kuzuia presha na kiharusi,
Lakini pia kwa kiasi fulani huzuia ugonjwa wa moyo.

2) HUONGEZA UMRI WA KUISHI.

Pombe huongeza umri wa kuishi kwa asilimia 18% zaidi ukilinganisha ja wale wasiokunywa.

3) HUONGEZA NGUVU ZA KIUME.

Pombe huongeza nguvu za kiume kwa asilimia 25% zaidi ya wale wasiokunywa,
Waokunywa pombe ni mashaihidi wa hili kwamba,
Muda ule ukiwa umekunywa pombe hamu inakua juu sana,
Na ukipata mwanamke unafanya vizuri zaidi kuliko ukiwa hujanywa,
Ikiwemo pamoja na kuchelewa sana kufika kileleni na kua na uume wenye nguvu sana kuliko kawaida.

4) HUPUNGUZA HATARI YA KUPATA KISUKARI.

Unywaji wa pombe kwa kiasi huongeza uwezo wa homoni ya insulini kufanya kazi vizuri,
Ambapo hali hii hupunguza hatari ya kupata ugonjwa hatari wa kisukari.

5)HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA UGONJWA WA AKILI.

Unywaji wa pombe kwa kiasi kinacho hitajika,
Hupunguza wa asilimia kubwa kuugua ugonjwa wa akili.

6) HUZUIA KUPATA MAWE KWENYE NYONGO.

Ugonjwa huu kitaalamu unaitwa gallstones,
Pombe hupunguza sana mtu kupata ugonjwa huo.

7) HUUPA MWILI MADINI MUHIMU.

Pombe ina madini muhimu yanayo hitajika mwilini,
Kwasababu pombe nyingi zina vitamin B nyingi aina ya thiamine na riboflavin,
Lakini pia zina calcium na magnesium nyingi,
Ambayo ni muhimu sana kwa jili ya kazi mbalimbali za mfumo wa mwili wa binadamu.

8) POMBE NI MZURI KWA WANAWAKE WENYE ZAIDI YA MIAKA 50.

Baada ya umri wa miaka 50 mwanamke huanza kupata dalili za kupungua kiasi cha homone mwilini kitaalamu kama monopause,
Hali hii husababisha mwanamke kubadilika tabia,
Ikiwemo mwili kuwa na joto zaidi au kushuka zaidi,
Pia wanawake wengine hupatwa na msongo wa mawazo,
Sasa utafiti unaonyesha kwamba kemikali zilizopo ndani ya bia,
Zinaweza kufanya kazi ya kuondoa hali hiyo inayo sababishwa na monopause.

9) HUONGEZA KUMBUKUMBU.

Kama wewe ni mnywaji wa pombe utaamini hiki ninacho kisema,
Kwani mara nyingi ukinywa unaanza kukumbuka mambo ya zamani sana.

10) HUSAIDIA FIGO.

Unywaji wa pombe kwa kiasi kinachotakiwa,
Kunapunguza hatari ya kupata mawe ya figo kwa asilimia 30% zaidi,
Kuliko wale ambao hawanywi pombe kabisa,
Hii ni kwasababu wanywaji wa pombe hukojoa sana na kusafisha figo.

NB;- Faida hizi hupatikana tu kwa wale wanaokunywa pombe,
Kama nilivyoelekeza hapo juu kwa maana ya kiasi kinachohitajika tu kiafya,
Nasio kwa watu wanaokunywa pombe kupitiliza,
Unywaji wa kupitiliza una madhara makubwa sana kiafya.
1000003879.jpg
 
Hasara za pombe
1.Huongeza uwezekano wa kuugua ugonjwa wa kisukari

2. Huongeza uwezekano wa kuugua BP

3. Huleta aibu na fedheha kwa mnywaji katika jamii.

4.Hupunguza kumbukumbu

5. Huchangia ugonjwa wa figo

6. Huchangia ugonjwa wa ini

7. Huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa akili

8. ...

9......
 
Hasara za pombe
1.Huongeza uwezekano wa kuugua ugonjwa wa kisukari

2. Huongeza uwezekano wa kuugua BP

3. Huleta aibu na fedheha kwa mnywaji katika jamii.

4.Hupunguza kumbukumbu

5. Huchangia ugonjwa wa figo

6. Huchangia ugonjwa wa ini

7. Huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa akili

8. ...

9......
hii nayo ni kweli
 
hata pombe za kienyeji nazo kuna feki?
Sawa, lkn kiujumla pombe zote hazifai,hasara ni kubwa kuliko faida,aloeleza mleta mada hapo,yageuze kinyume chake ndo utaelewa, yaani anaposema huzuia BP ,sivyo ilivyo bali uchochea mtu kupata hiyo BP.
 
Vipi kuhusu ulevi wa bangi nao una faida? Kuna mche wa bangi umeota sambamba na majani mengine mbele ya nyumba. Kutokana na umaarufu wa mmea huo nafikiria kuukata pamoja na nyasi zingine au kuupalilia ubaki kama ua tu ila nahofia ukionwa nitahisiwa nimeupanda makusudi mmea huo kumbe umejiotea wenyewe huenda mbengu ya mbegu ilindokea eneo hilo na wavuta bangi. Mind kwamba bangi situmii ila nauona mmea huo kama ua tu na jinsi ulivyo maarufu kwa mtazamo hasi. Ningepata na mmea wa tumbaku vikae pamoja ongeza na mrungi ndio mimea ya kilevi hiyo, hutazamwa kama mihadarati na sheria ya kukutwa nayo ni kali itahesabika kuwa umekutwa na madawa ya kulevya, ila kwa tumbaku haina sheria kali japo ni kundi moja la mimea ya kulevya
 
Vipi kuhusu ulevi wa bangi nao una faida? Kuna mche wa bangi umeota sambamba na majani mengine mbele ya nyumba. Kutokana na umaarufu wa mmea huo nafikiria kuukata pamoja na nyasi zingine au kuupalilia ubaki kama ua tu ila nahofia ukionwa nitahisiwa nimeupanda makusudi mmea huo kumbe umejiotea wenyewe huenda mbengu ya mbengu ilindokea eneo hilo na wavuta bangi. Mind kwamba bangi situmii ila nauona mmea huo kama ua tu na jinsi ulivyo maarufu kwa mtazamo hasi. Ningepata na mmea wa tumbaku vikae pamoja ongeza na mrungi ndio mimea ya kilevi hiyo, hutazamwa kama mihadarati na sheria ya kukutwa nayo ni kali itahesabika kuwa umekutwa na madawa ya kulevya, ila kwa tumbaku haina sheria kali japo ni kundi moja la mimea ya kulevya
Tumbaku ni hatari kwa afya yako ,sio dawa ya kulevya.
 
Sasa watu wakinywa pombe ili tu kujilinda na magonjwa na kuongeza mahitaji fulani ya mwili si ndio nchi itakuwa na walevi wengi walioharibikiwa akili na afya?
 
Vipi kuhusu ulevi wa bangi nao una faida? Kuna mche wa bangi umeota sambamba na majani mengine mbele ya nyumba. Kutokana na umaarufu wa mmea huo nafikiria kuukata pamoja na nyasi zingine au kuupalilia ubaki kama ua tu ila nahofia ukionwa nitahisiwa nimeupanda makusudi mmea huo kumbe umejiotea wenyewe huenda mbengu ya mbegu ilindokea eneo hilo na wavuta bangi. Mind kwamba bangi situmii ila nauona mmea huo kama ua tu na jinsi ulivyo maarufu kwa mtazamo hasi. Ningepata na mmea wa tumbaku vikae pamoja ongeza na mrungi ndio mimea ya kilevi hiyo, hutazamwa kama mihadarati na sheria ya kukutwa nayo ni kali itahesabika kuwa umekutwa na madawa ya kulevya, ila kwa tumbaku haina sheria kali japo ni kundi moja la mimea ya kulevya
Mkuu bora uukate tu!
 
Mimi sitakaa nitie pombe kinywani mwangu....nina sababu mujarabu ila bahati mbaya nina uraibu wa kunywa kahawa....
 
Back
Top Bottom