Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 2,582
- 4,554
Nchi hii imejaa utajiri kila mahali leo nitakujuza fursa mbalimbali zinazopatikana Handeni mkoani Tanga
1. Uuzaji wa magogo na Mbao
Hii ni moja ya biashara kubwa sana itakayokuingizia kipato kikubwa kwa muda mfupi sana ilimradi uwe full kwenye vibali vya maliasili ili usisumbuane nao
Misitu mingi ni misitu asili ambayo serikali huzuia ukataji miti ovyo kwahiyo ukija na mbadala wa miti ya mbao utapiga pesa nyingi sana kwani karibia 60% ya wakaazi wa mji huo ni mafundi selemala
2. Umiliki wa machine za kuranda na kuchana mbao
Kama unaijua keko ya Dar es salaam ilivyo basi nenda Handeni, hasa maeneo ya Mkata, kabuku na Handeni mjini
Ukiweza kumiliki mitambo ya uchanaji mbao na ukaweza kupiga kazi usiku na mchana utapiga pesa ndefu sana. Wengi wanafanyaga kazi usiku kuogopa maliasili kwahiyo lazima uwe popo ili kupata wateja wa uhakika
3. Kama una uhakika wa soko la fernitures kawekeze kwa mafundi wadogo wadogo
Watakutengenezea ferniture nzuri kwa bei rahisi sana kisha ukauza kwa bei itakayokupa faida kubwa. Ukiwa wewe ndio boss wao watakutengenezea na kukupa ukauze ukija unawakatia chao cha muhimu uaminifu tu
4. Kuuza mbuzi wa kuchinja au kuwauzia wachinjaji
Hii ni biashara kubwa sana hasa maeneo ya mkata, aisee wajomba ni wanakula mbuzi balaa na wengine na vigari vyao vya laki mbili ni wanabeba kuja nazo mjini hii itakufanya uwe tajiri bila wewe mwenyewe kujua
5. Hardware au duka la vifaa jenzi
Miji kama mkata, kabuku, segera, Handeni mjini, Kilindi n.k inakua kwa kasi sana. Watu wanafumua mijengo ya maana ukiweza kuwa na hardware ya kuaminika na ukazoeleka haraka utapiga mpunga wa maana kwa muda mchache sana
Kwa leo nitaishia hapo tukutane part two kwa wale wenye vimitaji vya kuunga unga kama mimi
Part two
Kama hujaona fursa Handeni acha nikujuze, acha kuamini mazingahombwe wekeza na ufanye biashara kwa ukubwa upate pesa utoke kwenye umasikini. Kwa wenye mitaji midogo fursa ni kama zifuatazo
6. Kuuza kuku na mbuzi wa kuchoma na kukaanga
Hii biashara ukiifanya kwa weledi na ukaacha uvivu kwa siku waweza funga na 50k faida kwa mtaji mdogo tu. Uzuri wauza mbuzi pia wanakopesha ukishauza unawapa chao ukienda nao fuleshi
7. Kuuza kuku wazima
Hawa wanatoka mashambani ukiwa mzoefu hutakuwa na ulazima wa kuwafuata huko mashambani unatega tu njiani wanakuja na wakulima. Utanunua kwa bei ndogo kabisa na kuuza kwa bei kubwa
8. Kuuza maji kwenye matoroli au ukiweza unachimba kisima
Ukiweza kuchimba kisima ndio vizuri, utaagiza maji kwenye magari halafu unauza kwa dumu au ndoo. Handeni maji ni shida sana ukiwekeza vizuri kwenye supply ya maji utatoboa haraka
9. Kama una kigari cha mkopo kifanye tax au bolt
Hii kitu bado ngeni ukiwa muanzilishi utaokota hela za bure. Maeneo kama Mkata na Handeni mjini kuna vibosile wengi sana na mishangazi huwezi kukosa 50k per day
10. Fanya umachinga wa bidhaa ndogo ndogo
Ukiachana na usajili wa laini hii fursa wengi bado hawajaiona, ukifanya kama wafanyavyo dar na majiji mengine makubwa ya kutembeza vitu mbalimbali (umachinga) utapiga hela sana watu wengi siku hizi ni wavivu kwenda dukani au sokoni
Karibu mwana Handeni mwenzangu uongezee fursa wadau wapate kusaidika