Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kazi hizi ni zile ambazo ni chafu na zingine zina vyeti na zimo katika mfumo rasmi ulowekwa na wazungu ambazo zingine zalipa kishenzi.
Nimetumia neno kazi za kishenzi kutokana na mazingira ya kazi hizi na aina ya watu wanozifanya ambao wengine ni watu waso na familia au wenye aina fulani ya matatizo ya kijamii kama kutokuoa au kuolewa.
Ila general idea ni kuona kwamba waweza kuifanya kazi ya kishenzi kuwa kazi inolipa kwa mpangilio unofaa ili kuongeza wigo wa ajira na kurasimisha ajira zisizo rasmi.
1. Mkurugenzi wa maziko au funeal director ni kazi ya kushughulikia maziko, maandalizi yake na kuwashughulikia wafiwa. Kazi hii pia hushughulikia mwili wa marehemu, kutayarisha pamoja na wanafamilia wa marehemu mazingira sahihi ya kufanya maziko. Kazi hii ina shahada ya chuo kikuu yaitwa associate degree in Mortuary Science and embalming na pia ipo leseni maalum kwa ajili ya kufanya kazi za kushughulka na maiti.
2. Uchimbaji na ukataji miamba. Hii ni kazi ya kutafuta miamba kwa ajili ya makaa ya mawe kama katika migodi ya makaa ya mawe kama mgodi wa Kiwira na mingine.
3. Portable toilet Cleaner au kazi ya kusambaza vyoo vya mobile. Sehemu za watu wengi kama mikutano ya siasa, mikutano ya dini na mikusanyiko huhitaji vyoo na watu wenyr hizi mobile toilets hupiga pesa ya maana sana. Hivyo kama mtu ana kampuni basi kampuni hiyo hupewa zabuni za kusambaza mobile toilets kwenye mazingira magumu na pia hukusanya uchafu kwa ajili ya kuutekeza kisayansi mahala salama kimazingira na si kiholela. Kinohitajika ni magari maalum yenye matangi na sehemu maalum ya kupoteza au dispose of area.
4. Fundi bomba au plumber- Huyu mtu hupiga pesa kati ya dola 200 hadi 300 kwa siku kulingana na aina au tatizo la bomba iwe chooni au jikoni au mfumo mzima wa mabomba. Fundi bomba kazi yake ni kuvunga, kufanya matengenezo mifumo ya uwangaji maji safi na maji taka pamoja na vifaa vingine vinohusiana navyo.
Mkaguzi wa mifumo ya maji taka au sewage inspector. Kazi hii yahusisha ukaguzi wa mifumo ya maji taka na mazingira yake ikiwemo kukabiliana na wadudu na wanyama kama panya. Hwa wakaguzi wa pata vyeti maalum kutoka taasisi ya kimataifa kiitwacho NACHI na ukiwa na sifa hizoi watambulika kisheria na waitwa InterNACHI Certified Sewer Scope Inspector.
Tembelea tovuti ya InterNACHI kupitia hapa Become an InterNACHI® Certified Sewer Scope Inspector
5. Landfill Operator au mzoa taka na uchambuzi taka. Kila wilaya au tarafa ni lazima iwe na sehemu ya kumwaga taka na kuchambua taka hizo. Sehemu hizi hupatina vitu vingi vya kuvifanyia recycling. Hili eneo lina nafasi kama wafanyakazi wa kawaida, wasimamizi na mameneja. Ni maeneo yenye harufu kali wakati wote ina sehemu hii hufanya kazi chini ya manispaa husika. Sifa za kufanya kazi huko ni pamoja na kuwa cheti maalum kwa kazi za ngazi za chini pamoja ana shahada ya mazingira au degree ni environmental sciences.
6. Msafishaji eneo lilofanyiwa uhalifu au Crime Scene Cleaner. Hii ni kazi ya kitaalam zaidi kwani huitaji msafishaji huyo kuwasiliana na polisi baada ya eneo lilofaniwa uhalifu kuwekewa uzio au cordoned kwa ajili ya uchunguzi. Kwahiyo baada ya matukio ya mauaji, utekaji, ajali yoyote kama ajali ya gari, na vingine huitaji usafishaji maalum na kwa kutumia vifaa maalu na kemikali. Pia kazi hii hulipa na malipo hufanywa kwa kampuni ambayo imesajiliwa rasmi kwa shughuli hizo.
Itaendelea.