Zijue mbinu za Kisasa za Kumkwepa kumlipa nauli Kondakta katika Daladala

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
  1. Epuka kupanda Daladala ambalo halijaa kwani utaumbuka kiurahisi sana bali subiria Daladala lenye nyomi / lililojaa ndiyo ulipande.
  2. Ukishaona Kondakta anaanza kuchukua nauli jifanye unaongea sana na Simu tena kwa Sauti kubwa huku ukiwa ' Seriuos ' kabisa halafu humtizami Kondakta. Mara nyingi sana Makondakta huwasau Watu ( Abiria ) wanaoongea sana na Simu katika Madaladala hadi kupelekea kusahau kuwadai nauli.
  3. Ikitokea alikupita wakati anachukua nauli akirudi Kwako na kukudai ' mkazie ' mimacho yako huku ukimuangalia ambapo Makondakta wengi hujawa na ' aibu ' kama si ' uwoga ' na kuondoka zao.
  4. Ukiona kaanza kuchukua nauli siti za mbele Wewe anza taratibu kujifanya kama vile unaonyesha unataka kushuka Kituo cha mbele na ukiona unakaribia kukutana nae katikati anzisha ' zogo ' la kuwataka abiria wenzako mliosimama wasogee kisha haraka sana ' Kiaina ' unahamia kule ambako Kondakta ameshamaliza kuchukua nauli.
  5. Pima saikolojia na Dereva na Kondakta wake ambapo ukiona wote wanapenda nyimbo za Seduce Me au Zilipendwa tiririka nazo kwa kuzisifia na kuzizungumzia sana au ukiona Dereva na Kondakta wake wanapenda sana mpira serereka na hizo hizo stori za akina Tshishimbi au Niyonzima na automatically tu utaona Kondakta au Dereva wamejenga Urafiki wa ghafla nawe na watasahau hata kukudai nauli yao.
  6. Pendelea sana kujifanya unasinzia ndani ya Daladala kwani mara nyingi sana Makondakta huwa wakiona Watu wamelala huwapita Kwanza ambapo akishamalizana na kule alikochukua nauli yake akirudi tena huku anakuwa amesahau.
  7. Kama hiyo njia mnayopita ina ' Yange Yange / Matrafiki ' wengi hakikisha kila mnapowapita basi Wewe unajifanya hata tu unawapungia mkono hao ' Matrafiki ' na kila unapomaliza kuwapungia mkono / kuwasalimia hakikisha macho yako yanamtizama Kondakta kitendo ambacho kitamfanya Yule Kondakta ahisi labda Wewe ni Askari au unaweza ' Kumlengesha ' kwa Matrafiki wengine wa mbele hivyo automatically tu utaona anakupita au hata akikupigisha stori lakini akiwa ni muoga muoga na hatothubutu kukuomba nauli.
ANGALIZO.

Hizi mbinu zitanoga endapo tu na Wewe basi mfukoni mwako una hata akiba ya Tsh 800/=. lakini kama ukizitumia halafu dili ' likabuma ' na ukashtukiwa unaweza ukaumbuka vibaya na kuishia tu Polisi na kufanya Kazi ya kufagia na kupiga deki hadi jioni.

Nawatakieni ukwepaji ulipaji nauli mwema Kesho asubuhi kwa tunaoamka na kutumia ' Daladala ' kwa ajili ya usafiri wa kutupeleka katika mihangaiko yetu na kwa wale ambao hizi mbinu Kuu Saba ( 7 ) zitwasaidieni msione aibu kuja kuniletea ' mrejesho / feedback '.

ONYO

Kuna wale ambao ni Mabingwa wa Kukopi na Kupesti kila ' Nyuzi ' nzuri ambayo GENTAMYCINE anakuja nayo humu JF na kuzifanya ni zao na kuzitumia katika ' Viblogu ' vyao kama si ' Viwebusaiti ' vyao. Tafadhalini hata Mimi huwa naumiza mno Kichwa kuja na ' taarifa ' mvuto kama hizi hivyo nawaombeni tu mkiikopi hii kitu fanyeni acknowledgement ama Kwangu Mimi GENTAMYCINE mwenyewe au huu ' Mtandao ' wangu pendwa wa JamiiForums nitawashukuruni mno.

Nawasilisha.
 
Umetoa angalizo zuri sana mkuu kwa maana kuna kubuma njia zote hizo

Na ikitokea umezitumia hizo mbinu zote Saba ( 7 ) halafu bado tena ' zikabuma ' basi jua Wewe utakuwa na bonge la ' Gundu '. Hizo mbinu ' Kondakta ' yoyote yule hata afanyeje hachomoki.
 
Huu ni uselamavi uliopitwa na wakati.

Zilipendwa.
 
Ikibuma je?

Utaenda kusaidia Kituo chochote cha Polisi kufagia ' Vibarazani ' mwao au kusafisha ' Mikojo ' ya ' Wahalifu ' utakaowakuta huko na ikifika hadi jioni ambapo kwa huruma yao wakikuachia akili itakuwa imeshakukaa sawa. Kama unajijua kabisa Wewe ni ' Kunguru / Muoga ' nakuonya mapema acha kutumia hizi mbinu ila kama Wewe ni ' Mbishi / Bandidu ' rukhsa kuzitumia kuanzia Kesho asubuhi.
 
Kuna siku nilipanda daladala la kwenda posta sasa kuna jamaa nilimkuta siti za mbelembele akipiga stori na kusema madereva na makonda wanaopata pesa nyingi lakini wanamalizia kwenye pombe na starehe hivyo maendeleo hayaonekani jamaa kapiga stori wee hizo mpaka kituo alichofikia na kushuka bila kulipa nauli ,alivyoshuka konda na dereva wake wakaanza kumshambulia watu wengine nuksi kweli kama huna nauli sema usaidiwe sio unaanza kuzuga na kuanza kusema tunaingiza pesa nyingi mara starehe stori kibao
 
Kwa huu uzi, siku yangu itamalizika vyema kabisa..
😀😀😀😀😀😀

Zaidi nimependa hiyo ya kuwa na hata akiba kama mbinu zikishindikana!
 
Mbinu ikibuma hata moja hapa ujue maumivu.

Kesho ' Matrafiki ' wajiandae kupokea ' Kesi ' nyingi za ukwepaji nauli wa Abiria au Vitengo vyote vya magonjwa ya Viungo Mahospitalini kuanzia Kesho wawe ' standby ' kwani naona dalili fulani za Watu ( Abiria ) kuvunjwa taya, bandama, ugoko na meno ya Sebuleni kufagiliwa na Makondakta.
 
Na ikitokea umezitumia hizo mbinu zote Saba ( 7 ) halafu bado tena ' zikabuma ' basi jua Wewe utakuwa na bonge la ' Gundu '. Hizo mbinu ' Kondakta ' yoyote yule hata afanyeje hachomoki.
Kweli mkuu..
 
Mkuu hili somo litawaCost watu humu[emoji23][emoji23]

Ugiligili

Wauza dawa za ' maumivu ' kuanzia Kesho naamini watauza sana kwani naona kabisa ongezeko la ' Kutukuka ' kabisa la wahitaji wa hizo dawa ambao wengi wao watakuwa ni Abiria watakaobuma katika utumiaji wa hizo mbinu zangu Saba ( 7 ) za ukwepaji ulipaji nauli katika Daladala.
 
Kesho ' Matrafiki ' wajiandae kupokea ' Kesi ' nyingi za ukwepaji nauli wa Abiria au Vitengo vyote vya magonjwa ya Viungo Mahospitalini kuanzia Kesho wawe ' standby ' kwani naona dalili fulani za Watu ( Abiria ) kuvunjwa taya, bandama, ugoko na meno ya Sebuleni kufagiliwa na Makondakta.
Umekuja dar lini?

Nitashangaa sana ukinijibu kwamba umezaliwa na kukulia hapahapa dar.
 
Back
Top Bottom