Zijue mbinu za Kisasa za Kumkwepa kumlipa nauli Kondakta katika Daladala

Zijue mbinu za Kisasa za Kumkwepa kumlipa nauli Kondakta katika Daladala

Hizo mbinu huwa zinanifikaga mara nyingi, sio kuwa sina hela ila tu huwa ni mtu wa kuchezea simu muda mrefu napokuwa kwenye gari. So hio ya konda kupita na hatimae kusahaulika inatokeaga sana saingine nawapa nikiwa nashuka ila muda mwengine nawapotezeaga tu kulingana na mood yangu!
 
Fundisha kukwepa kodi nauli ya 400 nikwepe ya nini

Enzi nasoma mwanafunzi nauli 50 nime panda sana dala dala bure

Hadi makonda wa posta wakanikariri wakiniona wanaomba nauli mlangoni
 
hahahaa...
hizo enzi za uanafunzi konda akikuomba nauli unasema umekaa vibaya, alafu baadae unahama siti watu wakipungua kama sio muangalifu hapo kaishaliwa, au unahamia siti ya mbele kutoka kwenye bansenburner mtu akishuka (hiace). Hapo ndio kaisha sahau.
ila sio vizuri huo ujanjaujanja kwa kweli.
 
Umewashtua masela!
Makonda watakaba mpaka penalt.
Usishangae ukadaiwa nauli wakati wa kutinga kwenye daladala.
 
Akya kya kya kya kya kya kya kya kya hizi mbinu zinafaa kwa wale wa mbagala na Gongo la mboto mida ya jioni na asubuhi
 
  1. Epuka kupanda Daladala ambalo halijaa kwani utaumbuka kiurahisi sana bali subiria Daladala lenye nyomi / lililojaa ndiyo ulipande.
  2. Ukishaona Kondakta anaanza kuchukua nauli jifanye unaongea sana na Simu tena kwa Sauti kubwa huku ukiwa ' Seriuos ' kabisa halafu humtizami Kondakta. Mara nyingi sana Makondakta huwasau Watu ( Abiria ) wanaoongea sana na Simu katika Madaladala hadi kupelekea kusahau kuwadai nauli.
  3. Ikitokea alikupita wakati anachukua nauli akirudi Kwako na kukudai ' mkazie ' mimacho yako huku ukimuangalia ambapo Makondakta wengi hujawa na ' aibu ' kama si ' uwoga ' na kuondoka zao.
  4. Ukiona kaanza kuchukua nauli siti za mbele Wewe anza taratibu kujifanya kama vile unaonyesha unataka kushuka Kituo cha mbele na ukiona unakaribia kukutana nae katikati anzisha ' zogo ' la kuwataka abiria wenzako mliosimama wasogee kisha haraka sana ' Kiaina ' unahamia kule ambako Kondakta ameshamaliza kuchukua nauli.
  5. Pima saikolojia na Dereva na Kondakta wake ambapo ukiona wote wanapenda nyimbo za Seduce Me au Zilipendwa tiririka nazo kwa kuzisifia na kuzizungumzia sana au ukiona Dereva na Kondakta wake wanapenda sana mpira serereka na hizo hizo stori za akina Tshishimbi au Niyonzima na automatically tu utaona Kondakta au Dereva wamejenga Urafiki wa ghafla nawe na watasahau hata kukudai nauli yao.
  6. Pendelea sana kujifanya unasinzia ndani ya Daladala kwani mara nyingi sana Makondakta huwa wakiona Watu wamelala huwapita Kwanza ambapo akishamalizana na kule alikochukua nauli yake akirudi tena huku anakuwa amesahau.
  7. Kama hiyo njia mnayopita ina ' Yange Yange / Matrafiki ' wengi hakikisha kila mnapowapita basi Wewe unajifanya hata tu unawapungia mkono hao ' Matrafiki ' na kila unapomaliza kuwapungia mkono / kuwasalimia hakikisha macho yako yanamtizama Kondakta kitendo ambacho kitamfanya Yule Kondakta ahisi labda Wewe ni Askari au unaweza ' Kumlengesha ' kwa Matrafiki wengine wa mbele hivyo automatically tu utaona anakupita au hata akikupigisha stori lakini akiwa ni muoga muoga na hatothubutu kukuomba nauli.
ANGALIZO.

Hizi mbinu zitanoga endapo tu na Wewe basi mfukoni mwako una hata akiba ya Tsh 800/=. lakini kama ukizitumia halafu dili ' likabuma ' na ukashtukiwa unaweza ukaumbuka vibaya na kuishia tu Polisi na kufanya Kazi ya kufagia na kupiga deki hadi jioni.

Nawatakieni ukwepaji ulipaji nauli mwema Kesho asubuhi kwa tunaoamka na kutumia ' Daladala ' kwa ajili ya usafiri wa kutupeleka katika mihangaiko yetu na kwa wale ambao hizi mbinu Kuu Saba ( 7 ) zitwasaidieni msione aibu kuja kuniletea ' mrejesho / feedback '.

ONYO

Kuna wale ambao ni Mabingwa wa Kukopi na Kupesti kila ' Nyuzi ' nzuri ambayo GENTAMYCINE anakuja nayo humu JF na kuzifanya ni zao na kuzitumia katika ' Viblogu ' vyao kama si ' Viwebusaiti ' vyao. Tafadhalini hata Mimi huwa naumiza mno Kichwa kuja na ' taarifa ' mvuto kama hizi hivyo nawaombeni tu mkiikopi hii kitu fanyeni acknowledgement ama Kwangu Mimi GENTAMYCINE mwenyewe au huu ' Mtandao ' wangu pendwa wa JamiiForums nitawashukuruni mno.

Nawasilisha.


Na kwa nini ukwepe kulipa Nauli? Kwa nini unataka kula jasho la Binadamu mwingine anayejituma kujikwamua kila siku kama wewe unavyojituma kwenye kazi yako? Unaelewa hata maana ya neno ,,HAKI"? Kama hauna hela ya nauli kwa nini usiongee naye kwanza na kumuomba? Acha hizo konda anahitaji hela kama wewe na mimi hata yeye ana familia ya kuhudumia pia hivyo tuache mambo ya kurudishana nyuma, lipa nauli kwa faida ya wote!

Kila la Heri!
 
Nimeshawahi kufanya muda wa usiku.
Kuna abiria huwa wanakwepa nauli. Utakuta umechukua nauli kwa kuanzia mbele, ile unamaliza nyuma, gari linafika kituoni halafu kuna abiria labda watatu wanashuka na watano wanaingia.
Sasa kati ya wale walioingia, unakuta wote wamepata siti, sasa si inabidi urudi kwa kuchezesha sarafu! unakuta mwingine anajikausha kabisa halafu unajua kabisa huyu abiria amepanda sasa hivi na ana mwonekano wa kipekee ambao haukuwepo kabla kwenye gari wakati nachukua nauli. Huyo unamkomalia hadi anaona aibu na hafiki mwisho wa safari.
Hiyo tabia wanayo sana masharobaro, halafu abiria akisema amlipie eti wanajifanya kukataa.
 
ongezea na hii

atalipa mbele(kama wewe upo nyuma) ,au atalipa nyuma (kama wewe upo mbele.

njia hii nzuri kama mpo wawili mnafahamiana (wambele na wanyuma)

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

*Akifa shekhe kazi ya Mungu*
*Akifa mlevi sababu ya Pombe*
 
Back
Top Bottom