Nimeshawahi kufanya muda wa usiku.
Kuna abiria huwa wanakwepa nauli. Utakuta umechukua nauli kwa kuanzia mbele, ile unamaliza nyuma, gari linafika kituoni halafu kuna abiria labda watatu wanashuka na watano wanaingia.
Sasa kati ya wale walioingia, unakuta wote wamepata siti, sasa si inabidi urudi kwa kuchezesha sarafu! unakuta mwingine anajikausha kabisa halafu unajua kabisa huyu abiria amepanda sasa hivi na ana mwonekano wa kipekee ambao haukuwepo kabla kwenye gari wakati nachukua nauli. Huyo unamkomalia hadi anaona aibu na hafiki mwisho wa safari.
Hiyo tabia wanayo sana masharobaro, halafu abiria akisema amlipie eti wanajifanya kukataa.