Zijue rekodi walizoweka wasanii wa Tanzania

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Kama wengi tunavyojua competition imekuwa kali mno kwenye muziki wa Tz kitu kinachofanya kazi za wasanii wetu kufanya kazi kwa ubora zaidi, siku zote kufeli ndio mama wa kufaulu, wasanii wengi kuna kipindi walifeli walijifunza walipokosea na kurudi wakiwa katika hali nzuri na kuongeza ushindani ndani ya muziki, zifuatazo ni rekodi za wanamuziki mbali mbali katika tasnia ya kimuziki hapa bongo.

MSANII ALIECHUKUA TUZO NYINGI ZA NYUMBANI KWA MPIGO

Mwaka 2014 Diamond alizoa tuzo 7 kwa mpigo kilimanjaro awards na hadi sasa ndiye anaeshikilia usukani kwenye wasanii waliochukua tuzo nyingi hapa Tanzania

MSANII ALIEFANIKIWA NA BAADAE KUFULIA
Mr. Nice wa Takeu style kuku kapanda baiskel bata kavaa raizoni, huyu msanii alifanikiwaga sana tu ila cha kushangaza kwa sasa ni mtu asiye na mbele wala nyuma katika maisha yake.

MSANII ALIERUDI KASI BAADA YA KUKAA KIMYA
Ni King Kiba kama anavyojiita baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu ally kiba alirudi kwa kasi mpya kwa kutoa hitsongs kama mwana na chekecha.

MSANII ANAETOA VIDEO BORA
Diamond again, Kiukweli huyu kijana video anazofanya ni za kiwango cha juu mno na huwa zinahitaji pesa nyingi sana ili zikamilike

MSANII WA TZ MWENYE TUZO NYINGI ZA KIMATAIFA
Ni Diamond tena kuna kuna kipindi ashawai kukwapua tuzo 3 za kimataifa kwa mpigo, ni juzi tu kachukua tuzo ya MTV mama na nyingine ya africa archievers awards nyingine bado zinasubiri.

MSANII MWENYE NGUVU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Huyu kijana wetu D a.ka Diamond huko mitandoni ni gumzo kwa sasa kwenye mtandao tu wa instagram ana followers zaidi ya 860,000 soon mungu akipenda anaingia na follower milioni.

WASANII WALIOCHUJA HARAKA

Hapa kwa kusema kweli Belle 9 na Hussein Machozi ndo panawafaa, Belle 9 na Hussein Machozi kwa sasa wamechuja kwa haraka mno, hawa wasanii washawai kutoa hitsongs kali sana ila kwa sasa mambo yameenda mrama

MSANII ALIEFANYA KOLABO YA KIDUNIA
Hapa ni Ally kiba, kuna kipindi aliitwa na R.Kelly kwenda kujiunga na kundi la one8 na kutoa single ya hands across the world, kiukweli ilikuwa ni hit song ilitamba dunia nzima yaani international level.

WASANII WASIOCHUJA

Waliwakuta wasanii wengi wakaaachwa wanahit, walikutwa na wasanii wengi waliachwa bado wanahit, hapa nawazungumzia lady jayd, Ay , Mwana fa na professor J , heshima mbele kwao hawa wasanii kiukweli they have to be inspired.

MSANII ANAYETENGENEZA PESA NYINGI

Hapa ni Diamond tena kwanza kabisa show zake ni kawaida kukuta viingilio vya laki mbili na ukikuta kiingilio cha chini kabisa yaani wale wenye ticket za kawaida basi ni elf 50 na ikitokea bahati basi mtazamia kwa elfu 30, huu ni uthibitisho tosha kabisa mapromoter wanaoandaa hizi show wanampa mpunga mrefu mno ambao umemsaidia kujenga nyumba kali na kuride ndinga hatari.
 
Labda tungeanza na definition kwanza ya neno REKODI
 
Maana kwenye thread hii vingi navyoviona siwez kuviita rekodi kwa nnavyoelewa mimi
 
MSANII ANAETOA VIDEO BORA - Diamond again, Kiukweli huyu kijana video anazofanya ni za kiwango cha juu mno na huwa zinahitaji pesa nyingi sana ili zikamilike, ndie msanii alieleta mapinduzi kwa wasanii wa tz kwenda kwa GodFather kushoot video wakiwemo kina OmmyDimpoz, chegge&Temba, AliKiba , n.k

rayc (uko wapi) imefanyika china video yake
Ali kiba (macmuga) souz halafu angalia contents katika hizo video daimond sio msanii wa kwanza kufanya video za gharama au nje ya nchi labda kwa hao wengine ila sio kingkiba au ray c
 

Ray c alivofanya shooting china je alileta hamasa ya wasanii kwenda China kufanya video kile kipindi,?, kiba Mac muga ilivyofanywa south Africa ilikuwa na kiwango cha kawaida mno, ilichukuliwa kawaida na wasanii wakaendelea kama kawa na Adam juma ila wasanii walivoona video za D no nzuri wengi ndo wakaanza kwenda sauzi kwa kampuni linaloandaa video za D wakiwemo chegge, temba, ali kiba,ommy, etc
 
REKODI HII IMESAHAULIKA JAMANI. msanii anategemea UCHAWI NA KUROGA hili awike nae ni DIMOND
 
kiwango cha kawaida kivipi? kwa wakati ule hizo zilikuwa video nzuri sana sio sasa hivi utandawazi umekuwa sawa Shyny c mi nilikuwa nazungumzia kufanya video nje ya nchi wakati ule sio sasa hivi instagram whats up fb mawasiliano yamerahisishwa
 
Last edited by a moderator:
REKODI YA MSANII KALUMANZIRA TUNGULI NI dimond,makofi kwake tafazari
 
kiwango cha kawaida kivipi kwa wakati ule hizo zilikuwa video nzuri sana sio sasa hivi utawazi umekuwa sawa Shyny c mi nilikuwa nazungumzia kufanya video nje ya nchi wakati ule sio sasa hivi instagram whats up fb mawasiliano yamerahisishwa

ya ray c sawa ilikuwa kali ila ya macmuga hata bongo ingewezwa kutengenezwa, mkuu rayc alipoenda China msanii gani mwengine aliepata shauku ya kumwiga ray c nae akaenda China kutoa video kwa kipindi kile, Mac muga ilivyotoka ni msanii gani mwengine alieapata shauku ya kumwiga ama kusaidiwa na kiba aende southafrica kutoa video kwa kipindi kile, ?
 
Last edited by a moderator:
REKODI YA MSANII KALUMANZIRA TUNGULI NI dimond,makofi kwake tafazari

kuna watu walizaliwa kutokana na hitilafu zinazofanya kon*om zipasuke, usiwape sababu walimwengu wakudhanie wewe ni mojawao
 
soko limebadilika sasa hivi unajua sio kama zama mkuu kwani ubora wa video ni nini??
 
soko limebadilika sasa hivi unajua sio kama zama mkuu kwani ubora wa video ni nini??

kitu chochote chenye ubora hupendwa na wengi ndomana hizi video za Godfather za kina diamond, kiba, shetta zinapigwa vituo Vingi Africa mana in high quality, ubora wa video pia tunaangalia recent teknolojia inayotumika internationally
 
kitu chochote chenye ubora hupendwa na wengi ndomana hizi video za Godfather za kina diamond, kiba, shetta zinapigwa vituo Vingi Africa mana in high quality, ubora wa video pia tunaangalia recent teknolojia inayotumika internationally
duu naona unataka tubishane ila kupendwa kwa video sio kwamba ndio bora hapana video inategemea na content mfano (nasema nawe) sasa yale mauno yote isipendwe au video za ney za mazombi (mr ney na sina mda) so kupendwa kwa video au kuwa na viewers inategemea na content ya video sio ubora
 
kuna watu walizaliwa kutokana na hitilafu zinazofanya kon*om zipasuke, usiwape sababu walimwengu wakudhanie wewe ni mojawao

baada ya mimba kutungwa kwa bahati mbaya inaonekana jamaa alipitia sehem ya haja kubwa wakati wa kuzaliwa kwake
 
Lady jayde na Ay wameanza kutoa video kule south Africa kabla ya diamond. kumbuka wimbo wa wangu JD na Mr blue ngoma ilitengenezwa na godfather
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…