Uchaguzi 2020 Zijue sababu kuchelewa vikao Kamati Kuu ya CCM kupitisha Wagombea wa Ubunge

CCM na rushwa ni mama na Baba
 
Hakuna kitu kama hicho, na wewe acha kupotosha..kama una mfano wa jimbo au kata ambapo wagombea wote walihonga wajumbe taja hapa ni jimbo gani au kata gani, tusiongee nadharia jamani mambo yote yanafahamika, katika kila jimbo na kata wapo wengi tu ambao hawakutoa hongo kabisa hata senti kwa mjumbe yeyote, wapo wengi tu! acheni kugeneralize
 

CCm kama wasemavyo ina wenyewe na wenyewe wanakuambia mkono mtupu haulambwi!! Ili uchaguliwe huko ccm ni lazima kuhonga hata JIWE analijua hilo na alihonga sana alipokuwa mbunge!! Hivi sasa anawahadaa watu tu!!! Ulizia wenyeji wa Chatto wakupe historia ya ubunge wake.
 
Tatizo lenu ni kutaka mabishano ambayo hayasaidii kitu chochote, tunaongea hapa kura za maoni mwaka huu wewe umerukia kitu kingine kabisa..point ni kwamba si wote walioshiriki kura za maoni CCM walihonga wajumbe!
 
Ujenzi wa mnara wa Babel.
 
Tatizo lenu ni kutaka mabishano ambayo hayasaidii kitu chochote, tunaongea hapa kura za maoni mwaka huu wewe umerukia kitu kingine kabisa..point ni kwamba si wote walioshiriki kura za maoni CCM walihonga wajumbe!

Wewe huijui ccm!! ccm ina wemyewe sasa nyie wakuja mnajifanya mnakijua hicho chama zaidi kuliko wao ndio wanawaonesha sasa!! Tutaona mwisho wake.
 
Kosa la rushwa ni kwa anayetoa tu? Vipi kwa anayepokea?? 😀
Ukimkata mgombea kwa tuhuma za rushwa ukawaacha wajumbe waliopokea utakua umepunguza matawi tu na mti utakua tena baada ya mvua kunyesha. Kama ni kukomesha rushwa kata mti wote mzima(matawi+mizizi) kitu ambacho hakiwezi kutokea tena mpaka uchaguzi ujao kwasababu rushwa inakamatwa on the spot (mtoaji na mpokeaji papo kwa hapo)
Kwaiyo kigezo cha rushwa hakina mantiki yoyote🚮
Sauti inatosha? Au niongeze
 
Kwa mf. Jimbo la kawe hivi mnaamini kwamba kweli watanzania kwa sasa tunawaamini sana vijana au kigezo gani kimetuka pale?😂😂
 
Hata walioshindwa walitoa rushwa ila washindi walitoa zaidi. Labda Mashinji aliyepata kura 2!
Wakati wa kupiga kura mjumbe anabalance pesa uliyompa na mapenzi yake kwako so hata aliyeshindwa anaweza kuwa ndiye alyetoa mzigo mrefu zaidi
Mchawi mjumbe😂, tatizo liko hapa sijui kwanini tunajifanya hatuoni
 
Wawakate tu waliotoa rushwa wote na wafanye uamuzi based na advantage ya mtu utendaji wake. Ila CCM kwa rushwa kiboko hadi viti maalumu rushwa, hichi chama kwa kweli kijifikirie mtu anayetoa rushwa hafai maana ni adui wa haki.
Naapa watafunika kikombe mwanaharamu apite, maana tofauti na vyama vingine CCM karibu wote walioongoza kwa kura na wale waliowafuatia
wote wametoa rushwa! Chama kinanuka!
 
TAKUKURU wamerudisha mpira CCM!
Hapo nimeshindwa kuelewa, kwamba ni CCM ndo wameomba hiyo pass (warudishiwe) au ni TAKUKURU wenyewe wameamua kuitoa. Jambo lingine sijui sheria na taratibu zao za ufanyaji kazi zinavyowaongoza na hiyo namna walivyorudisha mpira kwa wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…