Ratiba za kichama hapa Makao Makuu Dodoma zinaonesha kuwa vikao vya Kamati Kuu wa CCM almaarufu kama CC vilipaswa kufanyika tarehe 7 na 8 ya mwezi huu. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichoketi hapa Dodoma au hata Dar es Salaam. Ajenda kuu ya kikao hicho ni kupitisha majina ya Wagombea wa Ubunge wa Majimbo wa CCM Tanzania Bara na Visiwani.
Zipo sababu mbili zilizochelewesha vikao vya Kamati Kuu. Kwanza, kuna tuhuma lukuki za rushwa kwenye mchakato wa kura za maoni majimboni. Taarifa zimemiminwa CCM kutoka TAKUKURU, waliogombea, makada hadi wananchi wa kawaida kuhusu vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni chamani. Kamati ya Maadili ya chama imeelemewa na makabrasha ya tuhuma kutoka karibu kila mkoa wa Tanzania.
Katika hilo la rushwa, kuna wakubwa chamani wanataka itumike FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE katika kupata suluhu la jambo hilo. Yaani, rushwa isionekane kwenye macho ya wanaKamati Kuu na hivyo wagombea waangaliwe kwa vigezo vinginevyo kama kukubalika na si rushwa. Inapendeezwa kuonwa kuwa wagombea walizidiana dau wenyewe kwenye majimbo yao. Kuna mvutano mkubwa kwenye Kamati ya Maadili na hata baina ya viongozi waandamizi wa chama.
Sababu ya pili ni sauti za makada na wananchi kuhusu nani arudishwe wapi kugombea. Kuna waliokataliwa majimboni lakini wanatakiwa uongozini; kuna waliopita majimboni lakini hawatakiwi chamani na uongozini; kuna waliokataliwa lakini wanatakiwa huko huko majimboni. Kamati Kuu imetumia muda wa kutosha kutega masikio yake huko site ili kujiridhisha kabla ya kufanya uamuzi wake. Je, waliokatwa wataandikwa tena?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa jijini Dodoma)
Mzee Tupatupa hili suala la mlungula ni pana sana, ndio maana wenzetu ambao wamekuwa kwenye siasa miaka 1000 kabla yetu wanalitafsiri kwa majina tofauti tofauti. Wengine Corruption, sleesy nk. sasa ifuatayo ndio maana yake:
Ikiwa pesa imetolewa kwa ajili ya ushindi wa Mwanachama halisi na mzalendio dhidi ya mwanachama ambaye anaweza kuwa msaliti KUNA JINA LAKE.
Pesa inayotolewa kukipigania maslahi mapana ya chama chako dhidi ya chama pinzani INA JINA LAKE.
Pesa inayotolewa kwa kuhakikisha mgombea mnao mtaka ashinde lakini kwa ajili jya amii yote kwa wingi wao imekubaliana INA JINA LAKE.
Pesa yeyote itakayo tolewa na wana CCM kwa ajili ya kujiahami na upotoshaji wa vyama pinzani UNA JINA LAKE.
Mwambie Mwenyekiti wako aweze kufahamu kuwa unapo kupigania na kuhakikisa Tapeli wapinzani hawashindi hiyo inatakiwa kuwa na jina jingine ila kwa kuwa kishwahili kina upungufu katika kuelezea masuala ambayo siyo asili yetu , tuna pandikiza maneno ambayo sio kila mara sahihi.
NK; Ni sawa na mama yako mzazi anaelekea kubakwa na mtu ambaye lazima umzuie kwa njia yeyote ile bila kuwa na mbadala kwa kuwa mama hana uwezo kwa kujihami kwa njia yeyote ile, ukiende Polisi : shitaka wanachoangalia ni nguvu gani ilitumika kufuatana na tukio. Kama ni nguvu inayo enda sambamba na kuizidi nguvu ya Mshambuliaji ili umuokoe mama , hata kama ikitokea madhara makubwa zaidi hiyo huitwa , Shambulio la kujilinda. Kama nchi ukijitolea kuhakikisha nchi inabaki salama hata kama wewe utajitoa muhanga basi HUITWA SHUJAA WA TAIFA.
Wako wanachama ambao mnajua CCM ikishindwa anaweza kujiua; hii huitwa amelipa Ultimate price, hukumu yake lazima ipimwe kwa mintarafu kuwa ni lazima apate matokea kwa itakavyo kuwa.