Zijue sababu za jeshi letu JWTZ kutokutoa kichapo kingine kwa M23, kama tulivyotoa mwaka 2013 hadi 2014

Kwani kipindi cha Kikwete huyo mdau halikiwa hatumii bandari yetu? Bandari kavu ya kahama ilianza lini kwa kusudi gani? Hoja hii dhaifu labda ile nyingine kuwa unaangalia kuoata pesa kwa mwamvuli wa UN
Kipindi cha Kikwete mfadhili alikuwa anatumia bandari yetu kabla hawajakorofishana na Kikwete. Baada ya kukorofishana akaanza kupunguza matumizi ya bandari yetu, na baadae kujipanga kutafuta njia nyingine ya kutumia kupitisha mizigo yake. Hivyo akawa anapanga na wenzake kutumia bandari ya Mombasa Kenya.

Magufuli alipoingia madarakani safari yake ya kwanza nje kama raisi ikawa kwa huyo mfadhili ili kuweka mambo sawa na kumtaka mfadhili aachane na mawazo ya kutumia bandari ya Mombasa badala yake aendelee na hiyo hiyo ya kwetu kwa makubaliano ya kutoingilia masilahi ya mfadhili huyo huko Congo.

Hata raisi Samia alipoingia alikwenda huko mapema kuweka mambo sawa sawa. Angalia picha hiyo ya plan ya mfadhili aliyopanga kutumia bandari ya Mombasa kipindi cha mzozo wake na JK.
 

Attachments

  • Screenshot_20250127-183802.jpg
    345.2 KB · Views: 2
Nakumbuka 2013 nilikuwa kambi moja huko Kanda ya Ziwa... Tulikuwa tushapewa maelekezo kuwa wakati wowote tunaliamsha na Majirani.


Kwa hakika hekima ilitumika tu. Mambo yalikuwa yako hot sana.
Shukran kwa kuliweka wazi hili mkuu. Humu kuna vijana wanabisha, bila kujua wanachokibisha.
 
Umeandika hadithi nzuri sana mkuu ila fanya utafiti kwanza hasa wa kiuchumi. Kwa maana ya faida ya DRC kwa Tanzania na Faida Ya Rwanda kwa Tanzania..

Mbingu Na Ardhi!!

Naamini ukimaliza kufanya utafuti utafuta hii post!!
 
Hahahah!! Mpk mseme kumeanza kuchangamka.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Umeandika hadithi nzuri sana mkuu ila fanya utafiti kwanza hasa wa kiuchumi. Kwa maana ya faida ya DRC kwa Tanzania na Faida Ya Rwanda kwa Tanzania..

Mbingu Na Ardhi!!

Naamini ukimaliza kufanya utafuti utafuta hii post!!
Kwanini niifute mkuu?

Sisi kama taifa tunazihitaji nchi zote mbili. Na kwa mantiki hiyo hatuwezi kuchagua kuisaidia nchi moja dhidi ya nchi nyingine, kwa sababu hata hicho kidogo tunachopata kutoka kwenye hiyo nchi nyingine kuna majirani zetu wengine wanakikosa.

Kwa vile vita hiyo sio ya kwetu basi haina haja ya kuonesha wazi wazi kwamba tunapambana na nchi ambayo haijatuchokoza. Acha waliochokozana wayamalize wenyewe.

Ikishindikana kuna ushauri nimetoa kwenye post namba 65. Ufuatwe na Congo mara 1 halaf hao waasi waone moto wake.
 
Kuna sheria au Chapter mbili tofauti.
Moja inawataka kulinda aman bila kutumia nguvu na nyingine wanatumia nguvu , Kuna Chapter #6 na Chapter# 7 km sijakuelewa
Hii ya kutumia nguvu mpaka uruhusiwe.

Halafu kingine unapigana na mtu ambaye silaha yake muda wote inafanya kazi na wewe silaha Yako ndyo kwanza unakuta hyo siku umestukizwa ndyo unaanza nayo. lazima ikusumbue na ukizingatia kwenye shambulizi la ghafra majibizano lazima yawe ya papo kwa hapo kitendo Cha kusubiri ndyo unakwisha hivyo
 
Uko sahihii..
 
Chapter 7 , au Chapter VII ndio inaruhusu matumizi ya Nguvu
 
Chapter 7 , au Chapter VII ndio inaruhusu matumizi ya Nguvu
Unaweza kuifafanua hiyo chapter inayoruhusu matumizi ya nguvu.

I mean unaitumia hiyo chapter katika mazingira gani ili isionekane kua umevunja sheria za jeshi?
 
Unaweza kuifafanua hiyo chapter inayoruhusu matumizi ya nguvu.

I mean unaitumia hiyo chapter katika mazingira gani ili isionekane kua umevunja sheria za jeshi?
Kuna Chapter mbili , chapter 6 na chapter 7, ni mpk baraza la Usalama likae na kuona Kuna haja ya kutumia chapter ipi ktk kupata suluhu ya mgogoro husika

Chapter 7 Kama unakumbuka ndio iliyotumika kuwafurusha M23 kipindi kile na hiii tuliombwa na UN

Chapter 6 ni ulinzi wa kulinda aman bila kutumia nguvu

Chapter 7 ni ulinzi wa kulinda aman Kwa kutumia nguvu na kupora silaha Kwa waasi..nimekupa Kwa ufupi unaeza Ku google zaidi

Kumbuka ni lzm upewe kibali
 
Tuna jeshi zuri uongozi mbovu tangu 64 years. Ikibidi captain ashike mpini tu.
 
Jeshi letu saiv halina kiongozi shupavu ilitakiwa waziri wa mambo ya ndani na ulinzi awe mwanajeshi
Hiv jeshi masuala yake yanashughulikiwa na wizara ya mambo ya ndani?? Sio jeshi la polis ,magereza, fire etc??
 
Shukran mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri.
 
Hiv jeshi masuala yake yanashughulikiwa na wizara ya mambo ya ndani?? Sio jeshi la polis ,magereza, fire etc??
Nafikiri alimaanisha wizara zote mbili yani ya mambo ya ndani, na ya ulinzi ziongozwe na mawaziri wanaojua mambo ya jeshi.

Hakumaanisha waziri wa mambo ya ndani aongoze wizara ya ulinzi. Numbisa
 
Mpaka kufatilia mkuu,siku hizi wizara zinabadilishwa badilishwa sana
Hapana hizo ni wizara mbili tofauti.

1. Wizara ya ulinzi ipo chini ya mhe. Dr Stargomena Tax.
2. Wizara ya mambo ya ndani kwa sasa ipo chini ya mhe. Bashungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…