Zijue sababu za jeshi letu JWTZ kutokutoa kichapo kingine kwa M23, kama tulivyotoa mwaka 2013 hadi 2014

Zijue sababu za jeshi letu JWTZ kutokutoa kichapo kingine kwa M23, kama tulivyotoa mwaka 2013 hadi 2014

Kwani kipindi cha Kikwete huyo mdau halikiwa hatumii bandari yetu? Bandari kavu ya kahama ilianza lini kwa kusudi gani? Hoja hii dhaifu labda ile nyingine kuwa unaangalia kuoata pesa kwa mwamvuli wa UN
Kipindi cha Kikwete mfadhili alikuwa anatumia bandari yetu kabla hawajakorofishana na Kikwete. Baada ya kukorofishana akaanza kupunguza matumizi ya bandari yetu, na baadae kujipanga kutafuta njia nyingine ya kutumia kupitisha mizigo yake. Hivyo akawa anapanga na wenzake kutumia bandari ya Mombasa Kenya.

Magufuli alipoingia madarakani safari yake ya kwanza nje kama raisi ikawa kwa huyo mfadhili ili kuweka mambo sawa na kumtaka mfadhili aachane na mawazo ya kutumia bandari ya Mombasa badala yake aendelee na hiyo hiyo ya kwetu kwa makubaliano ya kutoingilia masilahi ya mfadhili huyo huko Congo.

Hata raisi Samia alipoingia alikwenda huko mapema kuweka mambo sawa sawa. Angalia picha hiyo ya plan ya mfadhili aliyopanga kutumia bandari ya Mombasa kipindi cha mzozo wake na JK.
 

Attachments

  • Screenshot_20250127-183802.jpg
    Screenshot_20250127-183802.jpg
    345.2 KB · Views: 2
Nakumbuka 2013 nilikuwa kambi moja huko Kanda ya Ziwa... Tulikuwa tushapewa maelekezo kuwa wakati wowote tunaliamsha na Majirani.


Kwa hakika hekima ilitumika tu. Mambo yalikuwa yako hot sana.
Shukran kwa kuliweka wazi hili mkuu. Humu kuna vijana wanabisha, bila kujua wanachokibisha.
 
Niaje waungwana

Kwanza kabla ya kuelezea sababu za jeshi letu kutokutoa kichapo kwa M23, naomba kwanza nianze kuwapa historia tukufu ya jeshi letu la JWTZ au TPDF kwa nchi mbali mbali za Africa na Dunia kwa ujumla.

JTWZ chini ya baba wa taifa letu hayati mwl. Julius K. Nyerere ndio iliyoongoza mapambano yasioshindwa ambayo kwa asilimia kubwa yalisaidia nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na Angola kuwa katika mikono salama, na amani ya kudumu mpaka leo.

Idi Amin alitaka kujichanganya eti aichukue Bukoba, matokeo yake imechukuliwa nchi yake mwenyewe, halaf yeye akatoka nduki.

JWTZ hiyo hiyo chini ya utawala wa hayati mzee Ally Hassan Mwinyi ndio iliyotoa kichapo kitakatifu kwa jeshi la Burundi ambalo lilitaka kuteka sehemu ya mkoa wa Kigoma, kwa kisingizio cha kuja kuwapiga waasi wa CNDD-FDD ambao walikuwa wakipambana na serikali ya Burundi chini ya uongozi wa raisi meja Pierre Buyoya (rip).

Ni kwamba Buyoya na serikali yake walikuwa wanadai kwamba serikali ya Tz imekuwa ikitoa msaada wa kuwahifadhi waasi hao katika maeneo ya mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Burundi. Hivyo dawa ya kukomesha jambo hilo ilikuwa ni kuivamia Tz (Buyoya sijui nani alimhadaa ashike moto kwa mkono), kuichapa na kuteka maeneo yote aliyodai yanatumiwa na waasi nchini kwetu kufanyia training na kupanga mipango ya kuingia Burundi kufanya maangamizi mara kwa mara.

Basi bwana Buyoya akaamuru jeshi lake lifanye ambush kupitia mipaka ya ardhini na majini. Aisee kilichotokea kwa upande wa Burundi mpaka leo ni hasara kwa nchi yao.

Kuna jamaa fulan Mrundi anasema kuwa sehemu hiyo iliyoangukiwa na kombora kutoka Tz mpaka sasa hapajawahi kuota chochote, na wala kujengwa chochote. Ni kama vile ardhi imeunguzwa hata kwa kutengenezea tofali za kuchoma haufai kudadeki. Baada ya lile tukio Buyoya na warundi wenzie wakawa wapole na askari waliokuwa wanalinda mipaka ya majini na ardhini kwa upande wa Burundi akawasogeza mbali mno kutoka mpakani.

Chini ya utawala wa raisi Kikwete kuna raisi alikuwa ashapinduliwa hapo Comoro, ikabidi aje kuomba msaada wa kumrudisha madarakani. Ni kitendo cha masaa tu raisi akarudishwa na wahuni waliopanga mapinduzi wakatiwa nguvuni.

Pia chini ya Kikwete raisi wa Burundi hayati Pierre Ngurunziza alikuwa ameshapinduliwa na kuambiwa abaki huku huku Tz alipokuwa amekuja kwa mkutano wa amani. Baada ya ujinga huo, Kikwete akatuma kikosi kidogo tu cha wanajeshi wa kumrudisha nchini kwake salama na kuwatia nguvuni wapuuzi wachache waliompindua raisi wao. Bila kuchelewa jeshi letu likamrudisha Ngurunziza, ila wapinduaji wakafanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani.

Chini ya utawala huo huo wa Kikwete jeshi letu lilitoa kipondo ambacho kilisababisha waasi wa M23 kutimkia Uganda na Rwanda. Na hii ni baada ya raisi wa Rwanda mhe. Paul Kagame kumletea dharau Kikwete na jeshi letu hali iliyosababisha Kikwete adili na kila kinachompaka Kagame jeuri. Alianza na wanyarwanda waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria, baadae akarukia Congo kuwafyeka M23 ambao waliaminika kuwa ni jeshi dogo la Rwanda. Kisha akasogeza jeshi mkoa wa Kagera kuwa tayari kuingia Kigali, sema hekima Za mzee Mwinyi na Mkapa zilichangia kumfanya Kikwete asivaamie Rwanda kumtoa adui yake.

Tukiachana na hayo. Tushapandikiziwa vikundi vya waasi kwa mgongo wa dini huko Tanga, Kibiti nk. Lakini jeshi letu halijawahi kucheka na kima wote tumewaangamizi kwa muda mfupi sana.

Hizo operations zote nilizoeleza hapo juu zilitekelezwa na TPDF bila kushindwa wala kurudi nyuma. Hivyo uwezo wa kumpiga adui toka miaka hiyo tulikuwa, tunao na tutaendelea kuwa nao. Huu ndio ukweli halisi.

Sasa tukija kwa hii vita ya sasa ya M23. Kuna watu wanajiuliza iweje M23 hii tulioichapa wakati wa Kikwete imetushinda wakati wa Samia!!

Ukweli ni kwamba jeshi letu lipo imara, vizuri na tayari kwa mapambano wakati wowote bila kujali ni nani aliepo madarakani. Kikubwa ambacho hufanyika ni kuliongezea silaha za kisasa, mbinu mpya za kijeshi, nguvu na morali zaidi za kulitumikia jeshi la wananchi. Pia jeshi letu hupambana kupitia kauli ya amiri jeshi mkuu na wasaidizi wake. So kama amiri jeshi mkuu haoni tija yoyote ya jeshi letu kupambana basi jeshi halitopambana.

Sasa kinachoendelea Congo kwa sasa ni tofauti na kile kilichokuwa kinaendelea kipindi kile cha 2013 hadi 2014. Kipindi kile tuliingia vitani kivita kweli kweli, huku amiri jeshi mkuu wa Tz akiwa na lengo la kumshikisha adabu amiri jeshi mkuu mwenzake wa nchi jirani. Hivyo ilikuwa ni vita ya serious ndiomaana tuliwachapa M23 bila huruma hadi wakakimbia wenyewe na kuacha silaha zao.

Lakini hii vita ya sasa hivi Congo sisi hatukwenda ki serious kwa sababu raisi amegundua kwamba hii vita haina faida yoyote kwetu. Sana sana tunaweza kupata hasara zaidi kuliko faida.

Hii ni kwa sababu mfadhili mkubwa anaewafadhili hawa M23 ndio mtu wa kwanza au wa pili kupitisha mizigo yake katika bandari yetu na ardhi yetu. Analipa mabilioni ya ushuru kila siku au kila week.

Hivyo tukiingia kwenye vita na mtu huyu ni sawa sawa na kuukata mkono wako mwenyewe unaokulisha. Kumbuka kwamba mfadhili huyo ana ukaribu na amiri jeshi mkuu wetu haswa kuhusu maswala ya kibiashara , upitishaji wa mizigo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi ya mfadhili. Sasa tukiwa serious kumtwanga itabidi atukimbie na kwenda kushirikiana na nchi nyingine kama vile Kenya nk.

Hizo ndio sababu kuu za sisi kutoiadhibu M23 kama kipindi kile. Serikali inaangalia hasara na faida inayopata kupitia vita hivi. Tukiwachapa basi hasara itakuwa kubwa kuliko faida. Lakini kwa vile sisi ni sehemu ya SADC na tumechaguliwa kwenda Congo. Basi acha jeshi letu litulie kule kujilia watoto wa kinyamulenge hadi muda ukapofika kurudishwa nyumban waruri kuendelea na maisha. But ukweli utabaki pale pale kwamba hapa East Africa hakuna jeshi wala kikundi cha wahuni kama hicho cha M23 ambacho kitaweza kupambana na JWTZ.
Umeandika hadithi nzuri sana mkuu ila fanya utafiti kwanza hasa wa kiuchumi. Kwa maana ya faida ya DRC kwa Tanzania na Faida Ya Rwanda kwa Tanzania..

Mbingu Na Ardhi!!

Naamini ukimaliza kufanya utafuti utafuta hii post!!
 
Hahahah!! Mpk mseme kumeanza kuchangamka.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Umeandika hadithi nzuri sana mkuu ila fanya utafiti kwanza hasa wa kiuchumi. Kwa maana ya faida ya DRC kwa Tanzania na Faida Ya Rwanda kwa Tanzania..

Mbingu Na Ardhi!!

Naamini ukimaliza kufanya utafuti utafuta hii post!!
Kwanini niifute mkuu?

Sisi kama taifa tunazihitaji nchi zote mbili. Na kwa mantiki hiyo hatuwezi kuchagua kuisaidia nchi moja dhidi ya nchi nyingine, kwa sababu hata hicho kidogo tunachopata kutoka kwenye hiyo nchi nyingine kuna majirani zetu wengine wanakikosa.

Kwa vile vita hiyo sio ya kwetu basi haina haja ya kuonesha wazi wazi kwamba tunapambana na nchi ambayo haijatuchokoza. Acha waliochokozana wayamalize wenyewe.

Ikishindikana kuna ushauri nimetoa kwenye post namba 65. Ufuatwe na Congo mara 1 halaf hao waasi waone moto wake.
 
Kuna sheria au Chapter mbili tofauti.
Moja inawataka kulinda aman bila kutumia nguvu na nyingine wanatumia nguvu , Kuna Chapter #6 na Chapter# 7 km sijakuelewa
Hii ya kutumia nguvu mpaka uruhusiwe.

Halafu kingine unapigana na mtu ambaye silaha yake muda wote inafanya kazi na wewe silaha Yako ndyo kwanza unakuta hyo siku umestukizwa ndyo unaanza nayo. lazima ikusumbue na ukizingatia kwenye shambulizi la ghafra majibizano lazima yawe ya papo kwa hapo kitendo Cha kusubiri ndyo unakwisha hivyo
 
Hii ya kutumia nguvu mpaka uruhusiwe.

Halafu kingine unapigana na mtu ambaye silaha yake muda wote inafanya kazi na wewe silaha Yako ndyo kwanza unakuta hyo siku umestukizwa ndyo unaanza nayo. lazima ikusumbue na ukizingatia kwenye shambulizi la ghafra majibizano lazima yawe ya papo kwa hapo kitendo Cha kusubiri ndyo unakwisha hivyo
Uko sahihii..
 
Hii ya kutumia nguvu mpaka uruhusiwe.

Halafu kingine unapigana na mtu ambaye silaha yake muda wote inafanya kazi na wewe silaha Yako ndyo kwanza unakuta hyo siku umestukizwa ndyo unaanza nayo. lazima ikusumbue na ukizingatia kwenye shambulizi la ghafra majibizano lazima yawe ya papo kwa hapo kitendo Cha kusubiri ndyo unakwisha hivyo
Chapter 7 , au Chapter VII ndio inaruhusu matumizi ya Nguvu
 
Unaweza kuifafanua hiyo chapter inayoruhusu matumizi ya nguvu.

I mean unaitumia hiyo chapter katika mazingira gani ili isionekane kua umevunja sheria za jeshi?
Kuna Chapter mbili , chapter 6 na chapter 7, ni mpk baraza la Usalama likae na kuona Kuna haja ya kutumia chapter ipi ktk kupata suluhu ya mgogoro husika

Chapter 7 Kama unakumbuka ndio iliyotumika kuwafurusha M23 kipindi kile na hiii tuliombwa na UN

Chapter 6 ni ulinzi wa kulinda aman bila kutumia nguvu

Chapter 7 ni ulinzi wa kulinda aman Kwa kutumia nguvu na kupora silaha Kwa waasi..nimekupa Kwa ufupi unaeza Ku google zaidi

Kumbuka ni lzm upewe kibali
 
Tuna jeshi zuri uongozi mbovu tangu 64 years. Ikibidi captain ashike mpini tu.
 
Jeshi letu saiv halina kiongozi shupavu ilitakiwa waziri wa mambo ya ndani na ulinzi awe mwanajeshi
Hiv jeshi masuala yake yanashughulikiwa na wizara ya mambo ya ndani?? Sio jeshi la polis ,magereza, fire etc??
 
Kuna Chapter mbili , chapter 6 na chapter 7, ni mpk baraza la Usalama likae na kuona Kuna haja ya kutumia chapter ipi ktk kupata suluhu ya mgogoro husika

Chapter 7 Kama unakumbuka ndio iliyotumika kuwafurusha M23 kipindi kile na hiii tuliombwa na UN

Chapter 6 ni ulinzi wa kulinda aman bila kutumia nguvu

Chapter 7 ni ulinzi wa kulinda aman Kwa kutumia nguvu na kupora silaha Kwa waasi..nimekupa Kwa ufupi unaeza Ku google zaidi

Kumbuka ni lzm upewe kibali
Shukran mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri.
 
Hiv jeshi masuala yake yanashughulikiwa na wizara ya mambo ya ndani?? Sio jeshi la polis ,magereza, fire etc??
Nafikiri alimaanisha wizara zote mbili yani ya mambo ya ndani, na ya ulinzi ziongozwe na mawaziri wanaojua mambo ya jeshi.

Hakumaanisha waziri wa mambo ya ndani aongoze wizara ya ulinzi. Numbisa
 
Mpaka kufatilia mkuu,siku hizi wizara zinabadilishwa badilishwa sana
Hapana hizo ni wizara mbili tofauti.

1. Wizara ya ulinzi ipo chini ya mhe. Dr Stargomena Tax.
2. Wizara ya mambo ya ndani kwa sasa ipo chini ya mhe. Bashungwa.
 
Back
Top Bottom