Zijue sababu za jeshi letu JWTZ kutokutoa kichapo kingine kwa M23, kama tulivyotoa mwaka 2013 hadi 2014

Hizo ni taratibu za askari wanaofanya kazi ya kulinda amani (Peace Keeping) ila ingekuwa ni vita rasmi,siku nyingi sana M23 wangeita maji MMA
Wewe unaujua ukweli mkuu. Sio hao chawa wa Kagame.
 
Hata hao M23, nao nidhaufu sana, niliona kipande kidogo cha front line kule TikTok ( nadhani mambo wao Ali live stream kimakosa Ile scene), nao wako disorganized, na wanatumia watoto wadogo vitani!
Kama M23 ni dhaifu mbona wameteka Goma ?
 
Hizo ni taratibu za askari wanaofanya kazi ya kulinda amani (Peace Keeping) ila ingekuwa ni vita rasmi,siku nyingi sana M23 wangeita maji MMA

Hao wajeda wetu mateka walikuwa usingizini wakati wanatekwa?
 
Kwa sasa hiyo M23 ya Sultan Makenga ni sehemu tu ya AFC ambacho ni combination ya makundi kibao ya waasi yenye silaha huko Mashariki ya DRC.

Zaidi ni kuwa kiongozi wa AFC hii ya jana tu bwana Nangaa Yubeluo anaweza kuwa na backup hata ndani ya DRC ukizingatia alikuwa Rais wa Tume Huru ya uchaguzi ya DRC yaani CENI tena juzi tu 2015-2021.

Kwa kifupi hii ya sasa siyo M23 ni AFC,sema M23 inatajwa sana sababu ndiye ITV yaani Super brand huko Mashariki.
 
Umeandika hadithi nzuri sana mkuu ila fanya utafiti kwanza hasa wa kiuchumi. Kwa maana ya faida ya DRC kwa Tanzania na Faida Ya Rwanda kwa Tanzania..

Mbingu Na Ardhi!!

Naamini ukimaliza kufanya utafuti utafuta hii post!!
Kumbuka DRC wanatumia pia bandari za Durban na Beira kwa kiwango kikubwa sana, the best way ni kutafuta namna ya kuvusha mizigo yao kupitia lake Tanganyika na siyo mpaka kuwe na nchi ya kati ya transit.
 
amani ya CONGO ni muhimu kuliko hata huo uhusiano wa kibiashara kati yetu na rwanda.
Muhimu kwa nani? Kama wao haoni umuhimu kuipigania kufa na kupona nchi yao sasa itakuwa muhimu kwa nani mwingine?
Kwetu hata wakichinjana 24/7 waendelee tu mpaka watakapoamua kuelewana.
 
Pamoja na faida ulizozitaja ni vyema M23 wakapigwa kidogo ili kulinda heshima ya JWTZ heshima ya jeshi ni muhimu kuliko faida za muda mfupi za kiuchumi lazima ku balance ili hali Kagame anasema hahusiki na M23 bali watwangwe halafu tuone. Wanasema mpige mbwa halafu mwenye mbwa atajitokeza.
 
Ikibidi kuwajambisha kidogo M23, tutawajambisha tu mkuu.
 
Ulichoandika kinaeleweka mkuu.
 
Kama tungeendelea kuwachapa basi wangekomaa na huu mpango pichani ili mizigo yao iwe inapitia huko kwa wenzetu.
Ndo uzwazwa huo. Unailenga Rwanda na mali za kuiba na kuiacha Zambia na jirani zake
 
Ndo uzwazwa huo. Unailenga Rwanda na mali za kuiba na kuiacha Zambia na jirani zake
Ni nani aliesema tunaiacha Zambia mkuu?
Kwani Zambia nayo inapigana na Rwanda?
 
Huna unalolifahamu
 
soko la Kongo ni kubwa kuliko la Rwanda ni swala tu la kukaa mguu sawa.
kibaya zaidi ubinafsi wa viongozi wetu unatuletea tabu kubwa kwetu.
ifike sehemu nafikiri Mama kwa heshima kabisa apumzike.
ukipoteza askari wawili kati ya mia ni kwamba umepoteza 2% ya askari ulionao lakini familia imepoteza 100% ya mzazi au mtu waliyemtegemea katika maisha yao hivyo kama anaona haina tija na inaguza maslahi binafsi na yuko tayari kula haramu kwakuwa ni DAMU ZA WATU wasio na hatia basi ajiunge moja kwa moja m23tuwapige wakongo vinginevyo wanaokufa pia ni waafrika wenzetu kwa mali zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…