Zijue sababu za jeshi letu JWTZ kutokutoa kichapo kingine kwa M23, kama tulivyotoa mwaka 2013 hadi 2014

Hata kongo wanapitisha mizigo yao bongo na wanatupa faida kubwa kuliko rwanda
 
Mkuu mbona haueleweki.. Mara useme soko la Congo kubwa kuliko la Rwanda, mara umlaumu raisi kwa vifo vya askari wawili ambao wametumwa kulinda hilo soko kubwa la Congo lisichukuliwe lote.

Sasa hapo point yako ni nini?
Kuwarudisha nyumban askari unaosema wanakufa ili hilo soko kubwa la Congo unalosema hapa tulikose lote?

Au unamaanisha nini?
 
Hata kongo wanapitisha mizigo yao bongo na wanatupa faida kubwa kuliko rwanda
Kwahiyo ndio tuamue kuchagua upande mmoja, ili tuuchangie upande mungine ambao haujawahi kutuchokoza, wala kutuvamia katika ardhi yetu?
 
Upuuuuziiiii!!Hizo hizo silaha zinazopita bandarini kupitia mfadhili uliyesema,Ndizo hizo hizo kunasiku zitakuja kututwanga tukiwa tumeshiba makande yanayotokana na hizo pesa anazolipa kupitisha Silaha.
 
Njia nyepesi ya kuwafurusha waasi ni kuwahamisha wakazi kwa muda eneo salama atakekaidi atahesabika ni muasi ahera Ina muhusu.
Ifanyike operation kama IDF ilivyofanya Gaza kuwashughulikia Hamasi kwa kuwahamisha wakazi wa Gaza kabla ya kushusha moto ambao magaidi wa Hamasi wakaomba poo.
Kwann tucheke na wahuni wachache Wanasababisha nchi za maziwa kukosa amani.
 
Nilimaanisha kujenga reli kuelekea Rwanda
Oh hapo nimekuelewa mkuu. Lakini kumbuka katika huo ujenzi Rwanda pia imekubali kuchangia, wakati Zambia haijatoa mchango wowote ili reli iweze kufika kwao.

Mpaka leo TAZARA imekwama kwa sababu ya kukosa maelewano mazuri kuhusu namna ya kuijenga upya reli ya TAZARA.

Lakini Rwanda linapokuja swala la kuleta maendeleo katika ardhi yake na raia wake, nchi hiyo ipo tayari kutumia gharama yoyote ili ifanikishe jambo hilo. Nafikiri hilo hata wewe unalijua.

So serikali haiwezi ku deal na nchi ambayo haiko tayari kushirikiana nayo kifedha kupelekea maendeleo katika nchi yao.

Waswahili wanasema "mkono mtupu haulambwi".
 
Wazo lako zuri mkuu.
 
Upuuuuziiiii!!Hizo hizo silaha zinazopita bandarini kupitia mfadhili uliyesema,Ndizo hizo hizo kunasiku zitakuja kututwanga tukiwa tumeshiba makande yanayotokana na hizo pesa anazolipa kupitisha Silaha.
Hawana ujanja wa kututwanga.
, maana silaha zao zote wanazopitisha bandarini tunazijua vizuri. Hivyo hawana ujanja wa kututisha kupitia silaha hizo.

Ndomaana Kikwete kipindi kile cha kutaka kuingia nao vitani, alipoenda pale Kagera katika sherehe za kuwakumbuka mashujaa wetu waliofariki katika vita vya Uganda.

Alisema watanzania laleni usingizi vizuri tena kwa kutulia. Kwa sababu jeshi letu na serikali yetu ipo kazini kuhakikisha hakuna mende yoyote atakaevuka mpaka kuja kufanya shambulizi katika ardhi ya Tanzania.

Alisema hivyo kwa sababu silaha zao zote alikuwa anazijua, nchi yao yote alikuwa anaijua na udhaifu wao wote alikuwa anaujua.

Wewe umeshiba mihogo na kulala chini ya mti kuhesabu ndege wanaopita angani huko kijijini kwenu. Hivyo mambo ya jeshi na uwezo wake hauwezi kuyajua. Naapa mbele ya Mungu kwamba huna unalojua kuhusu jeshi letu.
 
Kulikuwa na ulazima gani kuandika hayo maneno hapo chini?Wewe unajua Jeshi mana ni chakula chao wakiwa vitani,Shwaain
 
Bro kikwete hakufukuza wanyarwanda wanaoishi TZ, kule kagera, kwa taarifa yako, Rwanda kuna Watusi na wahutu, TZ kuna wanyambo, wanyankore, hawa wote ni jamii moja, kama ilivyo kwa Maasai wa TZ na Kenya, au mjaluo wa TZ na Mluo wa, Kenya!
 
Mimi nashangaa kuna reli ya tazara lakini malori mamia kwa mamia kila siku yanatoka dar to mbeya - to Zambia na kurudi kila siku. Njia ya dar to mbeya ingewekwa vizuri tungefaidika pakubwa. Tatizo viongozi wetu sio wafanyabiashara
 
Bro kikwete hakufukuza wanyarwanda wanaoishi TZ, kule kagera, kwa taarifa yako, Rwanda kuna Watusi na wahutu, TZ kuna wanyambo, wanyankore, hawa wote ni jamii moja, kama ilivyo kwa Maasai wa TZ na Kenya, au mjaluo wa TZ na Mluo wa, Kenya!
Mkuu acha kwanza mihemko ili uwe na muda wa kusoma vizuri kilichoandikwa, uwe na muda mzuri pia wa kutafakari unachoandika. Na zaidi uwe na muda mzuri wa ku comment bila kupindisha pindisha mada husika.

Mimi nimezungumzia wanyarwanda ambao walikuwa hawana vibali na sio wale wenye vibali. Halaf kingine sikuzungumzia watusi bali wanyarwanda wasiokuwa na vibali kwa umoja wao. Haijalishi ni muhutu, mtusi au mtwa.

Kingine ambacho nataka nikufahamishe ni kwamba sio kila mtusi ni Mnyarwanda. Kuna watusi ambao ni warundi pyu na hao ndio waliowasaidia watusi wa Rwanda kuingia kigali kutokea Burundi.

Wakati wa vita ya Rwanda, Burundi ilikuwa inaongozwa na watusi wa kirundi. Hivyo chini ya utawala wa wahutu huko Rwanda kuna watusi wengi walikimbilia Burundi kuomba hifadhi kwa watusi wenzao waliokuwa kwenye uongozi (Power),

Sasa sio kila mtusi anaeishi hayo maeneo uliyosema eti ni wanyarwanda. Wengine ni warundi pyu na wengine ndo kama hao uliosema. Lakini point yangu ni kwamba mimi sijazungumzia watusi, bali nimezungumzia wanyarwanda waliokuwa wanaishi Tz bila vibali huku wengi wao wakijifanya ni watanzania.
 
Mimi nashangaa kuna reli ya tazara lakini malori mamia kwa mamia kila siku yanatoka dar to mbeya - to Zambia na kurudi kila siku. Njia ya dar to mbeya ingewekwa vizuri tungefaidika pakubwa. Tatizo viongozi wetu sio wafanyabiashara
Mkuu wewe nafikiri sio mfuatiliaji wa mambo ya kimataifa. Ni kwamba njia ya kuelekea Rwanda, Congo na Burundi ina watu wengi wenye tija kuliko njia ya kuelekea Zambia na Malawi. Ni kwa sababu wewe haujawahi kufuatilia nchi ambazo zimekuwa zikitumia zaidi bandari yetu.

Halaf kingine Zambia ni kama Kenya. Ukiritimba ni mwingi sana. Haiwezi kupitia miezi 6 au mwaka bila kusikia malori yetu yamezuiwa kuingia Zambia nk.

Lakini huu upande mungine wa Rwanda, Burundi na Congo longo longo kama hizo huwa hazipo.

Hata hivyo naamini siku serikali ikiona njia ya huko Zambia inatija basi itajenga barabara nyingi zaidi ya zilizopo sasa. Tatizo wanaangalia tija ya nchi husika.

Unaweza kuwa na watoto wanne lkn ukaona kabisa mmoja ndio ana upendo, heshima na faida zaidi na wewe. Huku wengine wakiishia kuwa mateja wasiokujali wala kukuthamini. Kama mzazi ni lazima utawekeza akili na matumaini zaidi kwa yule anaekujali.
 
hapa kuna mawili huwenda mimi sikukuelewa au wewe hukunielewa pia lakini katika yote kila mmoja wetu arudi kusoma ujumbe wa mwenzake kisha tunaweza kuja na jibu zuri.
 
hapa kuna mawili huwenda mimi sikukuelewa au wewe hukunielewa pia lakini katika yote kila mmoja wetu arudi kusoma ujumbe wa mwenzake kisha tunaweza kuja na jibu zuri.
Ni kweli mkuu.
 
Angalia usije ukahamishwa wewd tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…