Zijue sababu za jeshi letu JWTZ kutokutoa kichapo kingine kwa M23, kama tulivyotoa mwaka 2013 hadi 2014

Halafu shida Sheria za munisco/UN ndyo tatizo pia,yaani kazi yao ni kulinda amani eti waasi wanavamia lakini wewe unaevamiwa usilete madhara kwa anaekuvamia. Hili kikwete alitishia kuondoka askari wake kwasababu ya hii sheria
Hapo ndipo lilipo tatizo. Yani wewe ushambuliwe, lkn usishambulie!!

Huu si upuuzi kbs.
 
hivi unajua manufaa ya kibiashara kwa nchi dhidi ya kufanya biashara na Kongo, kabla ya kupost kafanye utafiti
Tunamanufaa kwa nchi zote mbili. Hivyo hatuwezi kuingia kwenye matatizo ya kiuchumi kwa jiran mmoja kwa ajili ya kumsaidia jiran mungine katika ugomvi usiotuhusu.
 
Ok, sasa hao wanaolinda Amani ni Amani gani tofauti na hii ya vifo vya raia na wengine kupoteza makazi yao
Hakuna cha kulinda amani. Congo ni shamba la bibi. Hivyo kila nchi imetuma jeshi lake kwenda kuiba dhahabu na rasilimali zingine kupitia mgongo wa kwenda kulinda amani.
 
Kwani wakati wa JK kagame alikuwa hapitishi mizigo yake Dar port?
Upitishaji ulikuwa mdogo ukilinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya mzozo na kipindi cha mbele baada ya mzozo.

Na kulikuwa na mipango ya kuhakikisha Rwanda inaanza kutumia bandari ya Mombasa.
 
Attachments

  • Screenshot_20250127-183802.jpg
    Screenshot_20250127-183802.jpg
    345.2 KB · Views: 2
tuseme aache kupitshia kwetu ataptshia wapi? hebu amri itoke bhana emu 23 wakafilimbwe
Kama tungeendelea kuwachapa basi wangekomaa na huu mpango pichani ili mizigo yao iwe inapitia huko kwa wenzetu.
 
Attachments

  • Screenshot_20250127-183802.jpg
    Screenshot_20250127-183802.jpg
    345.2 KB · Views: 2
Niaje waungwana

Kwanza kabla ya kuelezea sababu za jeshi letu kutokutoa kichapo kwa M23, naomba kwanza nianze kuwapa historia tukufu ya jeshi letu la JWTZ au TPDF kwa nchi mbali mbali za Africa na Dunia kwa ujumla.

JTWZ chini ya baba wa taifa letu hayati mwl. Julius K. Nyerere ndio iliyoongoza mapambano yasioshindwa ambayo kwa asilimia kubwa yalisaidia nchi Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na Angola kuwa katika mikono salama na amani mpaka.

Idi Amin alitaka kujichanganya eti aichukue Bukoba, matokeo yake imechukuliwa nchi yake mwenyewe, halaf yeye akatoka nduki.

JWTZ hiyo hiyo chini ya utawala wa hayati mzee Ally Hassan Mwinyi ndio iliyotoa kichapo kitakatifu kwa jeshi la Burundi ambalo lilitaka kuteka sehemu ya mkoa wa Kigoma, kwa kisingizio cha kuja kuwapiga waasi wa CNDD-FDD ambao walikuwa wakipambana na serikali ya Burundi chini ya uongozi wa raisi meja Pierre Buyoya (rip).

Ni kwamba Buyoya na serikali yake walikuwa wanadai kwamba serikali ya Tz imekuwa ikitoa msaada wa kuwahifadhi waasi hao katika maeneo ya mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Burundi. Hivyo dawa ya kukomesha jambo hilo ilikuwa ni kuivamia Tz (Buyoya sijui nani alimhadaa ashike moto kwa mkono), kuichapa na kuteka maeneo yote aliyodai yanatumiwa na waasi nchini kwetu kufanyia training na kupanga mipango ya kuingia Burundi kufanya maangamizi mara kwa mara.

Basi bwana Buyoya akaamuru jeshi lake lifanye ambush kupitia mipaka ya ardhini na majini. Aisee kilichotokea kwa upande wa Burundi mpaka leo ni hasara kwa nchi yao.

Kuna jamaa fulan Mrundi anasema kuwa sehemu hiyo iliyoangukiwa na kombora kutoka Tz mpaka sasa hapajawahi kuota chochote, na wala kujengwa chochote. Ni kama vile ardhi imeunguzwa hata kwa kutengenezea tofali za kuchoma haufai kudadeki. Baada ya lile tukio Buyoya na warundi wenzie wakawa wapole na askari waliokuwa wanalinda mipaka ya majini na ardhini kwa upande wa Burundi akawasogeza mbali mno kutoka mpakani.

Chini ya utawala wa raisi Kikwete kuna raisi alikuwa ashapinduliwa hapo Comoro, ikabidi aje kuomba msaada wa kumrudisha madarakani. Ni kitendo cha masaa tu raisi akarudishwa na wahuni waliopanga mapinduzi wakatiwa nguvuni.

Pia chini ya Kikwete raisi wa Burundi hayati Pierre Ngurunziza alikuwa ameshapinduliwa na kuambiwa abaki huku huku Tz alipokuwa amekuja kwa mkutano wa amani. Baada ya ujinga huo, Kikwete akatuma kikosi kidogo tu cha wanajeshi wa kumrudisha nchini kwake salama na kuwatia nguvuni wapuuzi wachache waliompindua raisi wao. Bila kuchelewa jeshi letu likamrudisha Ngurunziza, ila wapinduaji wakafanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani.

Chini ya utawala huo huo wa Kikwete jeshi letu lilitoa kipondo ambacho kilisababisha waasi wa M23 kutimkia Uganda na Rwanda. Na hii ni baada ya raisi wa Rwanda mhe. Paul Kagame kumletea dharau Kikwete na jeshi letu hali iliyosababisha Kikwete adili na kila kinachompaka Kagame jeuri. Alianza na wanyarwanda waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria, baadae akarukia Congo kuwafyeka M23 ambao waliaminika kuwa ni jeshi dogo la Rwanda. Kisha akasogeza jeshi mkoa wa Kagera kuwa tayari kuingia Kigali, sema hekima Za mzee Mwinyi na Mkapa zilichangia kumfanya Kikwete asivaamie Rwanda kumtoa adui yake.

Tukiachana na hayo. Tushapandikiziwa vikundi vya waasi kwa mgongo wa dini huko Tanga, Kibiti nk. Lakini jeshi letu halijawahi kucheka na kima wote tumewaangamizi kwa muda mfupi sana.

Hizo operations zote nilizoeleza hapo juu zilitekelezwa na TPDF bila kushindwa wala kurudi nyuma. Hivyo uwezo wa kumpiga adui toka miaka hiyo tulikuwa, tunao na tutaendelea kuwa nao. Huu ndio ukweli halisi.

Sasa tukija kwa hii vita ya sasa ya M23. Kuna watu wanajiuliza iweje M23 hii tulioichapa wakati wa Kikwete imetushinda wakati wa Samia!!

Ukweli ni kwamba jeshi letu lipo imara, vizuri na tayari kwa mapambano wakati wowote bila kujali ni nani aliepo madarakani. Kikubwa ambacho hufanyika ni kuliongezea silaha za kisasa, mbinu mpya za kijeshi, nguvu na morali zaidi za kulitumikia jeshi la wananchi. Pia jeshi letu hupambana kupitia kauli ya amiri jeshi mkuu na wasaidizi wake. So kama amiri jeshi mkuu haoni tija yoyote ya jeshi letu kupambana basi jeshi halitopambana.

Sasa kinachoendelea Congo kwa sasa ni tofauti na kile kilichokuwa kinaendelea kipindi kile cha 2013 hadi 2014. Kipindi kile tuliingia vitani kivita kweli kweli, huku amiri jeshi mkuu wa Tz akiwa na lengo la kumshikisha adabu amiri jeshi mkuu mwenzake wa nchi jirani. Hivyo ilikuwa ni vita ya serious ndiomaana tuliwachapa M23 bila huruma hadi wakakimbia wenyewe na kuacha silaha zao.

Lakini hii vita ya sasa hivi Congo sisi hatukwenda ki serious kwa sababu raisi amegundua kwamba hii vita haina faida yoyote kweli. Sana sana tunaweza kupata hasara zaidi kuliko faida.

Hii ni kwa sababu mfadhili mkubwa anaewafadhili hawa M23 ndio mtu wa kwanza au wa pili kupitisha mizigo yake katika bandari yetu na ardhi yetu. Analipa mabilioni ya ushuru kila siku au kila week.

Hivyo tukiingia kwenye vita na mtu huyu ni sawa sawa na kuukata mkono wako mwenyewe unaokulisha. Kumbuka kwamba mfadhili huyo ana ukaribu na amiri jeshi mkuu wetu haswa kuhusu maswala ya kibiashara , upitishaji wa mizigo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi ya mfadhili. Sasa tukiwa serious kumtwanga itabidi atukimbie na kwenda kushirikiana na nchi nyingine kama vile Kenya nk.

Hizo ndio sababu kuu za sisi kutoiadhibu M23 kama kipindi kile. Serikali inaangalia hasara na faida inayopata kupitia vita hivi. Tukiwachapa basi hasara itakuwa kubwa kuliko faida. Lakini kwa vile sisi ni sehemu ya SADC na tumechaguliwa kwenda Congo. Basi acha jeshi letu litulie kule kujilia watoto wa kinyamulenge hadi muda ukapofika kurudishwa nyumban waruri kuendelea na maisha. But ukweli utabaki pale pale kwamba hapa East Africa hakuna jeshi kikundi cha wahuni kama hicho cha M23 kitaweza kupambana na JWTZ.
Historia Moja umeisahau. Kuna mwaka Rais wa kwanza wa Zambia Kenneth Kaunda alipinduliwa na jeshi ndani ya masaa machache JWTZ walipindua meza. Ilikua ni awamu ya Mwinyi.
 
JWTZ hiyo hiyo chini ya utawala wa hayati mzee Ally Hassan Mwinyi ndio iliyotoa kichapo kitakatifu kwa jeshi la Burundi ambalo lilitaka kuteka sehemu ya mkoa wa Kigoma, kwa kisingizio cha kuja kuwapiga waasi wa CNDD-FDD ambao walikuwa wakipambana na serikali ya Burundi chini ya uongozi wa raisi meja Pierre Buyoya (rip).
Ilikua ni kipindi cha rais Mkapa.
Kilichotokea kwenye zile chochoko ni kwamba wakata Buyoya akitafuta kuungwa mkono kuishambulia Tanzania, pale karibu na mpakani tulikuwa na vijana wana nyege sana ya vita kuliko maelezo.

Wakati jambo lile likijadiliwa bungeni, JK alikuwa ni waziri mambo ya nje, akitoa taarifa bungeni akasema "wakipiga risasi mbili, sisi tutajibu saba".

Kauli ile ilishangiliwa sana na wale vijana. Ghafla Buyoa akatangaza kuwa Tanzania imevamia rasmi Burundi. Ile taarifa ilitanazwakote Uliwenguni, nchi ilistuliwa na taarifa ile kupitia amka na BBC.

Kilichotokea, Buyoya alisogeza majesho yake ndani ya Km 15 kutoka mpakani, kikanuni hapa yeye ndiye alikuwa ameivamia Tanzania, il kilichofanya atamke kuvamiwa, pale kambini wale vijana wenye nyege ya vita wali 'misbehave', waliona wanacheleweshwa , 'wakatoroka', wakaingia Burundi....

Itaendelea...
 
Asante sana mkuu kwa ukumbusho murua kabisa 🤝
 
Tunasubiri muendelezo mkuu ili tuweke kumbukumbu sawa.
 
Kuna mwanajeshi wa Tanzania amefariki Congo anakuja kuzikwa Zanzibar kesho

In shaa Allah nitahudhuria kwenye haya maziko kma nitakua nisharejea kwenye mizunguko
Kifo hutokea popote, iwe Congo, Burundi, Tanzania, Kenya au Msumbiji utakufa tu. So sioni ajabu huyo mwanajeshi kufia Congo kama kifo ilipangwa afie huko maana kuna wengine wanafia Tanzania hapo hapo.
 
Hakuna cha kulinda amani. Congo ni shamba la bibi. Hivyo kila nchi imetuma jeshi lake kwenda kuiba dhahabu na rasilimali zingine kupitia mgongo wa kwenda kulinda amani.
Mkuu ni nchi tuu ikiamua inapeleka jeshi??? Na wanalipwa nani?
 
Hapana mimi nazungumzia zile nchi ambazo zimekubaliwa na Congo kupelekea wanajeshi wao huko.

Kulipwa inategemea. Kwa mfano wale waliopelekwa kupitia UN wanalipwa na UN. Kisha wale waliopelekwa kupitia jumuiya ya SADC wanalipwa na Jumuiya ya SADC wakisaidiwa na Umoja wa nchi za Africa mkuu.
 
Niaje waungwana

Kwanza kabla ya kuelezea sababu za jeshi letu kutokutoa kichapo kwa M23, naomba kwanza nianze kuwapa historia tukufu ya jeshi letu la JWTZ au TPDF kwa nchi mbali mbali za Africa na Dunia kwa ujumla.

JTWZ chini ya baba wa taifa letu hayati mwl. Julius K. Nyerere ndio iliyoongoza mapambano yasioshindwa ambayo kwa asilimia kubwa yalisaidia nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na Angola kuwa katika mikono salama, na amani ya kudumu mpaka leo.

Idi Amin alitaka kujichanganya eti aichukue Bukoba, matokeo yake imechukuliwa nchi yake mwenyewe, halaf yeye akatoka nduki.

JWTZ hiyo hiyo chini ya utawala wa hayati mzee Ally Hassan Mwinyi ndio iliyotoa kichapo kitakatifu kwa jeshi la Burundi ambalo lilitaka kuteka sehemu ya mkoa wa Kigoma, kwa kisingizio cha kuja kuwapiga waasi wa CNDD-FDD ambao walikuwa wakipambana na serikali ya Burundi chini ya uongozi wa raisi meja Pierre Buyoya (rip).

Ni kwamba Buyoya na serikali yake walikuwa wanadai kwamba serikali ya Tz imekuwa ikitoa msaada wa kuwahifadhi waasi hao katika maeneo ya mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Burundi. Hivyo dawa ya kukomesha jambo hilo ilikuwa ni kuivamia Tz (Buyoya sijui nani alimhadaa ashike moto kwa mkono), kuichapa na kuteka maeneo yote aliyodai yanatumiwa na waasi nchini kwetu kufanyia training na kupanga mipango ya kuingia Burundi kufanya maangamizi mara kwa mara.

Basi bwana Buyoya akaamuru jeshi lake lifanye ambush kupitia mipaka ya ardhini na majini. Aisee kilichotokea kwa upande wa Burundi mpaka leo ni hasara kwa nchi yao.

Kuna jamaa fulan Mrundi anasema kuwa sehemu hiyo iliyoangukiwa na kombora kutoka Tz mpaka sasa hapajawahi kuota chochote, na wala kujengwa chochote. Ni kama vile ardhi imeunguzwa hata kwa kutengenezea tofali za kuchoma haufai kudadeki. Baada ya lile tukio Buyoya na warundi wenzie wakawa wapole na askari waliokuwa wanalinda mipaka ya majini na ardhini kwa upande wa Burundi akawasogeza mbali mno kutoka mpakani.

Chini ya utawala wa raisi Kikwete kuna raisi alikuwa ashapinduliwa hapo Comoro, ikabidi aje kuomba msaada wa kumrudisha madarakani. Ni kitendo cha masaa tu raisi akarudishwa na wahuni waliopanga mapinduzi wakatiwa nguvuni.

Pia chini ya Kikwete raisi wa Burundi hayati Pierre Ngurunziza alikuwa ameshapinduliwa na kuambiwa abaki huku huku Tz alipokuwa amekuja kwa mkutano wa amani. Baada ya ujinga huo, Kikwete akatuma kikosi kidogo tu cha wanajeshi wa kumrudisha nchini kwake salama na kuwatia nguvuni wapuuzi wachache waliompindua raisi wao. Bila kuchelewa jeshi letu likamrudisha Ngurunziza, ila wapinduaji wakafanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani.

Chini ya utawala huo huo wa Kikwete jeshi letu lilitoa kipondo ambacho kilisababisha waasi wa M23 kutimkia Uganda na Rwanda. Na hii ni baada ya raisi wa Rwanda mhe. Paul Kagame kumletea dharau Kikwete na jeshi letu hali iliyosababisha Kikwete adili na kila kinachompaka Kagame jeuri. Alianza na wanyarwanda waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria, baadae akarukia Congo kuwafyeka M23 ambao waliaminika kuwa ni jeshi dogo la Rwanda. Kisha akasogeza jeshi mkoa wa Kagera kuwa tayari kuingia Kigali, sema hekima Za mzee Mwinyi na Mkapa zilichangia kumfanya Kikwete asivaamie Rwanda kumtoa adui yake.

Tukiachana na hayo. Tushapandikiziwa vikundi vya waasi kwa mgongo wa dini huko Tanga, Kibiti nk. Lakini jeshi letu halijawahi kucheka na kima wote tumewaangamizi kwa muda mfupi sana.

Hizo operations zote nilizoeleza hapo juu zilitekelezwa na TPDF bila kushindwa wala kurudi nyuma. Hivyo uwezo wa kumpiga adui toka miaka hiyo tulikuwa, tunao na tutaendelea kuwa nao. Huu ndio ukweli halisi.

Sasa tukija kwa hii vita ya sasa ya M23. Kuna watu wanajiuliza iweje M23 hii tulioichapa wakati wa Kikwete imetushinda wakati wa Samia!!

Ukweli ni kwamba jeshi letu lipo imara, vizuri na tayari kwa mapambano wakati wowote bila kujali ni nani aliepo madarakani. Kikubwa ambacho hufanyika ni kuliongezea silaha za kisasa, mbinu mpya za kijeshi, nguvu na morali zaidi za kulitumikia jeshi la wananchi. Pia jeshi letu hupambana kupitia kauli ya amiri jeshi mkuu na wasaidizi wake. So kama amiri jeshi mkuu haoni tija yoyote ya jeshi letu kupambana basi jeshi halitopambana.

Sasa kinachoendelea Congo kwa sasa ni tofauti na kile kilichokuwa kinaendelea kipindi kile cha 2013 hadi 2014. Kipindi kile tuliingia vitani kivita kweli kweli, huku amiri jeshi mkuu wa Tz akiwa na lengo la kumshikisha adabu amiri jeshi mkuu mwenzake wa nchi jirani. Hivyo ilikuwa ni vita ya serious ndiomaana tuliwachapa M23 bila huruma hadi wakakimbia wenyewe na kuacha silaha zao.

Lakini hii vita ya sasa hivi Congo sisi hatukwenda ki serious kwa sababu raisi amegundua kwamba hii vita haina faida yoyote kwetu. Sana sana tunaweza kupata hasara zaidi kuliko faida.

Hii ni kwa sababu mfadhili mkubwa anaewafadhili hawa M23 ndio mtu wa kwanza au wa pili kupitisha mizigo yake katika bandari yetu na ardhi yetu. Analipa mabilioni ya ushuru kila siku au kila week.

Hivyo tukiingia kwenye vita na mtu huyu ni sawa sawa na kuukata mkono wako mwenyewe unaokulisha. Kumbuka kwamba mfadhili huyo ana ukaribu na amiri jeshi mkuu wetu haswa kuhusu maswala ya kibiashara , upitishaji wa mizigo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi ya mfadhili. Sasa tukiwa serious kumtwanga itabidi atukimbie na kwenda kushirikiana na nchi nyingine kama vile Kenya nk.

Hizo ndio sababu kuu za sisi kutoiadhibu M23 kama kipindi kile. Serikali inaangalia hasara na faida inayopata kupitia vita hivi. Tukiwachapa basi hasara itakuwa kubwa kuliko faida. Lakini kwa vile sisi ni sehemu ya SADC na tumechaguliwa kwenda Congo. Basi acha jeshi letu litulie kule kujilia watoto wa kinyamulenge hadi muda ukapofika kurudishwa nyumban waruri kuendelea na maisha. But ukweli utabaki pale pale kwamba hapa East Africa hakuna jeshi wala kikundi cha wahuni kama hicho cha M23 ambacho kitaweza kupambana na JWTZ.
🛀
 
Back
Top Bottom