rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Nyie mnaosema mama anaupiga mwingi inabidi muwe mstari wa mbeleInabidi upelekwe DRC ukasaidie kuwapiga M23
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyie mnaosema mama anaupiga mwingi inabidi muwe mstari wa mbeleInabidi upelekwe DRC ukasaidie kuwapiga M23
Kuna sheria au Chapter mbili tofauti.Halafu shida Sheria za munisco/UN ndyo tatizo pia,yaani kazi yao ni kulinda amani eti waasi wanavamia lakini wewe unaevamiwa usilete madhara kwa anaekuvamia. Hili kikwete alitishia kuondoka askari wake kwasababu ya hii sheria
Kuna sheria ya kutumia nguvuNguvu inaweza kutumika pale tu inapohitajika kufanya hivyo.
Propaganda za Nyerere? He he he.Propaganda za Nyerere kama zipi mkuu?
Kuna batu banafaidika na kuchinjwa chinjwa na majambia.🤲🙌🏿Kumbuka kwamba mfadhili huyo ana ukaribu na amiri jeshi mkuu wetu haswa kuhusu maswala ya kibiashara , upitishaji wa mizigo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi ya mfadhili. Sasa tukiwa serious kumtwanga itabidi atukimbie na kwenda kushirikiana na nchi nyingine kama vile Kenya nk.
Ni bazuri kwa propagand. Ingekuwa ni kwli wana uwezo wa hali ya juu, na bamewapa ba israel vifaa vya kivita enye teknolojia ya juu, Kwanini vita ya Gaza imechukua muda mrefu?Marekani ni nchi kubwa yenye teknolojia na uwezo wa hali ya juu. Lakin mpaka leo uwezo wao na teknolojia yao vimeshindwa kujua chanzo cha moto na namna ya kuwasaidia kuzima moto unaoendelea kuwaka huko Los Angeles.
Je na wenyewe tuseme ni dhaifu?
Kama nilivyoeleza huko juu kwamba Congo ni shamba la bibi, hivyo kila mwenye ubavu kidogo anaingia kumjambisha bibi ili atoke na chochote.Baeleze Batanzani.
Ipo video inayosambaa mitandaoni inayoonyesha M23 wakifanya mashambulizi, kwenye hayo mashambulizi unabasikia bakisema 'Alah Akbar'
Kwa maelezo yako hapa chini, Je naweza unganisha dot?
Naona ninawesa.
Katika moja ya uropokaji wa Dictator Trump, alisikika akisema "Yule Prince nae yupo kule kwa bacongo" anatengeneza mabilioni, sio franga, sio shilingi, mabilioni ya madola...ushanielewa hapo?
Sasa nikiweka moja na mbili na hizi taarifa zako, naeza sema ,huyo Prince aliyetajwa ndie huyo huyo? yupo karibu na mkulu, ama nakosea batanzani?
Soma 👉
Kuna batu banafaidika na kuchinjwa chinjwa na majambia.🤲🙌🏿
🤣🤣🤣🤣Ni bazuri kwa propagand. Ingekuwa ni kwli wana uwezo wa hali ya juu, na bamewapa ba israel vifaa vya kivita enye teknolojia ya juu, Kwanini vita ya Gaza imechukua muda mrefu?
Balisema wanawenda kuangamiza Hamas wote.
Juzi wakibadilishana mateka, Hamas bameonekana wakiwa wamenawili, bana nguo na magqri mapya? Ikiwa ina maana bado wapo.
How?
Kwani kipindi cha Kikwete huyo mdau halikiwa hatumii bandari yetu? Bandari kavu ya kahama ilianza lini kwa kusudi gani? Hoja hii dhaifu labda ile nyingine kuwa unaangalia kuoata pesa kwa mwamvuli wa UNHakuna cha aibu mkuu. Hii ni diplamasia yenye faida kwetu. Wanajeshi kuwa kule wanalipwa. Lakini pia tulieenda kumchapa hatumchapi kwa kuhofia kwamba tukimchapa kisawa sawa ataacha kutumia bandari yetu kupitisha mizigo yake.
Ardhi ya Congo sisi haituhusu, sasa hatuwezi kukubali kumpoteza mtu anaeiingizia nchi yetu mamilioni ya shilingi kupitisha mizigo yake katika ardhi yetu kwa sababu ya kuisaidia Congo.
Vita hii tunaweza kuichukulia serious kama adui atasogea kuiteka Kigoma au Kagera. Ila kama ni vita vinavyopiganwa Congo basi acha jeshi letu likatengeneze mamilioni bila kuharibu uhusiano na yule tunaetakiwa kumtwanga.
Thats allKama nilivyoeleza huko juu kwamba Congo ni shamba la bibi, hivyo kila mwenye ubavu kidogo anaingia kumjambisha bibi ili atoke na chochote.
Congo haiibwi na Prince pekee bali inaibwa na mataifa mengi likiwemo hilo taifa la Trump. Rejea mauaji ya Patrick Lumumba ambayo yametokea kabla hata huyo Prince tunaemsema hapa hajazaliwa. Rejea mauaji ya Desiree Kabila, Mobutu nk ambao wameuwawa before hata huyo Prince hajajua kujitoa kamasi.
Congo ni nchi yenye utajiri mkubwa wa madini, hivyo nchi zote kubwa kubwa ikiwemo Belgium ambayo iliitawala Congo wanatumia udhaifu wa nchi hiyo kutengeneza vikundi vya waasi ili nchi isitawalike na wao waibe.
Kwahivyo kila nchi inayoiba madini Congo inatumia njia zake. Zipo zinazomsapoti huyo mfadhili wa M23 kwa silaha na mbinu kijeshi ili kuwachapa wanajeshi wa Congo kiurahisi. Na zipo zile zinazowatumia hao wanaosema alahu akbal ilimradi mission zao za kuiba ziende vizuri.
So ukiiangalia kwa makini utaona kuwa Congo inaibiwa na US, UK, France, Belgium, Saudia nk na ndiomaana haujawahi kusikia au kuona wakimuwekea vikwazo mdhamini wa hao M23 japo wanamjua na kumkemea kinafiki kila siku.
amani ya CONGO ni muhimu kuliko hata huo uhusiano wa kibiashara kati yetu na rwanda.Tunamanufaa kwa nchi zote mbili. Hivyo hatuwezi kuingia kwenye matatizo ya kiuchumi kwa jiran mmoja kwa ajili ya kumsaidia jiran mungine katika ugomvi usiotuhusu.
Umeandika blah blah nyingi za uongo na kweli lakini hitimisho lako limekuwa duni sana.Niaje waungwana
Kwanza kabla ya kuelezea sababu za jeshi letu kutokutoa kichapo kwa M23, naomba kwanza nianze kuwapa historia tukufu ya jeshi letu la JWTZ au TPDF kwa nchi mbali mbali za Africa na Dunia kwa ujumla.
JTWZ chini ya baba wa taifa letu hayati mwl. Julius K. Nyerere ndio iliyoongoza mapambano yasioshindwa ambayo kwa asilimia kubwa yalisaidia nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na Angola kuwa katika mikono salama, na amani ya kudumu mpaka leo.
Idi Amin alitaka kujichanganya eti aichukue Bukoba, matokeo yake imechukuliwa nchi yake mwenyewe, halaf yeye akatoka nduki.
JWTZ hiyo hiyo chini ya utawala wa hayati mzee Ally Hassan Mwinyi ndio iliyotoa kichapo kitakatifu kwa jeshi la Burundi ambalo lilitaka kuteka sehemu ya mkoa wa Kigoma, kwa kisingizio cha kuja kuwapiga waasi wa CNDD-FDD ambao walikuwa wakipambana na serikali ya Burundi chini ya uongozi wa raisi meja Pierre Buyoya (rip).
Ni kwamba Buyoya na serikali yake walikuwa wanadai kwamba serikali ya Tz imekuwa ikitoa msaada wa kuwahifadhi waasi hao katika maeneo ya mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Burundi. Hivyo dawa ya kukomesha jambo hilo ilikuwa ni kuivamia Tz (Buyoya sijui nani alimhadaa ashike moto kwa mkono), kuichapa na kuteka maeneo yote aliyodai yanatumiwa na waasi nchini kwetu kufanyia training na kupanga mipango ya kuingia Burundi kufanya maangamizi mara kwa mara.
Basi bwana Buyoya akaamuru jeshi lake lifanye ambush kupitia mipaka ya ardhini na majini. Aisee kilichotokea kwa upande wa Burundi mpaka leo ni hasara kwa nchi yao.
Kuna jamaa fulan Mrundi anasema kuwa sehemu hiyo iliyoangukiwa na kombora kutoka Tz mpaka sasa hapajawahi kuota chochote, na wala kujengwa chochote. Ni kama vile ardhi imeunguzwa hata kwa kutengenezea tofali za kuchoma haufai kudadeki. Baada ya lile tukio Buyoya na warundi wenzie wakawa wapole na askari waliokuwa wanalinda mipaka ya majini na ardhini kwa upande wa Burundi akawasogeza mbali mno kutoka mpakani.
Chini ya utawala wa raisi Kikwete kuna raisi alikuwa ashapinduliwa hapo Comoro, ikabidi aje kuomba msaada wa kumrudisha madarakani. Ni kitendo cha masaa tu raisi akarudishwa na wahuni waliopanga mapinduzi wakatiwa nguvuni.
Pia chini ya Kikwete raisi wa Burundi hayati Pierre Ngurunziza alikuwa ameshapinduliwa na kuambiwa abaki huku huku Tz alipokuwa amekuja kwa mkutano wa amani. Baada ya ujinga huo, Kikwete akatuma kikosi kidogo tu cha wanajeshi wa kumrudisha nchini kwake salama na kuwatia nguvuni wapuuzi wachache waliompindua raisi wao. Bila kuchelewa jeshi letu likamrudisha Ngurunziza, ila wapinduaji wakafanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani.
Chini ya utawala huo huo wa Kikwete jeshi letu lilitoa kipondo ambacho kilisababisha waasi wa M23 kutimkia Uganda na Rwanda. Na hii ni baada ya raisi wa Rwanda mhe. Paul Kagame kumletea dharau Kikwete na jeshi letu hali iliyosababisha Kikwete adili na kila kinachompaka Kagame jeuri. Alianza na wanyarwanda waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria, baadae akarukia Congo kuwafyeka M23 ambao waliaminika kuwa ni jeshi dogo la Rwanda. Kisha akasogeza jeshi mkoa wa Kagera kuwa tayari kuingia Kigali, sema hekima Za mzee Mwinyi na Mkapa zilichangia kumfanya Kikwete asivaamie Rwanda kumtoa adui yake.
Tukiachana na hayo. Tushapandikiziwa vikundi vya waasi kwa mgongo wa dini huko Tanga, Kibiti nk. Lakini jeshi letu halijawahi kucheka na kima wote tumewaangamizi kwa muda mfupi sana.
Hizo operations zote nilizoeleza hapo juu zilitekelezwa na TPDF bila kushindwa wala kurudi nyuma. Hivyo uwezo wa kumpiga adui toka miaka hiyo tulikuwa, tunao na tutaendelea kuwa nao. Huu ndio ukweli halisi.
Sasa tukija kwa hii vita ya sasa ya M23. Kuna watu wanajiuliza iweje M23 hii tulioichapa wakati wa Kikwete imetushinda wakati wa Samia!!
Ukweli ni kwamba jeshi letu lipo imara, vizuri na tayari kwa mapambano wakati wowote bila kujali ni nani aliepo madarakani. Kikubwa ambacho hufanyika ni kuliongezea silaha za kisasa, mbinu mpya za kijeshi, nguvu na morali zaidi za kulitumikia jeshi la wananchi. Pia jeshi letu hupambana kupitia kauli ya amiri jeshi mkuu na wasaidizi wake. So kama amiri jeshi mkuu haoni tija yoyote ya jeshi letu kupambana basi jeshi halitopambana.
Sasa kinachoendelea Congo kwa sasa ni tofauti na kile kilichokuwa kinaendelea kipindi kile cha 2013 hadi 2014. Kipindi kile tuliingia vitani kivita kweli kweli, huku amiri jeshi mkuu wa Tz akiwa na lengo la kumshikisha adabu amiri jeshi mkuu mwenzake wa nchi jirani. Hivyo ilikuwa ni vita ya serious ndiomaana tuliwachapa M23 bila huruma hadi wakakimbia wenyewe na kuacha silaha zao.
Lakini hii vita ya sasa hivi Congo sisi hatukwenda ki serious kwa sababu raisi amegundua kwamba hii vita haina faida yoyote kwetu. Sana sana tunaweza kupata hasara zaidi kuliko faida.
Hii ni kwa sababu mfadhili mkubwa anaewafadhili hawa M23 ndio mtu wa kwanza au wa pili kupitisha mizigo yake katika bandari yetu na ardhi yetu. Analipa mabilioni ya ushuru kila siku au kila week.
Hivyo tukiingia kwenye vita na mtu huyu ni sawa sawa na kuukata mkono wako mwenyewe unaokulisha. Kumbuka kwamba mfadhili huyo ana ukaribu na amiri jeshi mkuu wetu haswa kuhusu maswala ya kibiashara , upitishaji wa mizigo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yetu na nchi ya mfadhili. Sasa tukiwa serious kumtwanga itabidi atukimbie na kwenda kushirikiana na nchi nyingine kama vile Kenya nk.
Hizo ndio sababu kuu za sisi kutoiadhibu M23 kama kipindi kile. Serikali inaangalia hasara na faida inayopata kupitia vita hivi. Tukiwachapa basi hasara itakuwa kubwa kuliko faida. Lakini kwa vile sisi ni sehemu ya SADC na tumechaguliwa kwenda Congo. Basi acha jeshi letu litulie kule kujilia watoto wa kinyamulenge hadi muda ukapofika kurudishwa nyumban waruri kuendelea na maisha. But ukweli utabaki pale pale kwamba hapa East Africa hakuna jeshi wala kikundi cha wahuni kama hicho cha M23 ambacho kitaweza kupambana na JWTZ.
ChaiNiaje waungwana