mwanajamii26
Member
- Dec 16, 2014
- 58
- 13

Kama ilivyo ada kuwa upatapo mtoto ni lazima umpatie jina, lakini wengi wamekuwa wakiwapa watoto wao majina pasi na kuwa na sababu ya kwanini wanafanya hivyo.
Lakini hii ni tofauti kwa msanii Jayzee na mkewe Beyonce ambao wameamua kumpa mtoto wao jina la Blue Ivy kwa sababu zifuatazo;
Kwanza BLUE ni rangi ambayo inapendwa sana na mwanamziki Jay z, na ndio maana ameweza kutoa albam zenye jina la BLUE ambazo ni Blueprint 1, Blueprint 2, Blueprint 3.
IVY inawakilisha namba 4 (Iv=4 katika namba za kirumi). Na hii ni kwa sababu namba hii inawagusa wote, Beyonce na Jay Z mwenyewe kwani hii ni namba inayowakilisha tarehe zao za kuzaliwa ambapo Jay Z amezaliwa 4 December, na beyonce amezaliwa 4 September na pia waliweza kufunga ndoa tarehe 4 April, na kwa sababu hizo wakaamua kumwita mtoto wao BLUE IVY..

