Zijue sheria kandamizi dhidi ya wanaume

Zijue sheria kandamizi dhidi ya wanaume

Fugwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
1,676
Reaction score
663
WanaJF,
Naomba tu-share kuhusu uwepo wa sheria kandamizi, katiri na chinja chinja dhidi wanaume. Baadhi ya sheria hizo ni pamoja na:

  • Marriage Act
  • Sexual offences Special provision Act (SOSPA)
  • Armed Robbery
Nianze na Sheria ya Ndoa (Marriage Act); sheria hii kwa ujumla wake imefungua macho mapana kwa upande wa akina mama na kuwafumbia macho kabisa kabisa wanaume. Tatizo langu na sheria hii ni mgawanyo sawa wa mali kati ya wanandoa pale ndoa inapovunjika bila kujali nani kachangia nini. Tatizo lingine ni jukumu la kutunza familia ambalo ametwikwa mwanaume. Madhara yake kwa sasa yapo dhahiri; kwamba wanaume wengi wameurudia umaskini baada ya kuporwa mali na wenza wao kisa wamechuma pamoja hata kama mama alikuwa anapika chapati home ambapo watagawana sawia. Tatizo lingine kuna kosa la desertion of child, wanaume wengi wamo gerezani kwa kosa hilo si rahisi kumkuta mwanamke amefungwa kwa kosa hilo (ushahidi uko wazi). Huu ni uonevu na hujuma za wazi mchana kweupe dhidi ya wanaume.

Tuje kwenye sheria ya ubakaji niite hivyo (sexual offences special provision Act)-inasemekana sheria hii imeshafanyiwa marekebisho lakini jeuri na madhara ya sheria hii ni makubwa na hasa baada ya kuwekwa vigezo kandamizi dhidi ya wanaume ambavyo wanadai vikifanyika ni ubakaji (kukonyeza demu, kumtomasa au mfadhaiko). wanaume wengi wanatumikia vifungo vya maisha gerezani kutokana na sheria hii, wapo waliofanya hao wanastahili adhabu hiyo lkn wapo wale ambao sheria haikuwatendea haki, au mama kamtongoza kijana na kijana akasepa lkn mama kwa uwezo wake anasingia kumbaka au kashindwa kutoa rushwa kwa hakimu au wapo waliofungwa kwa kukosa fedha za kumlipa wakili mahakamani sasa wanasota magereza. WanaJF, kwa sasa magerezani kuna tabaka la wafungwa ambao kamwe hawawezi kuachiliwa au kutoka gerezani kwa namna yoyote ile hawa ni wakufia huko hususani wenye vifungo vya maisha,miaka 120, 90, 45, 30 na wakati wa kufungwa walikuwa na umri wa miaka 30, 40, 50. kundi hili haligushwi na msamaha wa Rais, hawawezi kutoka kupitia utaratibu wa parole wala wa community service, they are there to stay forever. Hali ni hivyo hivyo kwa sheria ya armed robbery, kwamba kweli wapo waliofanya lkn wapo wengi ambao hawakufanya lakini wanasota magerezani. Wanajamvi na lileta kwenu suala hili mliangalie kila mtu kwa utalaam wake, uzoefu tuchangie ili tuache jazba kwa wale ambao wanadhani maada hii haiwatendii haki. Karibuni.
 
Hali yako?
Nikianza na Sheria za Ndoa, mwanamke atapata mgao sawa endapo mlichuma mali mkiwa ndani ya ndoa hata kama hakufanya kazi ZA KIUCHUMI au alipika chapati kwasababu support yake ndio iliyokufanya wewe kupata hizo mali. Nguvu zake alizotumia kukusupport ndio mtaji wake. Upo?
Sheria za ubakaji SOSPA, zipo kwaajili ya kumlinda mwanamke.Kukonyeza, kutomasa and whatever it is, kwa mwanamke mwenye consent yake huna kec. But ukafanya hayo kwa mwanamke asiye na consent or msichana, my darling, iyo ni sawa na kumshushia mwanamke hadhi yake au kwa lugha nyingine umemyanyasa kimaadili YOU ARE LIABLE.
La mwisho ni kuwa put it in ur mind kuwa sheria haipo kwaajili ya kutetea wanawake/wasichana au rushwa bali ipo kwaajili ya kulinda haki ya wote. Wewe na Yeye. Ukijihisi umeonewa, kuna njia za kuprov innocence yako.
NB:Mwanamke ni female under 18
 
For more clarification find the case of bi hawa mohamed v.ally seif,hii case imeelezea kwa makin haki ya mwanaume na mwanamke ktk maswala ya talaka
 
Back
Top Bottom