Zijue sifa zinazomuwezesha mjasiriamali kupata mafanikio

Zijue sifa zinazomuwezesha mjasiriamali kupata mafanikio

Kibenje KK

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Posts
270
Reaction score
391
Najua una shauku ya kuwa MJASIRIAMALI mwenye mafakio. Lakini je, unazo sifa za kukuwezesha kufanikiwa kama MJASIRIAMALI?

Baadhi ya sifa zinazo mwezesha MJASIRIAMALI kupata mafanikio ni kama zifuatazo:-

1: Mawazo ya kiubunifu (Creative Thinking). MJASIRIAMALI huwaza kiubunifu ni jinsi gani ataiboresha bidhaa au huduma yake ili iwe bora zaidi.

2: Kutafuta maarifa pasipo kukoma(Knowledge seeking). MJASIRIAMALI hutafuta maarifa pasi na kikomo. Hujifunza kutokana na mafanikio au makosa. Haishi kujifunza vitu vitakavyoboresha biashara yake. Hupitwi na taarifa za muhimu, na anakwenda na wakati.

3: Uvumilivu na kutokukata tamaa(Perseverance). Ujasiriamali huhitaji Uvumilivu ili kufaidi matunda baadaye. MJASIRIAMALI hatakiwi kukata tamaa haraka.

4: Kutarajia changamoto na kujiandaa kuzikabili(Initiative). MJASIRIAMALI lazima atambue kuwa atakumbana na changamoto na ajiandae kuzikabili mbele ya safari.

5: Kutambua uwezo alionao na kujiamini(Self- confidence). MJASIRIAMALI lazima ajiamini yeye mwenyewe kulingana na uwezo wake vinginevyo hakuna mtu mwingine atakayemwamini.

6: Kufanya mambo hatarishi(Risk taker). MJASIRIAMALI ili kupata faida kubwa kila wakati atajikuta akilazimika kujiweka katika mazingira hatarishi.Kuhatarisha mtaji au fedha ndiyo maisha ya kila siku ya MJASIRIAMALI.

7: Kutengeneza mtandao (Relationship builder). MJASIRIAMALI atalazimika kutengeneza 'connection' na watu mbalimbali wa muhimu katika uendeshaji wa biashara yake.

8: Uaminifu (Commitment to others). MJASIRIAMALI lazima ajenge uaminifu na kutimiza ahadi kwa wateja, mawakala, wasambazaji na umma kwa ujumla. Atoe kile anachokiahidi na kwa ubora wa kiwango kinachotakiwa.

#begood #kelvinkibenje
 
Jiamini, uwe kinyume na mawazo ya watu na usijaribu kufit kwenye mawazo ya watu, uwe na maono na biashara yako.
 
Jiamini, uwe kinyume na mawazo ya watu na usijaribu kufit kwenye mawazo ya watu, uwe na maono na biashara yako.
Mkuu, Hupaswi kuwa kinyume ila unapaswa kuamini kwanza mawazo yako. Biashara ni watu, na biashara sio kwa ajili yako ni kwa ajili ya watu. Watu ndio wanakuajiri hivyo ni lazima uwasikilize ujue nini wanataka na ukiwapa ndio unapata pesa.
 
Back
Top Bottom