Zijue tabia za Kanisani

Zijue tabia za Kanisani

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Kwa akina dada vaa nguo yenye kusitiri mwili wako, ficha matiti yako na usionyeshe mapaja na matako yako ukiwa kanisani - haswa ikiwa umeketi mbele au unaongoza nyimbo za sifa na ibada. Kwa nini umkengeushe nabii na waabudu wengine?

Ukiwa kanisani, zima simu yako. Epuka kutafuna big G. Na usitupe takataka kanisani.

Ukiwa na changamoto ya kusikia usingizi wakati wa ibada, kaa safu ya katikati nyuma kabisa. Unaweza pia kupiga miayo huko.

Acha kuwatazama watu wanapoomba na kusifu - wewe pia umeenda kanisani kuabudu na kusifu hivyo sifu na uombe kama wao.

Acha kuchezea kurasa za biblia hovyo hovyo maana kufanya hivyo ni kukosa adabu - unaweza kufanya hivyo kibinafsi ukiwa nyumbani kwako.

Tafadhali jali watoto wanaolia. Usiondoke kabla ibada haijamaliza, isipokuwa kama utapata dharura.

Kama lilivyo shirika lingine lolote, kanisa pia lina bili - usiende kanisani mikono mtupu nenda na sadaka.

Ikiwa hujui kuimba ama huwa unaimba off-tune kama mimi, tafadhali punguza sauti yako[emoji1787]

Wengine wakimaliza kuomba tafadhali nyamaza. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko (1Kor 14:33).

Kwa wanandoa, peaneni mabusu mkiwa nyumbani au kwenye gari na sio ibadani.

Nakutakia ibada njema.

Ubarikiwe.
 
Una maanisha nini?

Ikiwa hapo ulipo upo kanisani unachezea simu kwanini? Utovu wa nidhamu huo. Angalia imani yako isije kukuponza na kushindwa kukuokoa.

Unapozungumzia maadili jitambue hatua zako kwanza; Je, unaenenda sawa na mafundisho ya Imani na kutii njia za kiroho ili uwe mtakatifu mbele ya muumba na sio kwa jamaa wanaokufahamu kwenye jamii yako inayokuzunguka!
 
Mtoa mada unaonekana una matatizo na GBV,mbona umechambua mavazi ya wanawake tu wawapo kwenye nyumba za ibada, je nini dress code ya wanaume kwenye hizi nyumba takatifu?
 
Back
Top Bottom