Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Habari yenu Tanesco,Natokea wilaya ya Mwanga,kijiji cha Kilaweni,Nilifanyiwa sarvey nikaambiwa gharama yangu ni laki tatu na Therathini na saba,Wakati hapo nguzo haiko mbali na kwangu ila sababu niliyopewa nikuwa waya utapita juu ya paa la nyumba ya mtu,Sasa pale nilipo sio mbali na kijiji kimoja ambacho kuna mradi wa Rea,Swali langu ni kuwa kama kule kijijini gharama ya laki tatu ni nyingi sana jamani,Naombeni ushauri wenu
 
Naomba namba za meneja wa REA
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.

5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
 
Ngoja ni-subscribe huu uzi kwa rejea kwani una miongozo mizuri kuhusu namna bora ya kupatiwa Huduma ya Umeme.
 
Je agizo la Waziri wa nishati Dr Kalemani la kuitaka TANESCO isiuzie wateja nguzo linatekelezeka au ilikuwa siasa tu?

Nina nyumba ipo umbali wa kama nguzo 4 hivi roughly.

How much will it cost?
 
Je agizo la Waziri wa nishati Dr Kalemani la kuitaka TANESCO isiuzie wateja nguzo linatekelezeka au ilikuwa siasa tu?

Nina nyumba ipo umbali wa kama nguzo 4 hivi roughly.

How much will it cost me?
Hilli ni tatizo, Morogoro bado nguzo zinauzwa sasa sijui tufate yepi! Yaani Waziri Mkuu kasisitiza sana na kweli tunawapongeza lakini watendaji wanatutolea bili za ajabu sana. Nawaomba viongozi wetu watembelee TANESCO Morogoro
 
Dah tanesco noma siku za kazi 60
Screenshot_20200114-182218.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Songea nina mwez wa 3 tangu nijaze fomu mpaka Leo hawajafika Ku survey kila nikienda wanasema wanakuja lakin hakuna kitu.nyumba ipo hapa hapa mjin block TT plot 274 mkuzo luwawasi.fomu imejazwa jina Hussein Asedi Mgao.no ya sim 0624 999 816.wenyewe wanasema ndani ya wiki watakuwa wamemhudumia mteja.lakin in uongo mtupu kila nikienda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kiasi gani kwa mita mypya kwenye nyumba yenye...umeme inayo hitaji umeme wa nyongeza ya mita…?
 
Nimefuata taratibu zote, ila nimekwama kupata control number , waliniambia eneo langu lina mita 89 niandike barua ipitie kwa mtendaji kama nitakuwa tayari kujilipia mwenyewe . Kwakuwa nilikuwa nahitaji huduma kwa haraka zaidi lakini sasa inakata wiki ya pili sijasikia chochote kutoka kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu je inaruhusiwa kkama unanyumba mbili moja kubwa na nyingine umejenga pembeni unaruhusiwa kuunganisha waya kutoka kwenye nyumba kubwa kuja kwenye nyiumba ndogo ukatumia mita moja tu?
 
Sera ya TANESCO ni kufunga mita moja ya umeme kwa kila nyumba/jengo.
Imezoeleka kuona uunganishaji wa nyaya za umeme kutoka nyumba, hasa kubwa, kwenda majengo ya jirani.
Huu utaratibu si mzuri kwa minajiri ya usalama dhidi ya matukio ya ajali za moto na udhibiti ufuatiliaji wa mitandao ya nyanya ya zilizotandikwa kwenye majengo husika.
 
Hayo makadirio ya muda yamewekwa ili kuonyesha kuwa Tanesco wako efficient, hali halisi nitofauti kabisa. Tangu kukamilisha fomu hadi surveyor kuja kupima inawweza kuchukua miezi sita maana wako wachache na hawana vyombo vya usafiri.
Laiti mishahara ya wafanyakazi wa tanesco ingekuwa unatokana na mauzo ya umeme, nadhani efficiency ingekuwepo, lakini sasa, wauze umeme wasiuze mishahara yao wanakosa?
 
Nyumba ya kupanga tunahitaji mita nyingne ili ziwe mbili. Je taratibu gani zifuatwe mpaka kupata mita nyingne?
 
Naomba usikimbie. Tujibu baadhi ya maswali japo machache:

1. Ni meter angapi maximum mtu atahitaji nguzo? (Yaani nguzo iliyopo hadi kufika ktk nyumba). Naomba maelezo hapa, kwani hapa ndio mafundi wa TANESCO hutupigia hela. mf ni 30m -70m au 30m to 100m? au 30-70m ni kile chuma tu bila nguzo kati ya 30m -100m?
2. Je ni sahihi ktk mfumo wa leo mtu kufunga/kuweka Cut-Out ktk meter kabla ya umeme kuingia ndani? (Japo ndani kutafungwa Circuit Breaker)
3. Naskia sijui Two Phases au Single Phase. Je ni mfumo upi ni mzr kwa matumizi ya nyumba ya makazi?

Note: Umesema Jedwali, lipo wapi sasa?
Tanesco
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.

5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
Separate meter maana yake ni Luku nyingine au ni kale kamashine kanakohesabu unit? Na je gharama za kuwa na separate meter ni kiasi gani? Nikihitaji Luku meter nyingine ili wapangaji wawe na luku yao na Mimi niwe na yangu natakiwa nifanyeje na malipo ni kiasi gani?
 
Ndugu TANESCO nimelipia umeme Nguzo2 urefu Mita100
kuanzia mwaka jana tareh19/10/2016 mpka Leo tarehe 24/04/2017 sijaunganishiwa umeme nimekuwa mtu wakuzungushwa kila nikienda Tanesco nazungushwa nimechoka.
Niliambiwa ndani ya siku60
TANESCO kwanini mteja wenu lazima alipie nguzo wakati waziri kasema ni bure? Mnashindwa nini kusoheza huduma kwa mteja atakayelipia maisha yote kuunganisha na umeme? Kwani atalipia umeme mpaka na watakuu? Botswana hakuna mteja Kulipia nguzo lakini Tanzania ni lazima.
Kwa mfano mobisol sola wats 200 unipia kiwango cha kuanzia 180 halafu unanalipia 117 kila mwezi kwa miaka 2,baada ya hapo hutozwi tena mpaka watukuu, na unatumia feni,Firiji ,TV na pasi unalipa kwa miezi 24 kidogo kidogo baadaye hulipi kabisa, mnaonaje na ninyi wateja wenu wawe wanalia kidogo mpaka wamalize deni lenu ? Kwasababu watalipa pesa tanesco milele pesa.mimi ni Donald Machombo toka Urambo.namba yangu 0623644349,wapeni services line wateja wenu ili mkusanye pesa milele.mwwisho watu wanachagua mobisol kwani wakilamiza deni hawalipi Bill milele.
 
Hamna taratibu zozote nyinyi ni jipu..UBENANI(Vikindu)..mwaka huu nguzo tano kutuletea ili baadhi ya nyumba ziwake umeme hamtaki kweli Mwenye nyumba kafa tambeni tu
 
Back
Top Bottom