Depretty
JF-Expert Member
- Jun 14, 2013
- 248
- 99
Habari
Hivi taratibu za ndoa za bomani zikoje?
Je, faida au hasara za kufunga ndoa bomani ni zipi?
Maswali zaidi:
Majibu:
====
Mara nyingi tunapoongelea suala la ndoa huwa tunarejea ndoa za aina tatu. Kwanza huwa tunaongelea ndoa za kidini, pili ndoa za kimila na tatu ndoa za kiserikali. Kila moja katika ndoa hizi inazo taratibu zake ambazo hutofautiana na nyingine. Ndoa za kidini na za kimila mara nyingi taratibu zake hujulikana kwa wengi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ndoa hizo hufungwa kwa wingi na hivyo taratibu zake ziko wazi kwakuwa hushuhudiwa mara kwa mara. Ndoa za kiserikali ( civil marriage) mara nyingi taratibu zake huwa hazijulikani sana. Hii ni kutokana na uchache wa ndoa hizi katika jamii zetu. Yumkini kuna umuhimu wa kuzijua kwakuwa waweza kuwa mhitaji wa kufunga ndoa ya aina hiyo.
1.MAHITAJI YA KUFUNGA NDOA YA KISERIKALI.
Mara zote ndoa ni hiari. Na hiari ya ndoa hutokana na mapemzi ya wahusika wawili. Wakati mwingine hutokea mapenzi yapo na uhiari upo lakini mazingira ya namna fulani hasa ya kimila au kidini yanazuia kabisa ndoa kufungwa japo wahusika wanahitaji ndoa. Hapa ndipo mahitaji ya kufunga ndoa kwa mkuu wa wilaya yanapokuja. Yumkini ndoa hii inapofungwa hadhi yake huwa sawa na ndoa nyingine zote na wahusika hustahili haki zote za msingi zinazotokana na ndoa.
2. SABABU ZINAZOWEZA KUKUFANYA UFUNGE NDOA KWA MKUU WA WILAYA.
( a ) Utofauti wa dini. Hii ni sababu kubwa inayoweza kupelekea wahusika kufunga ndoa kwa mkuu wa wilaya. Kifungu cha 25 cha Sheria ya Ndoa kinasema kuwa ndoa hutambulika kuwa ni ya kidini inapokuwa imefungwa kwa taratibu za dini husika. Hata hivyo karibia taratibu za kila dini huruhusu ndoa kwa sharti kuwa wahusika wote lazima wawe waumini wa dini moja. Kutokana na hilo huwa si rahisi kwa watu wa dini tofauti kufunga ndoa kutokana na sharti hilo. Lakini ndoa ya kwa mkuu wa wilaya jambo hilo halipo kwani watu wa dini tofauti wanaweza kufunga ndoa.
( b) Ndoa inayofungwa kwa mkuu wa wilaya hutoa uhuru kwa wahusika kueleza aina ya ndoa wanayoitaka ikiwa iwe ndoa ya mke mmoja au wake wawili. Ikiwa watasema wanataka ya mke mmoja basi mwanaume hatoruhusiwa kuongeza mke mbeleni na ikiwa watasema wanataka ya mke zaidi ya mmoja basi mwanaume anaweza kuongeza mke mwingine mbeleni akiamua kufanya hivyo. Ndoa za kidini na kimila hazina uhuru huu kwani taratibu zake tayari zimepangwa na hazibadiliki.
3. TARATIBU ZA NDOA KWA MKUU WA WILAYA.
( a ) Kwanza wahusika watatakiwa kutoa taarifa ya maandishi ndani ya siku 21 kabla ya siku ya ndoa ikieleza majina yao, ya wazazi wao, nia yao ya kutaka kufunga ndoa, umri wao , hadhi yao ya kindoa kama kuna mtu ana ndoa nyingine au mjane au mseja. Pia katika notisi hiyo lazima ielezwe iwapo wahusika hawana uhusiano wowote wa kiundugu uliozuiwa kwa mfano wasiwe kaka na dada, mtu na shangazi yake au mjomba wake,mtu na baba yake au mama yake n.k.
( b ) Ni jukumu la ofisi inayotarajia kufungisha ndoa hiyo kutangaza notisi hiyo ili ikiwa kuna mtu mwenye pingamizi juu ya ndoa hiyo ajitokeze na kuwasilisha pingamizi lake. Ikiwa kuna pingamizi lolote basi bodi ya usuluhishi wa ndoa ( Marriage Reconciliation Board) au mahakama ndiyo itakayoamua pingamizi hilo.
( c ) Ikiwa hamna pingamizi lolote baada ya siku 21 ndoa itafungwa na maneno yafutayo yatasemwa. Mwanaume atasema “Mimi Fulani ninamchukua fulani kama mke wangu”. Na mwanamke naye atasema “Mimi fulani ninakuchukua fulani kama mme wangu”. Ndoa itakuwa imekamilika na wahusika baada ya kusaini nyaraka za ndoa wataruhusiwa kuendelea na taratibu zao nyingine.
( d ) Kama ilivyo ndoa zote mashahidi huwa ni suala la msingi sana. Sheria imelazimisha wawepo mashahidi wasiopungua wawili katika ndoa hii ambao umri wao ni kuanzia miaka 18 na kuendelea. Pia wakati ndoa inafungwa haitakiwi kuwa siri. Sheria imesema kuwa watu waruhusiwe kuwapo na kushuhudia kadri eneo inakofungiwa litakavyokuwa linaruhusu.
Hii ndio ndoa ya serikali ( civil marriage) ambayo hujulikana kama ndoa ya kwa mkuu wa wilaya.

Utaratibu wa kufunga ndoa yenu bomani mnatakiwa muwe na barua ya serikali ya mtaa kwaajili ya kuwatambulisha mnapotoka.
Pia mnatakiwa mlipie ada ya kufungishwa ndoa ya shilingi 50,000/-.
Baada ya kuandikisha, mtasubiria itangazwe kwa muda wa siku 21, na baada ya hapo mtafungishwa ndoa.
Na bomani ndoa inafungwa siku ya jumatatu mpaka ijumaa, mkitaka kufungishwa ndoa siku ya jumamosi au jumapili basi mtalipia shilingi 150,000/-.
Na pia mkitaka kufungishwa ndoa nje na ofisi za serikali yaani pale bomani inawezekana ila mtalipia shilingi 300,000/- , na hayo malipo ni mbali na ile ada ya shilingi 50,000/-.
Kwa kufanya hivyo ndoa yako itakuwa imekamilika na kutambuliwa na jamii na mbinguni pia sasa na neno kwenye kitabu cha Rum 13:1-2 imeandikwa, kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu , kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU, na ile iliyopo imeamliwa na MUNGU.
Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU, nao washindanao watajipatia hukumu.
Maswali zaidi:
Naomba kupata majibu yafuatayo:
1. Hii ndoa inawasimamizi?
2. Barua ya utambulisho ina addresiwa kwa nani?
Majibu:
Ndio ina mashahidi/wasimamizi
Barua unaiadress ofisi ya mkuu wa wilaya husika.