Zijuwe dalili za kabla ya kuachwa.

Zijuwe dalili za kabla ya kuachwa.

Dalili ya mvua ni mawingu ingawaje baadhi ya wakati inaweza kunyesha bila ya hata kuonekana mawingu ya kuridhisha kama dalili yake. Na ni kama hivyo, kabla ya kuachwa huwa zipo dalili tofauti ambazo wengi wetu kwa kuona ni vitu vya kawaida, huwa hatuchukuwi tahadhari za mapema.
Baadhi ya dalili hizo ni hizi zifuatazo ila na wewe ongezea nyengine kwa kujuzana zaidi.

1. Mwenza kukosa raha mnapokuwa pamoja.
2. Kutopenda kutembelewa ikiwa mnakaa sehemu tofauti au kukutaka utowe taarifa kabla ya kumtembelea.
3. Kutoipa umuhimu mitoko yenu ya week end au mengineyo kama ilivyokuwa awali.
4. Kuanzisha majibu ya mkato.
5. Kukujibu kwa kujiamini zaidi.
6. Kutozijibu text zako kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali.
7. Kupenda kuzima simu kwa muda mrefu bila ya sababu za msingi na kutoyajali mawasiliano.
8. Kwenda pembeni kupokea call iliyoingia au kwenda kujibu text.
9. Kuchukizwa na kuishika simu yake.
10. Kutojiamini mnapokuwa pamoja.
Hivyo zinapojitokeza ishara kama hizo ni vyema kuuimarisha upya uhusiano wako kabla hayajakukuta.
asante kwa hizo dalili 10. mi ntamnyang'anya cmu ili zibaki dalili 6 (i.e 6,7,8 na 9 niczipate)ili nimwache mapema kabla ya yeye kuniacha
 
Sio wote ndugu yangu,Mimi siku nilipoachwa na Mume wangu wala sikutegema kwanza nilikuwa nimefunga sunna siku ya Jumatatu Mume karudi na cake ya Love kanikuta najiaandaa kuswali nimemaliza naanza kufturu napewa cake yangu nikajua mapenzi motomoto baadae anamuita shehe aliyetufungusha nikajua pengine ni maongezi yao ya kawaida sikutilia maanani,after ten mnts naitwa sikushutka nilijua pengine Mumewangu alikuwa na shida nakaa nimsikilize alichoniitia namsikia anamwabia yule shekhe nimekuita nataka uwe shahidi nampa mke wangu talaka, iliandikwa mbele yetu kwanza nilihisi koo limeishiwa mate,Nikamuuliza kulikoni ama kuna kitu nimekukwaza anasema hakuna yule ustaadhi anamuuliza talaka iandikwe na sababu ya kumuacha anasema hakuna sababu,Basi nilichukuwa karatasi yangu nikajikalia eda yangu ilipoisha nikamtimka kwetu.SIKUONA DALILI YA WINGU WALA MANYUNYU

Pole dear, Mungu atakupa mbadala mwema. mie naona naelekea huko maana vituko dah mtihani!
 
Asante kutujuza dalili10 muhimu,nimeguzwa na no2,8,9.mi aliniambia kazi nyingi,boss mkali,naongea na boss n.k.hakika nilimpenda na kumuamini,live bila chenga nikaachwa Mbele ya mdada mwingine tena kwangu,the worse thing yule dada akatembea na rafiki wa Ex wang ofic 1 na kumdamp ex,AlaMa za NYaKati ni MuHimu,hakika nimekumbuka mbali! Thanx anyway.
 
Mimi nilijulia wp ndg yangu ndio kwanza ilikuwa ndoa yangu ya kwanza na kwakweli sikuwa hata na hamu ya kusema eti Mali ama kitu kingine kwa kipindi kile nilikuwa namuhitaji Muumba wangu zaidi kuliko kitu chochote,nikikukmbuka nilivyokuwa najinyima na kumzuia Mume wangu tusifanye starehe ili tumalize ujenzi wa nyumba tuliyokuwa tunajenga,ndoo za mchanga nilizokuwa nabeba madirisha niliyokuwa nafata mkata kwa ajili ya kupata unafuu wa ujenzi leo nyumba imesimama na kila kitu kimekamilika ndani namalizia nje kwenye garden na bustani za mboga2 UNANIPA TALAKA?Jamani inauma yasikie tu kwa mtu anahadithia dunia yote niliyoona imenigeuka na kuwa shubiri kwangu,nilikuwa kila nikisikia wimbo wa Vumilia kwangu ilikuwa ni kilio,UTANIKUMBA KWA MEMA NILIYOKUFANYIA JAPO HUTAMBUI UMUHIMU WANGU,bora mtu akwambie kosa umuombe msamaha ujirekebishe kama kuna mahali umemkwaza kama binaadamu,lakini hili pigo langu mmmh.Nashukuru Mungu alinipa moyo wa subira na imani nikiamini yote ni maandiko yamepita sasa
 
Back
Top Bottom