Sio wote ndugu yangu,Mimi siku nilipoachwa na Mume wangu wala sikutegema kwanza nilikuwa nimefunga sunna siku ya Jumatatu Mume karudi na cake ya Love kanikuta najiaandaa kuswali nimemaliza naanza kufturu napewa cake yangu nikajua mapenzi motomoto baadae anamuita shehe aliyetufungusha nikajua pengine ni maongezi yao ya kawaida sikutilia maanani,after ten mnts naitwa sikushutka nilijua pengine Mumewangu alikuwa na shida nakaa nimsikilize alichoniitia namsikia anamwabia yule shekhe nimekuita nataka uwe shahidi nampa mke wangu talaka, iliandikwa mbele yetu kwanza nilihisi koo limeishiwa mate,Nikamuuliza kulikoni ama kuna kitu nimekukwaza anasema hakuna yule ustaadhi anamuuliza talaka iandikwe na sababu ya kumuacha anasema hakuna sababu,Basi nilichukuwa karatasi yangu nikajikalia eda yangu ilipoisha nikamtimka kwetu.SIKUONA DALILI YA WINGU WALA MANYUNYU