#COVID19 Zikijibiwa hizi hoja, naenda kuchanjwa!

#COVID19 Zikijibiwa hizi hoja, naenda kuchanjwa!

Hata wao chanjo hawana imani nayo! Cheki [emoji117]View attachment 1875067
  1. Sijaona dawa ikivutwa kutoka kwenye chupa
  2. Mchomaji ameshika kwenye sindano yenyewe
  3. Mchomwaji hajaonesha kuhisi maumivu
  4. Kisukumio cha dawa kipo chini ikiashiria syringe haina ujazo stahili wa dawa
  5. Ushikaji wa sindano na usukumaji wa dawa una mashaka
 
Kama chanjo ni hiyari kwanini inatumika nguvu kubwa kuwaswaga watu wapatiwe chanjo........

Katika uhuru wa kutoa maoni kwenye chanjo kwanini uhuru unaotakiwa ni wa kukubali chanjo lakini wa kupingana na chanjo unaonekana sio uhuru bali ni uchonganishi.......??

Kwanini serikali ikatae kuwajibika kwa chanjo inayoinadi kuwa ni salama kwa asilimia zaidi ya 99....??

Nikishachanjwa nitapatwa na nini kuzito ambacho serikali kama mlezi wa raia hataki kuwajibika nacho......??

Mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake

Nawakaribisha wote hasahasa wanaopigia debe chanjo wakiongozwa na Mshana Jr

Asante sana KikulachoChako kwa hoja hizi.
Hatuna muda huo wa kukuelimisha, endelea kukata, wenzako majaji tunachanja jumatatu, tena tunapelekwa Zanzibar kuchanja ya mrusi
 
Tatizo mnakaririshwa mambo, kwa hiyo kwa akili yako, unadhani madaktari bigwa na wasomi wakubwa kupinga chanjo unadhani wamechanganyikiwa eeh?

Ni chanjo ipi umewahi kuchomwa, ukaambiwa usaini likitokea la kutokea serikali haihusiki?

Dunia nzima chanjo inapigwa...we unadhani una akili kuzidi hao wote wanaopinga?
Daktari gani huyo ,anafanyia kazi wapi?
Au unasikiliza porojo za gwajiboy?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
We wala usichanjwe kaa tu.

1. Matumizi ya condom na net ni hiyari sio lazima lakini umewahi kuhoji nguvu kubwa inatotumika kutaka watu watumie? Unajua ni mamilioni mangapi ya shilingi yanatumika kujenga uelewa wa watu kutumia condom? Unadhani kwanini kama sio kutaka kulinda watu wagumu kama wewe

2. Umewahi kuwa na ndugu yako wa karibu anaingia kufanyiwa upasuaji hospitali ukatakiwa kusaini form ya kujitwisha mzigo na si hospitali, Dokta wala serekali? Kwanini unashangaa kwenye chanjo ya korona.
Hili ndilo Jibu sahihi la hoja yake... Umenishawishi hata mimi
 
ninavyofahamu na kama una swali niulize nitakujibu kadri ninavyofahamu,

Kwanini Chanjo ya COVID 19 inapigiwa chapuo sana Licha ya kwamba ni hiyari?

- Hii ni kwasababu dunia nzima ipo katika mpango na juhudi za kutokomeza kabisa ugonjwa huu, ndio maana chanjo inasisitizwa sana kwasababu bila watu wote kuchomwa chanjo itakua ni ngumu sana ugonjwa huu kuisha,


Kwanini wanaochoma chanjo wanaendelea kuvaa barakoa? Je nikipata chanjo naweza kuambukizwa na kuambukiza?


- Wanaopata chanjo wanashauriwa kuvaa barakoa kwani wanauwezekano pia wa kupata maambukizi ya korona, iko hivi,
Chanjo Ya korona inapoingia mwilini mwako inaboost immunity, yaani inauongezea kinga mwili wako, kinga hii inayoongezwa inauwezo mkubwa wa kupambana na UVIKO, maana yake wewe uliepata chanjo tayari utakua na kinga utakapopata maambukizi ya UVIKO mwili wako utaweza kupambana na virusi hivyo na hatimaye kutoweka maana tayari una kinga ya kujilinda,



Kwanini baaadhi ya chanjo inatakiwa uchomwe zaidi ya mara moja?

Ni kawaida sana baadhi ya chanjo kuchomwa zaidi ya mara moja ili kuimarisha zaidi kinga mwili, mfano kuna chanjo za Tetanus Taxoid (chanjo ya tetenasi) hii huchomwa mara tatu kwa mwanaume na mara tano kwa wanawake pia zipo chanjo nyingine za watoto ambazo huchomwa zaidi ya mara moja,
pia katika chanjo za korona zipo baadhi ambazo unachomwa zaidi ya mara moja na nyingine ni mara moja tu kama Johnson Johnson




Kwanini baadhi ya mataifa ya magharibi licha ya chanjo ila uginjwa bado upo na watu wanakufa kwa covid?

Ni kwel hata baadhi ya mataifa ambayo chanjo imetengenezwa huko bado wanaugonjwa na watu wanakufa lakini kiuhalisia sio kwa idadi ile kama ya mwanzo,
mfano mzuri anagalia China ambako ugonjwa umeanzia, kule sasahivi wanaelekea kusahau mambo ya Corona kwasababu zaidi ya 90% wamepata chanjo,
Angalia ulaya sasahivi hata watu wameanza kufunguliwa angalia michuano ya Euro watu waliruhusiwa kuingia uwanjani na ugonjwa ulienea lakini sasahivi upo very week kwasababu watu wameshapata chanjo,

Angalia nchi ya Italy kipindi cha COVID walikufa sana kwa siku walikua wanakufa zaidi ya watu elfu 6, lakini kwa sasa idadi ya vifo haipo kwasababu wengi wameishapata chanjo hivyo virusi vya korona vimedhoofishwa sana havina nguvu tena,




Kwanini Chanjo ya COVID imechukua mda mfupi sana? je tutaaminije kama haitaleta madhara baadaye?

hakuna muda malumu uliowekwa wa chanjo kutengenezwa, hata hiyo chanjo ya kifua kikuu ambayo wewe umezaliwa ukaikuta, pia kipindi inatengenezwa wapo watu waliokua wa kwanza kuitumia na haijawadhuru,
rejea ugonjwa wa Ebora ulilipika Congo, Siera lion, na equatorial Guinea, ugonjwa ule ulilipuka ghafla na utengenezaji wa chanjo yake haukuchukua muda mrwfu na chanjo ilionyesha ufanisi mkubwa mpaka leo hii ebora imebaki kuwa historia,




Je chanjo ya Covin ndiyo Alam ya 666?

hayo mambo yamekaa kiimani zaidi na sio kisayansi na kusema kwamba chanjo ni chapa ya 666 ni sababu zisizo na mashiko kwani hata kwenye maandishi chapa ya mnyama hadi itokee tayari dunia itakua imeshapitia kipindi cha kuabudu siku moja na kuwa na serikali moja pia chapa ya mnyama itakua inahusisha moja kwa moja mpinga kristo,


Je, Wazungungu wanataka kutuua kupitia chanjo?

wakuue kwa lipi, wangetaka kukuua wasinheruhusu nchi mbalimbali zitengeneze chanjo chanjo ingekua ni moja dunia nzima, lakini mpaka sasa nchi nyingi zimetengeneza chanjo ikiwemo Africa kusini china na india kama mpango ungekua ni kuuwa watu basi ingetumika chanjo moja dunia nzima,

lakini vilevile ieleweke kwamba Mzungu akiamua kukuua, hauna ujanja wa kukwepa



Kwanini kwenye fomu ya chanjo, serikali ilijitoabkuwajibika kwa lolote litakalotokea?

- chanjo kazi yake ni kuboost immunity ili mwili wako uwe na uwezo wa kupambana na Covid pale unapoipata,

sasa basi kipaumbele cha kwanza ni wenye magonjwa sugu, na wenye magonjwa sugu wengi immunity zao ziko chini sana so serikali ikisema iwalipe

ikitokea mtu yytr amepiga chanjo na akafa hata kwa ugonjwa mwingine watadai fidia,

means mimi niwe na Chronic heart diseases nikaamua kuchoma chanjo, mwezi mmoja ukipita nikafa kwa ugonjwa wa moyo au mwingine wwte ule lazima ndugu waidai serikali fidia,

sasa serikali italipa wangapi?

maana hapa ingesema ihusike watu wangeenda kuiangushia serikali jumba bovu, mtu anakufa kwa TB ila kwakua alipiga vaccine ya covvid atataka alipwe
sasa kama ni chanjo na unaamini inaweza ikapambana na maambukizi ya corana sasa kwanini niendelee na BARAKOA ??!!

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Wazee wetu wameishi na kufia kwenye maeneo au vijiji vyao na wameishi kwa furaha hadi wengine wakavuka miaka 100 na hadi leo hii kuna watu hadi wanazeeka hawajawahi kukanyaga Dar, kuna wazungu hadi wanazeeka hawajawahi kuvuka mipaka ya nchi zao na wengi wanasimuliwa au kuona kwenye luninga maisha ya huku afrika...........kwa hiyo sioni jipya.
... dunia imebadilika ndugu! Wazee wako walikua wana-post Jamii Forum? Leo hii kwenda hapo Dubai, Guangzhou, Comoro, SA, nchi jirani (madereva), n.k. kutafuta maisha au kibiashara ni jambo la kawaida mno kwa yeyote yule! Hiyo simu unayotumia au nguo ulizovaa kuna mtu amezifuata nje ya mipaka! Kuna safari za kidini (hijja), kuna safari za kimatibabu, n.k.
 
Hii kitu ya kusainishana imenistua Sana[emoji848]
IMG_20210729_134938.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa kama ni chanjo na unaamini inaweza ikapambana na maambukizi ya corana sasa kwanini niendelee na BARAKOA ??!!

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
sasa kama ni chanjo na unaamini inaweza ikapambana na maambukizi ya corana sasa kwanini niendelee na BARAKOA ??!!

Kazi kubwa ya chanjo sio kuzuia maambukizi Bali
Inashirikiana na Kinga zako za mwili kupambanaa na maambukizi ya ugonjwa husika pindi uoatapo maambukizi
Pia kwa kipindi hiki ambacho Bado virus vinajibadili mara kwa mara Ni vizuri kuchukua tahadhari hata Kama umechanjwa
 
Kazi kubwa ya chanjo sio kuzuia maambukizi Bali
Inashirikiana na Kinga zako za mwili kupambanaa na maambukizi ya ugonjwa husika pindi uoatapo maambukizi
Pia kwa kipindi hiki ambacho Bado virus vinajibadili mara kwa mara Ni vizuri kuchukua tahadhari hata Kama umechanjwa
 
Chanjo ni HIARI.

Kampeni inaendeshwa na wataalamu kueleza umuhimu mkubwa wa chanjo vs Covid-19 na side effects za chanjo - kwa faida ya wote.

Ni juu ya kila mtu kupima mwenyewe na kuchagua kama ilivyo habari ya mbinguni/peponi au jehanamu. Uchaguzi/uamuzi ni wako.

YOU MAKE THE CHOICE; YOU FACE THE CONSEQUENCES.

Hakuna haja ya kupigiana kelele.
 
Una faida gani kwa hili taifa hata usipochanjwa?
Na ndio sababu anauliza mbona inatumika nguvu kubwa kuinadi, hadi jeshi la polisi kuahidi kuwakamata watakao ipinga?
 
Kama chanjo ni hiyari kwanini inatumika nguvu kubwa kuwaswaga watu wapatiwe chanjo.

Katika uhuru wa kutoa maoni kwenye chanjo kwanini uhuru unaotakiwa ni wa kukubali chanjo lakini wa kupingana na chanjo unaonekana sio uhuru bali ni uchonganishi.?

Kwanini serikali ikatae kuwajibika kwa chanjo inayoinadi kuwa ni salama kwa asilimia zaidi ya 99?

Nikishachanjwa nitapatwa na nini kuzito ambacho serikali kama mlezi wa raia hataki kuwajibika nacho?

Mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake.

Nawakaribisha wote hasahasa wanaopigia debe chanjo wakiongozwa na Mshana Jr

Asante sana KikulachoChako kwa hoja hizi.
Nani akujibu? Unapotumia kondomu - kinga dhidi ya STDs na UKIMWI - huwa unahitaji kushawishiwa?
 
Hii issue ngumu Sana , kuna agenda ya Siri kwenye hzi mambo, anyway kila mmoja na akili yake kichwani!!! Badae wataifanya kuwa lazima Tu indirect
Ajenda Ni moja tu... Majaribio.
 
Kabla ya kuchanjwa unasainishwa form ambayo inasisitiza kuwa serikali haitawajibika na madhara yoyote yatakayotokea baada ya chanjo,form inanifanya niseme kuwa nitakuwa raia wa mwisho kuchanjwa katika dunia hii.
 
Back
Top Bottom