bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Leo imechezwa michezo kadhaa ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania ila macho na masikio ya wengi yalikua kule Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine mtanange Kati ya Wenyeji Tanzania Prison na Wageni wao Timu ya Simba
Mpaka mwamuzi wa kandanda lile anapuliza kipenga cha mwisho matokeo ni Tanzania Prison 2 na Simba 1 na hivyo Simba kuacha pointi zote 3 pale Mbeya
Pambano hilo limenogesha utamu wa ligi kuu hasa kwa timu mbili Hasimu/Watani wa jadi timu ya Yanga na Simba
Kwani Mpaka sasa Simba anaongoza ligi akiwa na pointi 35 akiwa amecheza michezo 15 na mtani wake Yanga akiwa wa pili na pointi zake 30 ila akiwa kacheza jumla ya michezo 14 hivyo akiwa na faida ya mchezo mmoja mkononi
Endapo timu ya Yanga itashinda mchezo wake wa kiporo itakua na jumla ya pointi 33 na kuwa na pengo la pointi 2.
Je Yanga atafanikiwa kushinda mchezo wake wa mwisho kabla ya mapumziko ya ligi kuanza na kupunguza pengo la pointi dhidi ya mpinzani wake?
Tusubiri.