Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
- Thread starter
-
- #61
:twitch:Mwambie wewe upo tayari kuhamia kwake na kuwa mume ***** kwake! Hivyo aachane na huyo anayetaka ahamie Mbagala na akukaribishe wewe Mwenge ili mwendeshe maisha yenu pamoja! Ila ukubali kuwa house-boy wake tu!!!!!!!!!!!!!!!!!:sick:
Mwita hebu nambie kwanza! UMEOA???!!!
mme wa huyu dada ana matatizo
kwani akikaa kwenye hiyo nyumba na akaendelea kulipa kodi ya nyumba yeye ni tatizo???
Na gari kwa nini iuzwe ???
Mambo mengine bwana ni hekima kidogo inahitajika
Wadau naomba mnisaidie kuchanga mawazo.
Zilipendwa wangu tuliyeachana miaka mitano iliyopita amenipigia simu anaomba ushauri.
Anasema mume wake amemtelekeza yeye na mtoto wake tangu alipokuwa na ujauzito wa miezi minne.Huyu shostito anafanya kazi kampuni moja ya simu na mumewe anafanya kazi serikalini.
Kisa cha mume kumkimbia ni kuwa mwanamke amekaidi kutekeleza matakwa yake. Mume anataka mkewe auze gari aliyonunua kabla hawajaoana na wahame toka kwenye nyumba wanayoishi mwenge iliyolipiwa na mke.Mume alihamia nyumbani kwa mkewe kabla hawajaoana, na mwanamke alinunua gari kabla hawajaoana, na jamaa hakuchangia hata senti moja.
Mwanamke kakataa kuuza gari ila amekubali kuhama nyumba kwa masharti kwamba iwe ni maeneo ya mwenge, sinza, kinondoni, ubungo ama mabibo. Mumewe anataka wahamie mbagala, kwamba ndipo anaweza kumudu kulipa kodi ya nyumba, hataki mkewe aongeze hata senti.Mume kuona mwanamke hatekelezi matakwa yake akaona isiwe tabu, kafunga virago amehamia mbagala.
Wadau mnisaidie, nimshaurije huyu shostito?
Wadau naomba mnisaidie kuchanga mawazo.
Zilipendwa wangu tuliyeachana miaka mitano iliyopita amenipigia simu anaomba ushauri.
Wakati mwingine sio lazima uwe na jibu la kumpa ndugu yangu, maana kuna ka mtego hapo! I hope you are a man enough to know what am saying!
Wadau naomba mnisaidie kuchanga mawazo.
Zilipendwa wangu tuliyeachana miaka mitano iliyopita amenipigia simu anaomba ushauri.
Anasema mume wake amemtelekeza yeye na mtoto wake tangu alipokuwa na ujauzito wa miezi minne.Huyu shostito anafanya kazi kampuni moja ya simu na mumewe anafanya kazi serikalini.
Kisa cha mume kumkimbia ni kuwa mwanamke amekaidi kutekeleza matakwa yake. Mume anataka mkewe auze gari aliyonunua kabla hawajaoana na wahame toka kwenye nyumba wanayoishi mwenge iliyolipiwa na mke.Mume alihamia nyumbani kwa mkewe kabla hawajaoana, na mwanamke alinunua gari kabla hawajaoana, na jamaa hakuchangia hata senti moja.
Mwanamke kakataa kuuza gari ila amekubali kuhama nyumba kwa masharti kwamba iwe ni maeneo ya mwenge, sinza, kinondoni, ubungo ama mabibo. Mumewe anataka wahamie mbagala, kwamba ndipo anaweza kumudu kulipa kodi ya nyumba, hataki mkewe aongeze hata senti.Mume kuona mwanamke hatekelezi matakwa yake akaona isiwe tabu, kafunga virago amehamia mbagala.
Wadau mnisaidie, nimshaurije huyu shostito?
Ushauri ni mwingi wa kutosha umepewa; Mimi naona hapo wamekutana fahari wawili na hawawezi kaa zizi moja, ili uhusiano udumu lazima mmoja ajaribu kujishusha na hapo upande wa pili kama una hekima utaongeza upendo zaidi, lakini kutunishiana misuri ni hatari.
Inaonekana huyo mwnaume alipohamia kwa mwanamke mambo yalikuwa shwali lakini baadaye mwanamke alikunjua makucha na kumbeza mwanaume.
Mwaka mzima umepita sipati picha nani hasa alipuuza hadi muda huo bila kutatua tatizo ndio wanashituka saa hizi, au wameshasuluhisha sehemu mbalimbali bado imeshindikana.
Lakini jamani Mbagala si bado ni DSM kwa nini asihamie tu! Kuna watu ndoa zao ni mikoa tofauti itakuwa hii ya mbagala.
Nilishawahi shiriki mgogoro fulani mwanamke alikuwa na kiwanja cha urithi Mbezi Beach lakini mwanaume alikataa kushiriki kwa namana yoyote kutoa hela yake kuendeleza kiwanja husika, ikabidi mwanamke akubali wakiuze na sasa wana nyumba nzuri Kigamboni maisha ya ndoa ya amani yanaendelea.
jamani,,huwezi jua huyo jamaa yanampata yapi kwa huyo mama kwani story yenyewe ni ya upande mmoja.