hatuwezi kujua kila kitu kinachoendelea hapo. hayao aliyokueleza huyo zilipendwa wako ni ya upande mmoja. inawezekana naye anamfanya ajisikie inferiority kwa kuwa yeye kipato chake ni kidogo na kamkuta mke ana hatua kubwa ya kimaisha. kuna mawili hapo, aither ni inferioritu complex ambayo ni purely psychological issue au ni mke ana ubinafsi na mali zake alizochuma akiwa peke yake hadi mume anakosa amani.
kama lolote kati ya hayo limeishaleta tabu, ni vizuri mwanaume akapewa counseling badala ya kumpuuza ili naye sauti yake na nafasi yake kama mwanaume uhuishwe ndani ya ndoa yake. ushauri nasaha ukiwa unaendelea mwanamke ajitahidi kufuata anachopenda mwanaume huku akimshirikisha kila hatua na ikibidi ampe suti kubwa zaidi kwani mwenziye tayari kishaathirika kisaikolojia, kisha waanze maisha upya kwa pamoja, nyumba, magari ni vitu vya kupita tu na huyo mwanaume anayemdharau huwezijua Mungu kamuhifadhia nini stooni mwake, aweza kuwa siku moja juu kumzidi yeye na ndipo atakapoona haya hata kumdondoshea chozi la huba.
all in all, Mungu ametuita katika amani. ndoa isiyo na amani isyo ndoa na Mungu hapendezewi nayo. kuishi mbagala kwa amani ni bora mara milioni kuliko kuisho oysterbay au masaki bila amani? sembuse mwenge?
Miss Judy nakubaliana na wewe asilimia mia moja,
Lakini kuna kitu najiuliza, hebu tufikirie mwanaume mwenye akili, na utashi,
Mwanaume mwenye kuyajua maisha, na mwenye uwezo wa kuamua kama mwanaume,
Mwanaume ambaye ni msaada kwa mwanamke, kuna mambo huyajui yeye anakufundisha,
na kukuongoza.
Aliweza je kukubali kwa moyo wake wote kuhamia nyumbani kwa huyo mdada,
Ok, labda kuna vitu, vya tofauti ameviona, ilibidi atumie akili ya kiume hapo, sio ya kusema uza,
gari hamia Mbagala, tuangalie na maisha yalivyo, unahama Mwenge unafanya kazi Airtel,
unahamia Mbagala tena kwenye nyumba ya kupanga ni akili hiyo.
Basi angekomaa, akajenga au hata kama ni kupanga kwa ustaarabu na akili,
Na habari ya kuuza vitu ambavyo mmeshapewa na Mungu bila sababu sio akili.
Akili ya mwanaume naiamini ndo maana anaweza hata akukudanganya mpaka uje,
ugundue unadanganywa ushachoka, labda kwa sababu ya neema ya Mungu tunawagundua.
Sasa atumie akili hizo hizo kuhakikisha anakwenda sawa na huyu dada.
Na maendeleo yanakuwepo.
Mambo yakuanza sifuri hakuna.
Akomae na maisha amzidi basi, kama tatizo ni hilo.