ni pm namba yako nikutumie kwa whatsaap kuweka siwezi hapa hii UPDATE ya sasa JF inayeyushawakuu naomba mnisaidie nyimbo za
1. binadamu hawana shukrani -ndanda kosovo na fm academia. unakibwagizo sasa wanaanza kulia eeeh nuhu..eeeh nuhu tufungulie safina. naomba mniwekee hapa wadau
2. nadhan ni mao santiago kama sikosei anasema "marafiki wote wamenikimbia sasa upendo tulipatana umefika wapi.... kibwagizo cha kula kwake vichochoroni,kulala kwake vichochoroni.
naombeni mnisaidie huu wimbo wadau.
ni pm namba yako nikutumie kwa whatsaap kuweka siwezi hapa hii UPDATE ya sasa JF inayeyusha
Mkuu na mm nisaidie jizo nyimboni pm namba yako nikutumie kwa whatsaap kuweka siwezi hapa hii UPDATE ya sasa JF inayeyusha
Mkuu bado hujapata hii ngoma"unavyojitia kununa nuna bila sababu tutaja achana bure, nikuulizapo jambo huja juu, huja juu kipenzi changuu" huu wimbo ipo sauti ya gurumo,bichuka,. Hivi huu wimbo unaitwaje? na ulipigwa band gani? na mtunzi ni nani? pia mwenye audio yake anisaidie!
Bado mkuu! Nisaidie kama unayo?Mkuu bado hujapata hii ngoma
Hata mm cjapataBado mkuu! Nisaidie kama unayo?
makumbele hadi kesho haichuji broPia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....
Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....
Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............
Hakika ya kale ni dhahabu...
SUPER RAINBAL, hakika kazi zao zilisimama ju ya mstari. Huu wimbo aliurudia Binti Ajulikanae kama Rubby mwana dada machachari kweli kweli.Milima ya Kwetu
Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,
japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,
(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,
Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,
Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,
kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,
kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,
kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,
hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,
hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2
Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2
chorus:
walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,
(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,
(chorus)
Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,
Angalia kibao kitamu kama hiki cha Tancut Almasi...
Ninakwendaa safari, safari yenyewe safari ya kikazi,
Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2
Ninakwendaa safari, safari yenyewe safari ya kikazi,
Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2
Ninakwendaa safari, safari yenyewe ya masafa marefu,
Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2
Ninakwendaa safari, safari yenyewe ya masafa marefu,
Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2
Lakini usisikie yaoo mama watoto oo,&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..,
Nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetu&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.,
Chunga watoto wetu mamaa nitarudi, tutaonana kwa mapenzi ya Mungu,
Chunga watoto wetu mamaa nitarudi, tutaonana kwa mapenzi ya Mungu,
Safari sio kifoo o mama iyeye,
Subiri nitarudii o mama watoto,
Safari sio kifoo o mama iyeye,
Subiri nitarudii o mama watoto,
Nikirudi mamaa nitakuletea zawadi,
Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili
Iyeye, oo mama iyee,
Nikirudi mamaa nitakuletea zawadi,
Zawadii nono, mama watooto.
(a keba, keba, keba, keba, keba, keba, keba, kebaaa,)
(fimbo, fimbo, fimbo, fimbo, lugoda,lugoda, lugoda, lugoda - Mangalaa..