ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Napenda kuuliza huyu mama Lady Isa (isabelle) alikuwa anatokea nchi gani kati ya DR Congo au Kenya?
Nyimbo zake
1. Kutereza si kuanguka,
2. Dunia ina mambo (lukumba lukumba)

 
Huu wimbo nimeusaka kila mahali nimeukosa. Kuna mahali mdau aliniwekea wimbo wa Vijana Jazz uitwao -Kapu la Mjanja- Hizi nyimbo kuna mambo fulani nikizisikia huwa kuna kumbukumbu fulan ambazo hunipa hisia kali sana. Kama mkuu Balantanda au mdau yeyote ataweza kuniwekea nitashukuru sana.
 
Daaaaa,ni shida. Siku hizi jaman vipaji viko wapi?
 
DDC MILIMANI PARK Sikinde na wimbo A,B,C D live Nairobi

Source: KinMedia TV
 
FM ACADEMIA 2018 Dar es Salaam, Tanzania timu ni ile ile lakini kocha mpya full dozee wazee wa Ngwasuma chini ya Patcho Mwamba live HD

Source: saluti5.com
 
nyie wazee wa zamani mlishindwa hata kurekodi video za nyimbo zenu au hata performance
 
March 17, 2018
Dar-es-Salaam, Tanzania

Rashid Pembe aelezea siri ya anguko la muziki wa dansi Tanzania lilianzia mwaka 1994 na kufikia kilele mwaka 2004.

Ambapo wadau wakubwa kama studio, media n.k waliofadhili kutoa, kutangaza na kuuza album za muziki wa dansi kuelekeza nguvu zao ktk muziki wa bongo -flava ili hata watoto wadogo wa miaka hiyo ya 90 waikubali.

Anakubali media zina nguvu za kumnyanyua msanii au bendi na kutoa mfano Saida Karoli alivyobaniwa na media alipotea na kurudi kwao. Lakini media walipoamua kumpa airtime Saida Karoli amerudi upya na kuendelea na muziki wake.

Endelea kumsikiliza mpiga saxophone nguli wa Vijana Jazz Rashid Pembe akifunguka wanavyokabiliana na mabadiliko hayo kwa kwenda Facebook, youtube na WhatsApp ili kufikia umma wenye kufuatilia muziki wa dansi :
Source: saluti5.com
 
Nimeguswa na hisia za Mzee Pembe,Vijana Jazz ikiwa iko moto kweli kweli,ndo hivyo zimebaki stori!
Ila sikumpata vizuri,mbona miaka ya 1996/97,Vijana Jazz walitoa Album iliyo hit(Tafrija la Kuuaga Umaskini-Umaskini bye bye) ambapo ilifanya vizuri tu. Naona anguko la Dansi lilianza miaka ya 1999 kuja hadi 2000. Baada ya hapo ilikuja Dansi mpya ya Twanga Pepeta miaka hiyo ya 1999-2006!Twanga,Muungano,TOT,Tam Tam na FM Academia,Beta Musica,Extra Bongo na Dar Musica. Hata hivyo nazo zinaelekea kufutika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…