Huyo ndio Jabali la muziki Marijan Rajab na Dar International mkuu...
Marijan Rajab kabla hajahamia Dar International alikuwa katika bendi ya Safari Trippers ambayo ilisambaratika mwaka 1977......Baada ya Safari Trippers kufa nini kilifuata?.....Mwaka huohuo 1977 mwanamuziki mwingine Nguli chini Abel Barthazar alianzisha bendi ya Dar Internatinal ambayo pamoja naye(Balthazar) pia walikuwepo Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,ALi Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......
Bendi hii ilianza kwa kutoka na vibao kama Nyerere mwanamapinduzi,Rufaa ya kifo,Mwana uoe,Betty,Margreth na Sikitiko,....Vibao hiivi vilitamba hasa na bendi ilianza kushika chati ya juu katika medani za muziki wa Dansi Tanzania.....Bendi hii ilikuwa maarufu ghafla na kwa kupitia Marijan Rajab ilipiga muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo(miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).....Mwaka 1978 baada ya Marijan Rajab kujiondoa bendi haikudumu sana kwani ilisambaratika baada ya wanamuziki nane(08) tegemeo wa bendi hiyo Abel Barthzar(aliondoka kabla ya wenzie),King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jef waliondoka na kwenda kuanzisha bendi ya Mlimani Park Orchestra(baadae DDC Mlimani Park Orchestra).....
Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....
Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........
Hao ndio Dar International Orchestra wana Super bomboka chini yake Jabali la muziki Hayati Marijan Rajab(R.I.P)......