ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Picha za vichwa vilivyopata kutamba na Vijana Jazz...

manetibc.jpg

1, Hemed Maneti Ulaya


JERRY+NASHON

2. Jerry Nashon 'Dudumizi'


DSC03205.JPG

3. Beno Villa Anthony



john+kitime.jpg

4.John Kitime



Kida+Waziri+Vijana+Jazz+1991.jpg

5. Kida Waziri



sully2.jpg

6.Suleiman Mbwembwe(kushoto) na Hamza Kalala(kulia).



DSC07922.jpg

7. Abuu 'Lokassa' Semhando



eddy+vijana.jpg

8.Eddy Sheggy



Shaban+Yohana+Wanted.jpg

9. Shaban Yohana 'Wanted'


IMG_0985.JPG

10. Rashid Pembe 'Profesa'
 
vjn+ogopa+tapeli.jpg

Kiongozi wa UVCCM enzi hizo Mohamed Seif Khatib akiwa na kikosi kizima cha Vijana Jazz kilichotamba enzi za miaka ya mwanzoni ya 90.....Picha kwa hisani ya John Kitime
 
vjn+ogopa+tapeli.jpg

Kiongozi wa UVCCM enzi hizo Mohamed Seif Khatib akiwa na kikosi kizima cha Vijana Jazz kilichotamba enzi za miaka ya mwanzoni ya 90.....Picha kwa hisani ya John Kitime


Mzee Kitime leo ataongoza jahazi la njenje katika vunja jungu...palepale Salender Bridge...
 
Hizi nyimbo enzi hizo mi nadhani raha yake ilikuwa unasikilizia huku unakunywa ulanzi au mbege(pombe za kienyeji)but siyo pombe za sasa hivi.....halafu hivi zile katitu za kenya bado zinaendelea?
 
Kuna kibao kimoja cha Wana msondo nakikumbuka kwa ubeti mmoja tu Bala kama kipo kwenye maktaba yako kipe mwendelezo

..ilikuwa jumamosi ilee... tukiwa msondo ngomaa
kulia kwangu nilimuona binti shakila mwenye furaha...akilisakata msondooo
..nilishindwa kujizuia nikajikuta tupo bega kwa bega
Nilimuomba tucheze nae bila kupinga alikubali...nikamueleza kuwa nimetokea kumpendaaa
..nae akanijibu hapa nimefwata msondo usinifurahishee....wasiliana nami kesho keko machungwaaa ahaa..


Nyimbo inaitwa Mahamudu ilipigwa kipindi inaitwa JUWATA...

Mahamudu eeh ni mashakani
Cha kufanya sikijuiii
Usiku wa Jumamosi ile
Nikiwa msondo Ngomaa
Kulia kwangu nilimuona
Bibi Shakira mwenye furahaa
Akiusakata Msondoo
Nilishindwa kujizuia
Nikajikuta niko bega kwa bega
Nilimuomba tucheze nae
Bila kusita alikubali
Nikamueleza kuwa
nimetokea kumpenda
Nae akanijibu hapa nimefuata Msondo
Nijifurahishe
Wasiliana nami kesho Keko Machungwa...

ZENGEKALA...
Nilipofika Keko Machungwaa
Kama tulivyokubaliana na Shaky
Nilikumkuta nikamuelezaa
Nia yangu tuwe wapendanaoo Mamaa
Alinijibu kwa huzuni kubwaa aaah

WOTE...
Huuuku akitabasam

Dah
 
Nakumbuka kulikuwa na bendi ya Chezimba ilikuwa inapiga Twiga Hotel samora...wimbo wao maarufu "Kijongoo sina nyumba..."
Then kulikuwa na bendi nyingine ikiitwa Bene Bene, Jambo Stars....Of course Tanzanites na wimbo wao "KIdude"

Katika nyimbo za zamani ambayo naitafuta basi ni hiyo ya Chezimba ''Kijogolo sina Nyumba weeh ntajenga Barabarani''
Ntajenga nyumba ya mawe ooh
Ghorofa ndani kwa ndani...

Mara ya mwisho niliisikia Mombasa kwenye nyumba ya Muuza Mirungi dah.
 
Katika nyimbo za zamani ambayo naitafuta basi ni hiyo ya Chezimba ''Kijogolo sina Nyumba weeh ntajenga Barabarani''
Ntajenga nyumba ya mawe ooh
Ghorofa ndani kwa ndani...

Mara ya mwisho niliisikia Mombasa kwenye nyumba ya Muuza Mirungi dah.

hapamtani umenikumbusha mbali wacha na mie niendelee ''' sijaona manowari eeh ikipita barabarani, fimbo ooh fimbo mkononi.....


dah haka kawimbo kalikuwaga katamu sana mi huwa najiuliza ukienda RTD oops sorry TBC Taifa, huwezi pata hizi nyimbo?
 
Kaka Balantanda umepotea kabisa/Unakikumbuka kisa cha kweli cha nyimbo hizi?1) Homa imenizidia (OSS-Bitchuka)2) Mtoto akililia wembe (DDC-Chidumule)3) Nimekubali maneno -Mwana Kaza moyo (DDC)


kati ya nyimbo hizo, mbili za Juu anaimbwa Bichuka na sakata lake la kuhamia OSS.
Homa imenizidia anajiimba yeye mwenyewe na mtoto akililia wembe anachambwa na Chidumule ngoma ngumu ambaye alikuwa na uwezo wa kumshambulia msanii yeyote yule atakayeleta za kuleta
 
hapamtani umenikumbusha mbali wacha na mie niendelee ''' sijaona manowari eeh ikipita barabarani, fimbo ooh fimbo mkononi.....


dah haka kawimbo kalikuwaga katamu sana mi huwa najiuliza ukienda RTD oops sorry TBC Taifa, huwezi pata hizi nyimbo?


zipo zoote hizo ila hawakupi ng'o...
mimi hazina kubwa ya nyimbo za Bongo za zamani nilipatiwa na mzee mmoja Nguli pale Lang'ata Nairobi.
 
Kulikuwa na kiphndi cha rtd kikiitwa
ngano na muziki basi nilihakikisha redio haikosi betrii
 
Miaka ya 1980 Nilijaliwa kuziona LIVE bendi nyingi DSM kama Mwenge Jazz Paselepa, Urafiki, Biashara Jazz, Bima Lee, Tancut Almas, Uda Jazz, Mlimani Park, Msondo Ngoma, Remmy Ongala na O'chestra Matimila, Maquis, baadaye nitakuja na orodha ya wanamuziki niliowashuhudia kwa macho, kwa kweli kuna tofauti kubwa sana na sasa!
 
Ubaya uliuanza zamani wakati ningali mdogo...
Na hayo unayo yafanya kaka si mageni hapa ulimwenguni
Wala usije ukajisifu kwa uhodari wa maovu yako
Na hata mtenda mema huwa hajisifu...
Kaa chini ufanye uteuzi ni lipi la kufanya kwani ubaya haulipwi na pia wema hauozi x2

''Chagua moja''

Ubaya uliunza zamani ''zamani sana'' wakati ningali mdogo
Mambo unayoyafanya huko uliko
Nimeshasikia

Ubaya uliuanza zamani ''zamani'' wakati ningali mdogo
Nafanahamu lengo lako nieleze tunacho gombania

Ubaya uliuanza zamani ''saana'' wakati ningali mdogo
Kama ni kipato chatokana na bidii zangu

Ubaya uliuanza zamani ''zamani sana'' wakati ningali mdogo
Mambo unayoyafanya huko uliko nimeshasikia

Ubaya uliuanza zamani ''saana'' wakati ningali mdogo zamani
Nimefahamu lengo lako nieleze tunachogombania

Ubaya uliuanza zamani ''saana'' wakati ningali mdogo
Kama ni kipato chatokana na ujuzi wangu

''Mulenga''
 
Ingali bado najiuliza usiku na mchana
Na mume wangu kanitoka
upweke umenizunguka eeh

Watoto wamekuja juu
Wanadai nyumba yao
Watoto wamekuja juu
wanadai nyumba yao

Na kila nikifikiria jinsi nilivyo taabika
na malezi ya watoto ingawa sikuwazaa

Watoto wamekuja juu
Wanadai nyumba yao
Watoto wamekuja juu
Wanadai nyumba yao

Ingali bado najiuliza
Usiku na mchana
Na mume wangu kanitoka upweke umenizunguka ee

Watoto wamekuja juu
Wanadai nyumba yao
Watoto wamekuja juu
Wanadai nyumba yao

Kila nilifanyao wao haliwapendezi
na wala hawakumbuki
usia wa Baba yao x2

aaah Marehemu alihusia
wasinitupetupe
Wala msininyanyase Maama
Ooh Mamaa
Mmmh marehemu alihusia eeh
Msininyanyase
wala msinitupetupe Baba eeh
Oooh Mama
Mmmh marehemu alihusia eeh
Wasinidharau
Wala Msininyanyase Baaba eeh
Ooh Mama

Majirani wameshauri eti niwashitaki
Wakati nyumba ni mali yao
jama nifanye nini
Wengine wameshauri eti nirudi Nyumbani
sina Baba wala Mama
Huko niende kwa nani

aaah Marehemu alihusia
wasinitupetupe
Wala msininyanyase Maama
Ooh Mamaa
Mmmh marehemu alihusia eeh
Msininyanyase
wala msinitupetupe Baba eeh
Oooh Mama
Mmmh marehemu alihusia eeh
Wasinidharau
Wala Msininyanyase Baaba eeh
Ooh Mama
 
Baba Anna ee
Ni lini utarudia nyumbani
Uje uwaone watoto wako
Uje uwaone Baba na Mama kwetu X2

Najua kazi nyingi zimekuzonga
Huko uliko nako ni mbaali sana
Baba Anna eeh
Hata hivyo ufanye kila njia
Kwani kuna matatizo matatizo matatizo kwetu eeh

Baba Anna ee
Ni lini utarudia nyumbani
Uje uwanone watoto wako
Uje uwaone Baba na Mama kwetu

Najua kazi nyingi zimekuzonga
Huko uliko nako ni mbaali sana Baba Anna eeh
Hata hivyo ufanye kila njia
Kwani kuna matatizo matatizo matatizo kwenu eeh

Baba Anna eeh
Ni lini utarudia nyumbani
Uje uwanone watoto wako
Uje uwaone Baba na Mama kwenu

Watoto wako wanakukumbuka
Kila siku hawaishi kukuuliza
Na mama nae ananung'unika
Kwani miaka mingi imepita
Baba amekuwa mtu mzima
Hawezi kuhangaika huku na kule
Kwa hiyo bwana ufanye haraka
Matatizo yametuzidi ooh x2

Fanya ujee
Leo nasema
Fanya ujee
Bwana naomba
Fanya uje
Niko peke yangu
Fanya ujee
Maisha ya tabu
Fanya ujee
Kila kitu ni pesa
Fanya ujee
chakula ni pesa
Fanya ujee
mavazi ni pesa
Fanya ujee
Eeh bwana
Fanya uje
ufanye haraka
Fanya ujee
Leo nasema ooh
Fanya ujee
Bwana naomba
Fanya ujee
 
Bwana mdogo sogea nikutume eeh
Sogea nikutume ye ye ye yeee
Bwana mdogo sogea nikutume ooh
Sogea nikutume ye ye ye ye
Heey young brother come cross to me
I need you come cross to me brother
I want to take my greatings back home
Tell my Grandmother that am still sweat in town
I want to take my greatings back home to the village telling my grandfather that am still sweating in town
Life in town means more money, if you dont have money you will suffer, if you dont have money you'll never sleep, if no money you cant never eat, you cant even wash your own clothes, pesa pesa jama inaleta maneno, kweli pesa pesaa inapeleka watu jela ayaa wouooo Mama yo yo yo nalia mie...

Kurudi nyumbani mama tunaona haaya, mikono mitupu mama tutarudi vp, tumepoteza miaka mingi mjini Dar Es Salaam
Kweli pesa pesa inaleta maneno
Jama pesa pesa pesa pesa inapeleka watu jela ooh

Life in town means more money, if you dont have money you will suffer, if you dont have money you'll never sleep, if no money you cant never eat, you cant even wash your own clothes, pesa pesa jama inaleta maneno, kweli pesa pesaa inapeleka watu jela ayaa wouooo Mama yo yo yo nalia mieEe
 
Back
Top Bottom