Dahh! Asante sana Balantanda na wengine wote kwa kazi nzuri. Naumba kuuliza kuna mtu aliimbwa na vijana jazz. Wimbo unahusu sherehe ya kuuaga umasikini mtu huyo aliitwa Joseph Pauline unao kwenye maktaba yako . Tafadhali naomba niwekee Kama upo
Yote aliyofanya ndugu yangu Joseph Pauline ni sawaa au amekosea eeeh ni sawa au amekosea a eeeh .
Pauline kafanya mambo katuacha kwenye mataa ee Pauline .....
Katuacha tumeduwaa eeh
Vyombo......
Chorus. ......Jambo la kushangaza Pauline kafanya party la kuuga umasikini eeeh, Pauline oooh oohh laa la la laaa la.
Tumesukuma nae mikokoteni maskani ooohh oohh jama aa Pauline rafiki yetu la la la la
Chorus repeats!
Watu wengi walihudhuria pati hilo ooo
Fred Benjamini alikuwepo
Toto Tundu alikuwepo
Shomari Ally akikuwepo
Shakashia alikuwepo
Suleiman Mbwembwe alikuwepoooo
Mkuu nimekumbuka mistari hiyo japo kwa kujivuruga. Majina ya wanamuziki waliotajwa kwenye wimbo huu walikuwa mahiri sana wakati ule. Na ni katika Album hii Vijana Jazz ilianza kufifia. Wengi waliondoka na wengine walishatangulia mbele ya haki. Ni Album ya msimu wa 1996/97. Baada ya hapo Vijana haikutoa Album iliyohit kwani ilitoa I love you Mpiga debe miaka ya 1999 na Mabaa Maid miaka hiyo ya 1999/2000.
Sababu kubwa ni viongoz wa bendi yaani UVCCM kuipa sapoti kubwa TOT Band.
Album hiyo yenye wimbo ulioutaja ndo ya mwisho katika mtiririko wa Pure Vijana Jazz Air Pamba moto, Saga Rhumba! Ukiondoa wimbo huo, nyimbo zingine nzuri kabisa katka album hiyo ni Mama Samia, Mbuzi yake kamba nk. Naitafuta hii Album katika CD ila naikosa. Ninayo kwenye tape, bahati mbaya vifaa vyangu siyo rafiki tena kwa tape.
Ila Bantalanda ninashida sana na wimbo Kapu la Mjanja na Janja ya Nyani pamoja na Visa vya Mume.
Wimbo huu visa vya mume naupenda sana hasa pale wanaposema- Nikipika wali unasema una mawe e , nikipika ugali unasema una mabuja sema kinachokukera bwana eeeh. Ilikuwa ni combination ya hatari wakina Adam Bakari( sauti ya zege). Daa zaman kulikuwa na Muziki na Vijana Jazz ilikuwa ni noma. Ila nayo ilipata Upinzani mkali kutoka Washirika Tanzania Stars(Watu Njatanjata) na Bimalee.