ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Kitu Maiga cha Marquiz du Zaire.
Solo alisimama Nguza Viking
Bass: Banza Mchafu
Kwenye kuimba alikuwepo Mutombo Lufumbu, King Kikii, Mbuya Makonga. Ila niliipenda zaidi saxafone la Mafumu Bilal.
 
Majumba na maeneo ambayo vijana wa zamani, nikimaanisha wale wa miaka ya 80's na 90's walikuwa na maeneo yao ya kujidai, haswa wale watoto wa mjini. Kulikuwa na majumba kadhaa ya kucheza disco.

Sea View (Sansui) = DJ Seydou (Afro 70, Safari Trippers wakipiga hapo)

Africana = DJ Mehboob

Motel Agip na New Africa hotel ghorofa ya saba = DJ Emperor (Joseph Kusaga wa Clouds fm), Boniface kilosa alias Bonny Love na DJ Jesse Malongo.

Rungwe Oceanic Beach Resort kwa Mzee Mwakitwange = DJ Ngomely, DJ Pop Juice

Silver Sands = John Peter Pantalakis, Mzee mzima Choggy Sly na Kalikali baadaye alihamia YMCA.

New Space 1900, Mbowe hoteli = Chriss Phabby

New Vision = DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela, DJ Young

RSVP Discotheque = Saidi Mkandara a.k.a DJ Seydou na DJ Gerry Kotto.

Keys Hotel = DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis

Ukienda kwenye hayo madisco, wapiga picha maarufu walikuwa Bob Spear narafiki yake, kisha akaja Issa Michuzi.

Style kubwa za uchezaji disco zilikuwa Robot, Breakdance, Reggae, Rhumba na Chachacha.


Nyimbo kama hizi zilitamba sana.

Easy - Commodores


Endless Love - Diana Ross & Lionel Richie


I'm Coming Out - Diana Ross


Midas Touch - Midnight Star


Forget Me Nots - Patrice Rushen


Let The Music Play - Shannon


Don’t StopTill you Get Enough - Michael Jackson


Master Blaster Jammin - Stevie Wonder


A Night To Remember - Shalamar


Ukienda kule kwenye madisco ya Uswahili haswa madisco ya Jeshini utakutana na ngoma za bakurutu kina TP Ok Jazz na Franco, Tabu Ley, kwenye majumba ya disco ukitaka kuwaudhi basi piga hizi nyimbo tukizita nyimbo za Bolingo.

Le T.P. O.K. Jazz Mzee Franco


Massu


Maze - Tabu Ley Rochereau



Ukitaka kuzifaidi nyimbo hizi, basi tulizifaidi sana kule viwanja vya sabasaba, kwenye banda la Yahaya Hussein.


Aisee kweli JF kuna watu. Khaa!!
 
Last edited by a moderator:
Umesahau msasani beach,ambapo alianza Eddy sally na choggy sly.
 
Baadaye wakaja Jpp,Double k triple t,dj Rusual,the Rach cutty,Baharia Agib show
 
Tumezisahau bendi za majeshi,police jazz alikotoka tx wana vangavanga,mwenge jazz ,akina George mpupua,Luza ktk sax,jkt kimbunga stereo,jkt kimulimuli mzee Zahiri ,ilikuwa hatari alipoimba hadithi ya mapenzi
 
Marijani,toka safari trippers wana sokomoko ,Dar international aliimba mayasa,Vicky ,style ni super bomboka
 
Wakati walipokuwa kampuni (omaco)maquiz walikuwa white house njia ya kwenda msewe,kuna gereji hapo sasa.pale ilikuwa telemukaaa ,chekeeecha
 
marquiz waliimba wimbo unaitwa WANAUME WA LEO...dah ni balaa
 
Hapa ni Shaban Dede katika ubora wake;

(Mawazo yamezidi,
moyo unakereheshwa mama ee,
nakuwa kama kichaa,
kwa mawazo niliyo nayo,
mimi nawe kutengana dada) x2

Kutengana kwetu bibi,
mimi kunanishangaza sherii,
umeshahu kabisaaaaa,
Kiapo cha harusi yetu,
wanisikitisha sana.

Mulenga,

mtoto wa mama Tujemaso
wanikondesha bure mama,
aaa Tujemaso,
wasema mimi sikujui,
wala hunitaki tena.

(Unasema mimi masikini
Sikupeleki disco wala sinema,
kumbuka hizo ni starehe,
wala zisiwe sababu,
ya kufanya tutengane dada) x2

 
Last edited by a moderator:
kibao cha fransisca sikumbuki aliimba nani ila maneno nayokumbuka miaka hiyo ya 80s mwishoni yalikuwa ni hivi.
mwenzenu makubwa yamenikuta...
sijui nifanye nini fransisca aelewe kwamba
nafasi yako bado ipo moyoni mwangu ....
ukimuona huko aliko mwambien kuwa nateseka sanaa
...........

hizi ni nyimbo zinazonikumbusha zamani sana enzi hizo tunasikilizo RTD vipindi kama MICHAKATO,WAKATI WA KAZI,SALAMU KWA WAGONJWA,CLUB RAHA LEO SHOW,.... kipindi hicho nasoma shule ya msingi tukiwa tunaingia vipindi vya saa sita na nusu nakuwa home nasikilizia kipindi cha wakati wa kazi. ukisikia watu kama akina bokoman mwana mkongo man ,tewa s tewa, kunguru mwoga, father nagumo fanani comoro wakitumiana salamu na kupeana jumbe moto moto. halaf inapigwa song... usipowajibka shauri yako uyakumbwa na fagio la chuma n.k
 
natafuta sana hiki kibao cha Komandoo Hamza kalala .. nalila masumanda.... huko uliko ni mbali e mamaa eeeehh yaa nalila masumanda ...eeeh...ling'ombe nalila....
 
kibao cha fransisca sikumbuki aliimba nani ila maneno nayokumbuka miaka hiyo ya 80s mwishoni yalikuwa ni hivi.
mwenzenu makubwa yamenikuta...
sijui nifanye nini fransisca aelewe kwamba
nafasi yako bado ipo moyoni mwangu ....
ukimuona huko aliko mwambien kuwa nateseka sanaa
...........

hizi ni nyimbo zinazonikumbusha zamani sana enzi hizo tunasikilizo RTD vipindi kama MICHAKATO,WAKATI WA KAZI,SALAMU KWA WAGONJWA,CLUB RAHA LEO SHOW,.... kipindi hicho nasoma shule ya msingi tukiwa tunaingia vipindi vya saa sita na nusu nakuwa home nasikilizia kipindi cha wakati wa kazi. ukisikia watu kama akina bokoman mwana mkongo man ,tewa s tewa, kunguru mwoga, father nagumo fanani comoro wakitumiana salamu na kupeana jumbe moto moto. halaf inapigwa song... usipowajibka shauri yako uyakumbwa na fagio la chuma n.k
Wimbo wa Francisca waliimba Legho Star Band wana 'Sopa bango'...

Wimbo ulitungwa na kuimbwa na 'mtoto mzuri' Tshimanga Kalala Assossa...Kinanda kilipapaswa na Anania Ngoliga...

RTD hakujawahi kuwa na kipindi cha 'MICHAKATO'....Ni kipindi cha 'MISAKATO' ambacho kiliasisiwa na kutangazwa na Uncle J...Julius Nyaisangah (R.I.P)...
 
natafuta sana hiki kibao cha Komandoo Hamza kalala .. nalila masumanda.... huko uliko ni mbali e mamaa eeeehh yaa nalila masumanda ...eeeh...ling'ombe nalila....
Nalila Masumanda ni wimbo uliotungwa na Komando Hamza Kalala akiwa na Washirika Tanzania Stars Band 'Watunjatanjata'...Baadae aliurudia wimbo huu akiwa na bendi yake ya Bantu Group....

Nakucha nakubulagwa maganiko....Hamza Kalala....Nalila masumanda eeh...

Nakucha nakubulagwa maganiko....Hamza Kalala....Nalila masumanda eeeeh...

Huko uliko ni mbali e mama Stella...nakung'wila ki...Nalila masumanda eeeh...

Nalihaya kwiza nassa....Aliyo naliduma...Nalidumila kunguno...

Ing'ombe jamala masundo...Nakung'wila ki....Nalila masumanda eeeh...


Huko uliko ni mbali e mama Stella...Nakung'wila ki....Nalila masumanda eeeh...
 
Back
Top Bottom