ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

natafuta sana hiki kibao cha Komandoo Hamza kalala .. nalila masumanda.... huko uliko ni mbali e mamaa eeeehh yaa nalila masumanda ...eeeh...ling'ombe nalila....
 
Mbaraka Mwinshehe na moro Jazz wimbo wa kuwapongeza waandishi wa habari niliupenda sana.
"Twawapa hongera waandishi wetu
Wa magazeti wa Afrika mashariki
Kutuletea habari motomoto
Za kila siku kwa wasomaji wenu
Ni Moro jazz kwa niaba ya jamii
Twawapa hongera kwa kazi zenu safi,bidii twawaomba muongeze, tuzidi kupenda magazeti yetu"
 
huwa nakaa nasikiliza hizi nyimbo nakumbuka mbali sana. miaka hiyo tunasikia mv mapenzi, neema, siwema mtu mzima marijan, talaka ya hasira- akiambiwa aangukie anatoa pesa nyingi.. kuliko ile mahali aliyotoa... ukisikia milima ya kwetu- nikitizama milima ya kwetu.... au solemba na ukaingia msemo wa " jamaa amemwacha solemba" baadaye ndo ukaja msemo wa kumwacha mtu kwenye mataa. sisi wa enzi hizo kumwigiza mtu mjini ilikuwa ni kumwacha solemba.
 
nashukru kwa marekebisho taarifa nimeipokea. ni kweli ilikuwa ni misakato na alikuwa akiendesha uncle j nyaisangah kama pia alivyokuwa kwenye club raha leo show na general tyre na gari lako.
 
Duh! kuna hii pili mswahili mtaalamu mareno batembo imekuwa siku nyingi kibao hiki.
 
Wakuu mwenye wimbo ule wa Magereza Jazz "Ashura" auweke hapa tafadhali.
 
Mi nalia tu na wimbo wa NALILA MASUMANDA WA HAMZA KALALA... NTAUPATA WAPI WADAU? MWNYE NAO AUWEKE HAPA AU ANI PM tafdhari tubadilishane nyimbo kadhaa za kale ntampatia nami
 
Kama huamini nenda mombasa au unguja kama huamini wee nenda mombasa au unguja kijogolo sina nyumba wee ntajenga barabarani ntajenga nyumba ya mawe ooh gorofa ndani kwa ndani, ushaona manuari wee ikipita barabarani
 
Kama huamini nenda mombasa au unguja kama huamini wee nenda mombasa au unguja kijogolo sina nyumba wee ntajenga barabarani ntajenga nyumba ya mawe ooh gorofa ndani kwa ndani, ushaona manuari wee ikipita barabarani
Chezimba band katika ubora wao...

Ndani ya Kilimanjaro Hotel....

Band ya Paul Muto hii....Hapa Muddy, Pale Rachi, Kuti, Ones T, Bruno Njohole na wengineo....Bila kumsahau Baunsa wa band aliyeitwa Noriega...

Hapa Chezimba band...Pale Tatinane ya Omary Naliene na Abdallah Dullaj....Pale the Tanzanite band ya John Mhina....(Pajero pajero lonannichengua....Nimeinama nimeinuka nimeokota kidude)....

Hakika ya Kale ni dhahabu...
 
"Nimesimama kwenye kona...
ya uhuru na msimbazi natizama wanaokwenda wanaorudi mama huende nikaiona sura yke tumaa
Usinione nimekonda ewe tuma hakuna lingine mama ila ni ww tumaa
Usiku wote nalala nikikuota nakuita jina lako ooh ooh tuma naomba mama km unanisikia unikumbuke japo kwa barua mamaa
 
Balantanda shukrani kwa uzi murua nimeupitia na nimefarijika.

Mwenge jazz nao walikuwa na ngoma kama sikosei inaitwa kupatwa kwa mwezi au dunia duara sijui jina halisi sema wimbo naupenda japo mi ni wa juzi
 
Last edited by a moderator:
Balantanda asante sana...umenifanya nikumbuke mbali sana..... huu wimbo umetulia nikisia na mdomo wa bata unavyopulizwa nakumbuka miaka hiyo ya 90 nasikia huu wimbo kwnye kipindi cha wakati wa kazi.... asante sana mkuu. nalila masumanda
 
Last edited by a moderator:
kuna wimbo una maneno kama sijasahau... wanaimba wanasema
"judy eeeehh eehh nikupe nini uridhike ,judy eeh chakukupa sina mama eehh...
ufukara nilio nao..ufukara umekuwa kashfa ya mapenzi yangu...
nlizunguka dunia nzima kukupenda....
sijui waliimba akina nani na unaitwaje au nani anao
 
kuna wimbo una maneno kama sijasahau... wanaimba wanasema
"judy eeeehh eehh nikupe nini uridhike ,judy eeh chakukupa sina mama eehh...
ufukara nilio nao..ufukara umekuwa kashfa ya mapenzi yangu...
nlizunguka dunia nzima kukupenda....
sijui waliimba akina nani na unaitwaje au nani anao

Anaitwa EDDY SHEGGY(RIP) Washirika stars watunjatanjata,unanikumbusha zamani sana Tukuyu Mbeya Magereza shule ya msingi.
 
Shukrani kwenu Balantanda BAK na wengineo kwa kutukumbusha enzi zetu when music was music!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom