Heri ya Mwaka mpya wadau....
Za mwaka mpya safi mkuu. Kea sasa Tanzania hatuna Music, ni pigo kubwa sana!
Sikinde, Msondo, Vijana Jazz, Washirika Tanzania Stars, Bimalee, Polisi Jazz(mkote ngoma-Ashura),Bantu Group, Marquiz nk zilikua bendi zilizoitambulisha Tanzania abroad, ni kwa masikitiko makubwa nyingi ya bendi hizi zimekufa na hata magwiji wake wengi ni marehemu na wengine umri umewatupa mkono, na sioni dalili ya muziki mtamu kwa level ya miaka ya 80-1997. Mwaka huo wa 1997 ndiyo muziki wa Dansi Tanzania ulianza kufifia, mwaka huo wa 1996-97 Vijana Jazz walitoa Album yao ya mwisho kwa hadhi ya Vijana Jazz(Umaskini bye bye)! Katika Album hiyo wakongwe walimaliza kazi hiyo ni:Fred Benjamin, Toto Tundu, Shakashia,Shomari Ally,Suleiman Mbwembwe na wengine. Baada ya hapo Vijana Jazz ikapoteza dira, wakatoa Album ile ya Mabaa Medi na I Love You Mpiga Debe, ambayo kwangu mimi nasema haikufuata mitindo ile halisi ya Vijana Jazz tuliyoizoe na hapo ikawa mwisho wa Dansi za miaka ya 80-90!
Zilikuja bendi za dansi ya kisasa kama Twanga Pepeta, Double M, Mchinga Sound, Muungano Band, Tam Tam na T.O.T Band. Hicho ni kizazi cha dansi miaka ya 2000-2005 hivi, baada ya hapo zikaanza kutoweka taratibu, na leo 6/2/2016,ukiniuliza zilizobaki hata sijui zaidi ya Twanga Pepeta ambayo nayo miaka ya 2010 kuja huku mbele ikaanza kutofanya vyema.
Kwa kifupi Muziki wa Dansi umekufa na Bongo Flavor haina mwelekeo,tupo kama hatupo,inasikitisha kweli!
Nimalizie kwa kumbuka nyimbo hizi, kama Bantalanda ukinipatia Lyrics zake nitashukuru sana:-
1. Vijana Jazz(Top Queen,Shoga,Kapu la Mjanja, Janja ya Nyani)
2.DDC( Naomi, Naomba Tuaminiane)
3.Washirika(Penzi la Ulaghai, Nimekusamehe, Ukewenza-Kulala Sebuleni)
4.Marquiz(Leila, Makumbele)
5.MCA( Shida, Kasoro yangu)
6.Bantu Group(Baba Jane I & II)
Moja wapo ya nyimbo hizo nakuomba uniwekee Lyrics kwa wowote utakaofanikiwa kuupata kwenye Library zako ahsante
Chaza/Oyerster!