ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

kaka kuna viba vya zamani 2 navitafuta kwa udi na uvumba, nio tayari utoa 40,000tsh kwa yeyote ataenitaftia.
1. kivumbi kimenizonga (ioss ya Ndala kasheba) na tucheze sote tukunyema ( Mk beats ya shem karenga)
 
kaka kuna viba vya zamani 2 navitafuta kwa udi na uvumba, nio tayari utoa 40,000tsh kwa yeyote ataenitaftia.
1. kivumbi kimenizonga (ioss ya Ndala kasheba) na tucheze sote tukunyema ( Mk beats ya shem karenga)
 
Kuna wimbo mmoja una maneno "Emmy nikubalie" nautafuta sijui nani kauimba
 
Mwenye wimbo wa ALLY ZAIRI ZORRO unaitwa BEATRICE Affair anisaidie please... 'sisi sote milele beatriceee.... Sisi sote milele kama watoto wazur wapendezaoo
......................
 
habari wana JF
leo naomba tukumbushana nyimbo za wakati ule miaka ya tisini had elfumbili wakati wa utawala wa mzee wa ruksa hadi rais mkapa...upi wimbo ambao ulkua ukiusikia unakukonga moyo...wimbo kama kitambaa cheupe,kasuku, rangi yaa chungwa n.k
 
Rangi ya chungwa sijui walini ila najua niwa kitambo ulionikosha
 
Shambani shambani
Mazao bora shambani
Haya twendeni shambani
Wananchi tukalime
Tusikae mitaani taani
Wanawake kwa waume waume
 
kuna wimbo ulipigwa na Tancut ulikua unaitwa "mapenzi ya pesa" ni moja ya nyimba njuri zilizowahi kupigwa na bendi hii, ujumbe ulioko kwenye huu wimbo unaonekana dhahiri katika miaka ya leo hii, japo ni wimbo uliopgwa enzi hizo
 
Bwana Balantanda naomba unisaidie jambo moja kuna wimbo nautafuta sana japo sijui unaitwaje na ulipigwa na bendi gani lakini baadhi ya maneno yalio kat
ika wimbo huo yanasema " ......... Sophia Sophia mtoto wa mamaa, tafadhali jaribu kubadilika......"
 
Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....

Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....

Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............

Hakika ya kale ni dhahabu...
umemsahau King Kiki
 
Wadau wimbo Wa Vijana jazz wenye mane no "nakula futari bila kuswali..." Unaitwaje!?
 
Bwana Balantanda naomba unisaidie jambo moja kuna wimbo nautafuta sana japo sijui unaitwaje na ulipigwa na bendi gani lakini baadhi ya maneno yalio kat
ika wimbo huo yanasema " ......... Sophia Sophia mtoto wa mamaa, tafadhali jaribu kubadilika......"
Marquis Original
 
Jamani mwenye link ya wimbo wa marijani unaitwa uamuzi wa kuoa sasa hivi sana
Duu nina historia yake kubwa sana
 
natafuta huu wimbo

[Sara(Wacha Majivuno) - Urafiki Jazz band ]



Heeee Sara wacha majivuno ee

Usiwe kama Mwanaisha

Kanikataa sababu mimi ni Mshona Viatu eee


Kampata aaa Mshkaji mwingine ehehe hee hee

Mwenye gari kubwa sana mtumba

Kavunja uchumba mwanaisha sababu mimi ni Mshona Viatu ee



(Chorus)



[Wote]

Tamaa yako Mwanaisha, itakuponza,
Kwa kumfuata yule bwana mwenye mtumba,

Mwanaisha ,Mwanaisha, ogopa sana mamaaaa
kazi ni kazi Mwanaisha , bora mkono uende kinywani eeeh

aliye na huu wimbo aniibox tafadhali nimeshautafuta sana
Nenda kwa Wanne Star Mtoni kwa Aziz Ali.Utapata kila wimbo unaoutaka.
 
Umenieleza mazuri toka mdomo wako oh
Bila kupinga nikaamini bila shaka ah mamaa
kumbe mwenzangu una mengi moyoni eh
Usije ukapata tabu ukaanza kilioo
Niachie mimi nilie nimekwisha zoea aha

Kusema kweli sura yako wee dada uzuri wa sura yako unachenga watu hee
Umenikatili na mapenzi yako ee mama hiyohiyo....
Oo mamaa oo yeleliyo ooh mimi namlilia Ziada.
Shemeji usiondoke nyumbani subiri uwe shahidi,Ziada hayupo nyumbani yapata mwaka wa tatu.

Huyo alikuwa marehemu Kabeya Badu akilalamika katika wimbo wa Ziada.Daa!RIP.
 
Back
Top Bottom