ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

BYRON LEE AND THE DRAGONAIRES - TINEY WINEY - (MUSIC VIDEO)




Un verdadero clasico, no podia faltar en mi lista de videos! disfrutenlo y comenten... a bailar!
Source: Miguel Palacios
 
Ben Pol - Sikukuu (Official Music Video)

Ben Pol perfoming Sikukuu (Christmas) which was originally performed by George Kinyonga & Orchestra Jobiso.



Source : Ben Pol
 
Hii kitu inanikumbusha mbali sana - pikiniki darasa la Saba!! ilikuwa hatareee hasa ikifika pale kwenye chorus!! dakika ya 4 sekunde 30..sikia kitu hichoo

 
"wengi wamelazwa hospitalini na kuwekewa P.O.P shauri yako Hawae,Hawae P.O.P aah P.O.P......"
Nani anakumbuka umepigwa na nani?
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki,Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga,Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.

Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
EKA MADA ZENYE MAANA KWA JAMII BHANA. SASA NDO NINI ETI OOH JUWATA JAZZ SIJUI MSONDO .DAH HIYO NI KUCHOSHA AKILI ZA WATU BURE TU.
 
Man Kifimbo - Nataka Kucheza (Official Music Video) feat. Baby Pelkonen


 
February 19, 2020

MJENGONI CLASSIC BAND

Mapenzi yanauma Rmx Digital Mukongya Feat Nyoshi El Sadaat, Patcho Mwamba, King Kikii, Babu Bomba & Dully Sykes

Muunganiko mkali kati ya magwiji wa muziki wa Dance tanzania, video itakayokuwa gumzo na mwanzo mpya kwa wanamuziki wa Dance Tanzania



Source: Mzee Musika
 
EKA MADA ZENYE MAANA KWA JAMII BHANA. SASA NDO NINI ETI OOH JUWATA JAZZ SIJUI MSONDO .DAH HIYO NI KUCHOSHA AKILI ZA WATU BURE TU.

Dogo, JF ina majukwaa chungu nzima, kama hili la burudani halina maana kwako pita kimya kimya! Nenda kwenye jukwaa lenye maana kwako na linalokuchangamsha akili!
 
Back
Top Bottom