Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....
Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.
Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch ‘King Michael' na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....
Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....
Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....