taarifa zinaenea kwamba zile karatasi za kura zilizokuwa zimekamatwa kule Tunduma kwenye lori inasemekana zimerudishwa Zambia na badala yake zimeingizwa nchini kwa ndege bila kutua kwenye kiwanja chochote cha ndege za abiria, bali sasa zimetua kwenye kiwanja cha ndege za kijeshi kwenye kambi ya Ngerengere, mkoani Morogoro.
Imetumika mbinu ileile kama ya Meremeta kwani ukiongelea Meremeta basi inaelezwa kwamba ni suala la kijeshi na hivyo ni suala la ulinzi na usalama wa Taifa na halipaswi kuongelewa. Na kwa sababu Ngerengere hapakanyagiki kiurahisi basi hata ndege ikitua pale hakuna anayeweza kuweka wasiwasi.
Ndiyo sababu si rahisi kumsikia hadharani mtu akitaja kwamba zile kura tayari zimo nchini lakini sasa ziko Ngerengere zikisubiri kusambazwa kulikopangwa.
Baada ya kufanikisha kuziingiza sasa imebaki kuzisambaza ktuoka hapo Ngerengere jeshini. Hivyo inabidi kukaa mkao wa kujua kuwa hilo lipo.
Tuendelee kusambaratisha mbinu hata kwa kutaarifiana hivi.