Zima gari lako haraka kama ikiwaka taa hii kwenye dashboard

Zima gari lako haraka kama ikiwaka taa hii kwenye dashboard

Mkuu nimegiza kagari kangu RAUM nitumie njia gani kuweza kutunza katika matumizi
 
Yangu kwa zaidi ya miezi 6 ilikua inawaka hii taa na kuzima, mara nyingi nikiendesha kuanzia 10km inawaka, pia nikiwa nimesimama kwenye jam inawaka na gari kuzima.

Baadae camshaft ilikatika, wakati mafundi wanafunga Camshaft nyingine walikuta pia oil pump ni mbovu.
 
Yangu kwa zaidi ya miezi 6 ilikua inawaka hii taa na kuzima, mara nyingi nikiendesha kuanzia 10km inawaka, pia nikiwa nimesimama kwenye jam inawaka na gari kuzima.

Baadae crankshaft ilikatika, wakati mafundi wanafunga Crankshaft nyingine walikuta pia oil pump ni mbovu.

Huenda upande mmoja wa Crackshaft vyuma viligangiana kwa sababu ya joto ndo maana ikakatika.
 
Hii kitu imenicost mwaka Juz natokea mkoani nmeianza kongowe kibaha naelekea dar.

Taa iliwaka nikaipuuza kwa kuchukulia kwamba nmetoka mkoani nmetia oil mpya Tena BP, litakua wenge la Gari Hilo.

Aisee, Kilichonikuta.
Ile nmeimaliza mawasiliano naikaribia mlimani city, Gari ikazima.

Nikajua itakua issue ya umeme,
Akaitwa fund umeme akapima na kunambia iko fresh ila ikipiga starter engine haizunguki. Akamwita mwezake specialist wa engine.

Jamaa kufika kupima oil, nyepesi Kama maji afu imebaki chache mno.

Kagua kila sehem, hamna panakoonesha leakaje. Ikaonekaa Ile oil nilipigwa.

Hii ilinipa funzo maana kabla ya hapo nilikua nanunua kwa dealers kwa elfu70 kidumu, Hii iloleta majanga nilinunja kwa elfu55 mpkani uko.
Nikijisifu kwamba Hapa bongo tunapigwa mno kumbe

Ilinicost kununua shaft mpya, piston mkono mmoja mpya na vikorokoro vingine kibao. Engine ikafumuliwa upya na kueukwa upya.

Issue ya kipumbavu kabisa,
Kila kitu kabisa almost Ilinipasuka 850k kimzaha mzaha.

NAJUTA KUTOKUUSOMA UZI WAKO MAPEMA.

Mtoa mada mungu akupe maisha marefu[emoji120]
 
Natamani ningesoma huu uzi kabla ya September mwaka jana.

Nilikua na 1hz, hard top. Hapo ni kama siku 3 imetoka service, naenda zangu field. Baada ya km27 ikaniwashia hii taa, nikasema ngoja niikokote nimalize hili korongo niegeshe. Masikini weee....

Gari ilizima wakati napandisha lile korongo, na baada ya dk1 ndani kulikua kuna nuka ile harufu ile (kama limewahi kukukuta then unaijua ile harufu ya kuungua).

Ile kufungua bonet, ni imetapakaa oil tupuu, uvungu wa gari wote umejaa oil, nyuma kwenye spare tyre na vioo ni oil tupu.

Kumbe jamaa walifunga filter vibaya, ile rubber nyeusi ilikua imetwist, haikukaa sawasawa kwenye reli yake, upande flani imeweka seal, upande flan iko wazi. Kwahiyo pressure ya oil ilivyozidi, ikafumua palipo weak, yote ikaishia pale.

Ilibidi niwaangushie jumba lao bovu, tulisumbuana ila mwisho wa siku walifix kila kitu kwa gharama zao, maana ulikua uzembe wao kwenye kufunga filter. Na uzuri incharge alikubali kua alimpa kijana afanye ile service.

Japo kazi ilikua pevu, vikombe, craink shaft, hatari sanaa..

Nilijilaumu saaanaaa, kwanini sikuizima pale pale nilipoona taa, kwanini nilijiaminisha ningefika mwisho wa korongo. But it was too late.
Pole sana kaka
 
Back
Top Bottom