Natamani ningesoma huu uzi kabla ya September mwaka jana.
Nilikua na 1hz, hard top. Hapo ni kama siku 3 imetoka service, naenda zangu field. Baada ya km27 ikaniwashia hii taa, nikasema ngoja niikokote nimalize hili korongo niegeshe. Masikini weee....
Gari ilizima wakati napandisha lile korongo, na baada ya dk1 ndani kulikua kuna nuka ile harufu ile (kama limewahi kukukuta then unaijua ile harufu ya kuungua).
Ile kufungua bonet, ni imetapakaa oil tupuu, uvungu wa gari wote umejaa oil, nyuma kwenye spare tyre na vioo ni oil tupu.
Kumbe jamaa walifunga filter vibaya, ile rubber nyeusi ilikua imetwist, haikukaa sawasawa kwenye reli yake, upande flani imeweka seal, upande flan iko wazi. Kwahiyo pressure ya oil ilivyozidi, ikafumua palipo weak, yote ikaishia pale.
Ilibidi niwaangushie jumba lao bovu, tulisumbuana ila mwisho wa siku walifix kila kitu kwa gharama zao, maana ulikua uzembe wao kwenye kufunga filter. Na uzuri incharge alikubali kua alimpa kijana afanye ile service.
Japo kazi ilikua pevu, vikombe, craink shaft, hatari sanaa..
Nilijilaumu saaanaaa, kwanini sikuizima pale pale nilipoona taa, kwanini nilijiaminisha ningefika mwisho wa korongo. But it was too late.