DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Leo hii majira ya saa 11 jioni katika Block Namba 4 ghorofa ya Saba, Kota za Magomeni Jijini Dar es Salaam imeungua moto ambao chanzo chake, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni umetokana na mtoto kuchezea kiberiti.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa Kinondoni Mrakibu Msaidizi Jacob Chacha amesema katika moto huu uliotokea Magomeni Kota Block Namba 4 grorofa namba 7 kwa bahati mbaya mtoto anayekadiriwa kuwa na miaka 3 hadi 4 aitwae Ian Nyirenda inasadikiwa amefarikia dunia.

chanzo;EFM