Zimbabwe, 1994: Kwa jinsi wanafunzi walivyokuwa wanasimulia sio rahisi eti walikuwa wamesitiwa kutunga story ya kuona Aliens

Zimbabwe, 1994: Kwa jinsi wanafunzi walivyokuwa wanasimulia sio rahisi eti walikuwa wamesitiwa kutunga story ya kuona Aliens

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Miaka 30 baadae, nashawishika kuwa wanafunzi wale 62 wa miaka kati ya 6 hadi 12 katika shule iliyopo Zimbabwe waliona vitu ambavyo havikuwa vya dunia hii.

Ilikuwa ni asubuhi ya saa nne tarehe 16 mwaka 1994, wanafunzi hawa wakiwa break. Miongoni mwao walisema waliona chombo mfano wa ndege huku viumbe wenye macho makubwa wakitokea katika chombo hicho.

Tofauti na hapo kuna video pia ya interview ya rubani aitwaye chris zurinskas ambae anasema siku chache kabla ya tukio la hilo la wanafunzi shuleni na yeye pia akiwa angani maeneo karibia na shule hio aliweza kuona "UFO."


Haiwezekani watoto wa primary wadanganye in details na kwa uhakika. Kwa jinsi walivyokuwa wanasimulia stori zile sio kwa design ya mtoto akiwa anadanganya ila pale mtoto anapokuwa amepigwa na butwaa na ana mchechecheto wa kuhadithia.


Cha kushangaza hata miaka kadhaa kupita walipokuwa wamekuwa watu wazima bado waliendelea ku-stick na story yao hakuna aliesema kuwa tulipangwa tudunganye labda for bait, clout au umaarufu.

 
Back
Top Bottom