Zimbabwe ilikuwa na vikwazo vya kiuchumi lakini ilikuwa na bilionea kama Ginimbi

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Milionea wa Zimbabwe atazikwa na utajiri wake na watakaohudhuria kuvalia mavazi meupe.

Ginimbi Instagram

Marafiki wa milionea raia wa Zimbwabwe, Genius Kadungure aliyejulikana kama Ginimbi kwa muktadha wa kijamii, wamesema atazikwa na gunia lilojaa Dola, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Mfanyabiashara huyo aliyeishi maisha ya kifahari aliacha maagizo hayo kwa wanachama wa "all-white funeral", kama ilivyoandikwa na gazeti la Herald.

Ginimbi alifariki kutokana na ajali ya gari Jumapili, jijini Harare pamoja na mlimbwende Mitchelle Amuli aliyejulikana kama Moana.

GINIMBI GENIUS KADUNGURE

GINIMBI GENIUS KADUNGURE
Familia ya Moana imetaka fedha za mazishi kutoka kwa wanaowafariji.

Familia imeahirisha mazishi kwa wiki mbili ikisubiria majibu ya DNA na kukusanya michango ya kifedha kwa ajili ya kumuaga kwa heshima, imeripotiwa na Zim Morning post.

Matajiri wa Zimbabwe wamekuwa wakiahidi fedha kwa ajili ya mazishi ya Ginimbi.

Naibu Waziri Tino Machakaire ameahidi kununua jeneza kubwa kwa ajili ya Ginimbi, Mbunge Temba Mliswa amechangia wanyama wengi kwa ajili ya kuchinjwa kwenye mazishi hayo.

GINIMBI GENIUS KADUNGURE

GINIMBI GENIUS KADUNGURE
Wakati mwanasiasa Acie Lumumba ameahidi lita 1000 za mafuta ya dizeli, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani.

Ginimbi na Maona kwa pamoja walikuwa wanatoka kwenye sherere ya "all-white" ambapo gari yao iligongana na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao, ilichepuka nje ya barabara na kugonga mti kisha kulipuka moto.

Sherehe ya Ginimbi ya kuvalia mavazi meupe maarufu 'All White Party'
Ginimbi Genius Kadungure alijulikana kama mfalme wa mitindo mbali na kufanya sherehe kubwa.

Mwaka 2010 alifanya sherehe kubwa ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo waliohudhuria walivaa mavazi meupe maarufu kama all White party mjini Harare Zimbabwe , sherehe hiyo ilizungumziwa sana mjini humo.

Miaka miwili baadaye mwaka 2012 alisimamia maadhimisho ya siku nyengine ya kuzalia kwake.

Mwaka 2013, Ginimbi aligharamia sherehe ya siku tatu katika kijiji cha kwao huko Domboshava ili kusherehekea nyumba mpya aliyojenga katika eneo hilo.
 
Mwaka 2013, Ginimbi aligharamia sherehe ya siku tatu katika kijiji cha kwao huko Domboshava ili kusherehekea nyumba mpya aliyojenga katika eneo hilo

Credit: BBC
 
maisha mafupi ya raha hela za ndagu bwana kafa na miaka 36 so young
 
Alipataje utajiri huyu jamaa.
Alikuwa na kawaida ya kuendesha nagari ya kifahari kwa mwendo wa kasi, baba yake aliwahi kumuonya kuhusu tabia hiyo hatarishi lakini inaelekea Ginimbi alipuuzia ushauri wa baba yake, ndio maana babake alipo pata taarifa kwamba mwanae kafariki kwa ajali hakushangaa.

Inasemekana Ginimbi alifanikiwa kufungua mlango wa gari na kutoka nje baada ya kupata ajali - sasa katika harakati zake za kutaka kumuokoa mwanamke aliyekuwa nae kwenye gari pamoja na abiria wengine wawili Ginimbi alijaribu kufungua milango ya Gari lakini lock zikagoma kufunguka - baadae Gari likalipuka na kuwaunguza abiria wote pamoja na Ginimbi ambaye alikuwa tayari yuko nje ya Gari.
 
Daah hapa ile kauli ya kila nafsi itaonja mauti ndipo inapojidhihirisha
 
Gari inapata wapi ujasiri wa kulipuka kama sio ilikua na Full tank

huyu mtu anatembea na gari iko full tank,bongo huku magari yanabingirika

kama dunia kwenye mhimili wake na hayalipuki,tunatembea na wese kibaba tu

tukijisemea moyoni,yakipungua ntaongeza sheli pale mbele na tushukuru huu umaskini

wetu ndio unatusababisha tupumue hadi leo la sivyo tungekua na milipuko ya magari hii bongo mpk.
 
Wanaongea na kula bata?

[emoji23]mkuu,huko sasa ni nje ya mada,anyway kuna tafiti zinafanyika za kuzuia kifo,wazungu wameshafanya uhamishaji wa kichwa yani kichwa chako kinakatwa unapewa mwili mwingine hivyo basi mtu mwenye pesa atabaki kuwa na unafuu fulani siku zote,kuna yule mzee anaitwa warren buffet nadhani,angekuwa masikini yule angeshakufa zamani sana maana kafanyiwa heart transplant zaidi ya mara 2
 
Nipe mfano wa mtu mmoja ambaye alihamishiwa kichwa kutoka sehemu nyingine na kikafanya kazi.
Na kuhusu huyo buffet kufanyiwa hizo na akapona jua siku yake ya kufa bado haijafika,siku yake ikifika hayo mautundu yote yanafeli.
 
Back
Top Bottom