Zimbabwe: Mwanahabari aliyemkosoa Rais Emmerson Mnangagwa aachiwa huru

Zimbabwe: Mwanahabari aliyemkosoa Rais Emmerson Mnangagwa aachiwa huru

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Mnangagwa aachiwa huru
Nchini Zimbabwe, Mhariri wa Gazeti huru la Zimbabwe Independent Faith Zaba, aliyekamatwa wiki hii kwa kuandika na kuchapisha makala ya kumkosoa Rais Emmerson Mnangagwa, ameachiwa huru kwa dhamana.Mhariri huyo ameachiwa kwa Dola 200 na kutakiwa kuwasilisha pasi yake ya kusafiri Mahakamani jijini Harare.

Faith Zaba, mwenye umri wa miaka 55, alikamatwa siku ya Jumannne kwa kumdharau rais Mnangagwa.

Kichwa cha Makala aliyoandika, yalisomeka, wakati nchi inapoongozwa na kundi la watu wenye tabia za kihalifu, limeelezwa na serikali ya Zimbabwe kama kumdharau kiongozi wa nchi na kuwachochea wananchi dhidi ya kiongozi wao.

Akitoa hukumu ya kuachiwa kwa mhariri huyo, Hakimu Vakayi Chikwekwe, amesema masharti ya kupewa dhamana yanakubalika, lakini ametakiwa kuripoti katika kituo cha polisi kila Ijumaa hadi pale, kesi yake itakapokamilika.

Wanaharakati wa haki za binadamu, wamelaani kukamatwa kwa Zaba, kama mwendelezo wa kuwahangaisha wakosoaji wa serikali ya Mnangagwa, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2017.
 
Ingekuwa ni nchi ya Burundi, wangempoteza mazima.
 
Ingekuwa ni ile jamuuri ya mapopobawa angepakwa wese halafu wamrekodi ama wampoteze.
 
Back
Top Bottom